Madaktari wote waliogoma kufukuzwa kazi na utumishi!

Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?

Wala madaktari hawahitaji mshahara mkubwa kiasi hicho Ritz,wanachohitaji hasa ni kuboreshwa kwa mazingira yao ya kazi.
Sana serikali inataka kujiaibisha kwa kuanika kwa uzembe wake kw majirani zake wa EA.
 
Wachina wanaweza kuichukua hospitali nzima na hao wafanyakazi kulipwa na serikali yao ya uchina ,kuna madaktari kama milioni moja hawana kazi nchini China.


Wasiwalete madaktari kwanza hao wachina, watuletee kwanza rais na cabinet nzima ya uongozi wa serikali kwasababu tatizo lipo kwenye serikali na sio madaktari. Wakifanya hivyo tutawashukuru sana na watakuwa wametusaidia vya kutosha.
 
Wacha kuota ndoto za jioni wewe! Suluhu nini kila Dr mmoja serikali imlipe milioni 13 kwa mwezi?

Ila suluhu si kwa kuwafukuza utumishi...... huu ni unyanyasaji mkubwa! nahisi hapa patachimbika....mnafikiri madaktari wengine watatulia, au wananchi, hapa vita baridi itaanza, walahi tena.
 
Hao imported doctors huko wanakotoka wanatumia vifaa standard,dawa zipo na kila kitu kipo kwenye mstari..sasa ukiwaleta humu kwetu mtaibua mgomo mwingine maana ni likely watagoma kufanya kazi kwenye mazingira magumu na hatarishi..sidhani kama ni suluhu kufukuza madaktari kwa nchi inayohitaji madaktari sana kama yetu...
Kwenye hili serikali iache siasa,iwe makini na kutatua huu mgogoro..!!
 
Daktari mmoja anataka kulipwa Milioni 13 kwa mwezi come on!!

Ritz, hivi sisi hatuwezi kuendesha mambo kwa diplomasia? Hawawezi kulipwa hivyo but we could do something...hakuna kitu kibaya kama kuahidi kushughulikia tatizo halafu kila mtu anasahau yale aliyosema baada tu ya kumaliza makubaliano yenu ya kuanza kufanyia kazi. Napenda kujua, Serikali imefanyia kazi madai ya madaktari kwa kiwango gani ili tuone basi hata kama kuna dalili za kuonyesha kweli dhamira ya kutatua hayo matatizo ipo.
Vinginevyo hapa ni kutesa wananchi tu...
 
Last edited by a moderator:
Ccm ndo inafanya mgomo usiishe. kwanini hela za epa wasipewe madokta wakati swala lao linaendelea kushughulikiwa badala yake zinaenda kutekeleza ilani ya ccm tena bara tu?. sina imani na viongozi wa nchi. Mia
 
Daktari mmoja anataka kulipwa Milioni 13 kwa mwezi come on!!

mkuu sijui hizo habari uliitoa wapi sabab mimi nafaham wanadai 3.5M ...na madr wanajua kabisa serekali haitaweza kuwalipa hiyo pesa lakini wamesema hivyo ili endapo serekali ikiwapandishia mshahara ustofautiane sana na hiyo figure(let say 2.5-3.0)
 
Wachina wanaweza kuichukua hospitali nzima na hao wafanyakazi kulipwa na serikali yao ya uchina ,kuna madaktari kama milioni moja hawana kazi nchini China.

Halafu Tanzania itakapokuwa sehemu ya jamuhuri ya China mtaanza kusema nini?Mbona kila siku tunasema hatutaki ujamaa wala hatuwapendi wajamaa. Haya mambo ya tofauti ya kipato ndio chachu ya ubepari...na hii migomo ni sehemu ya kuendeleza ubepari huo huo. Zamani zile vipato vilikuwa vinakaribiana...siku hizi kila mtu anajitahidi kuongeza hela ya akiba kwa akaunti yake. Wao kama madaktari watatumia mbinu gani?
 
Kwa mujibu wa chanzo muhimu katika wizara ya afya, Serikali imejiandaa kuchukua hatu kali kwa madaktari wote waliogoma ifikapo kesho Ikiwa ''Ni pamoja kuwafukuza kazi na utumishi'' baada ya juhudi za Serikali na za Kimahakama ''KUTOHESHIMIWA''. Pamoja na hatua hizo pia taratibu za kuandaa madktari mbadala toka taasisi nyingine za Serikali ikiwa ni pamoja na uwezekano wakupata msaada wa dharura wa Madaktari toka mojawapo ya Nchi za Afrika Mashariki, zinaendelea vizuri. Aidha ulinzi nao unaendelea na utaendelea kuimarishwa katika sehemu na maeneo mbalimbali.

Kauli hii bila shaka ina underline tamko la Serikali leo Bungeni kuwa '' LIWALO NA LIWE''
una kifafa wewe, nenda kapimwe haraka kabla hujaharibikiwa
 
wewe upo upande gani.?

Hili swala sio la upande kuna ndugu zetu jamaa zetu na Watanzania kwa ujumla wagonjwa, wengine tunapongea wapo kwenye hodi wamelazwa kwa magonjwa tunachotakiwa kuepusha janga ili Watanzania wasipoteze maisha sasa unaponiuliza nipo upande gani sikuelewi.
 
Hii haiwezi kuwa kweli, as long as serikali imepeleka ishu mahakamani haiwezi fanya hivyo maana ni kuingilia uhuru wa mahakama...
 
Hili la kufukuza madaktari liko wazi. Lakini swali ni hili: will it solve the problem?

Issue ya madaktari ni ngumu sana kama serikali inadhani kuwafukuza ndio njia muafaka, kabla ya kutekeleza uamuzi huo iende kujifunza hapo Kenya walipotangaza kuwafukuza kazi walifanikiwa kwa kiwango gani? Mwisho wa siku waliwarudisha kazini wote bila masharti yoyote.

Hata uingereza juzi tu madaktari wamegoma na hatukusikia serikali huko ikitangaza kuwafukuza ama kwenda mahakamani. Walikaa kwenye meza ya mazungumzo na kuyamaliza.
Serikali yetu ijifunze kuzungumza na kuwa wakweli kutekeleza makubaliano, vinginevyo migomo hii haitakwisha kamwe hata kama watatumia nguvu nyingi na vitisho kiasi gani.
 
Back
Top Bottom