Sio kweli kabisa kwa sababu nakumbuka vizuri Jumuiya ya Wafanyakazi nchini TUCTA waliomba kuhusishwa, Chadema waliomba kuhusishswa wakiwakilishwa na mjumbe wetu Mnyika wote wakapigwa chini tena wakisisitiza kwamba hili sio swala la kisiasa wala hawataki kusaidiwa. Ni lao wao na watakwenda nalo sambamba.Mkuu mawazo ni mazuri sana lakini hilo haliwezekanio tz hakuna ushirikiano wa wafanyakazi na ndani ya wafanyakazi hao kuna system at work kwa hiyo mobilization ni ngumu sana bora hivyo walivyofanya ujumbe umefika japo kwa ghrama ya watz wenzao ilikuwa hakuna namna nyingine ya kufikisha ujumbe ispokuwa mgomo
Kama unakumbuka toka siku ile mimi sikukubaliana na PR yao, na baadaye taasisi ya haki za Binadamu ambao walikuwa wakijihusisha kulingana na kazi zao wakaandaa maandamano lakini hakuna jumuiya yoyote iliungana nao isipokuwa baadhi watu wachache sana.. Ni muhimu sana ukumbuke tu ya kwamba UNION zinaundwa kutambua na kulinda haki za wafanyakazi hasa ktk mfumo huu wa Kibepari na kama jumuiya hizi hazipati nguvu ya wananchi wenyewe kwa kupitia jumuiya hizi hakuna litakalo fanyika...
Kifupi tazama matatizo tulokuwa nayo tumeshindwa tu ku coordinate maanake Madaktari hawaridhiki na mishahara, walimu, Polisi, watumishi wote wa serikali ngazi za chini wote hawa wanalia na joto la jiwe kwa maisha magumu. Na wote hawa ni waajiriwa wa serikali iweje useme haiwezekani wakati wote wanapanga kufanya migomo wakisikilizia mgomo wa kwanza utatoa matunda gani?
Serikali hii sii wajinga, wanajua fika wakiwakubalia Tucta, wengine watafuata ndio maana JK akaweka ngumu lakini akipanga kuongeza mishahara chini chini, halafu Madaktari nao waliposikia posho za Wabunge wakaja juu..maana haingii akilini mbunge kuvuta karibu mil 7 kwa mwenzi wakati Daktari hafiki mil1.5 kwa mwaka. The only way out ni wananchi wenyewe kuwa kitu kimoja na muhimu zaidi ni kuonyesha kwamba mnathamini UTU (Humanity) hapo lazima mtazoa walalahoi.
Jambo moja baya sana lililotokea nchini ni kuzaliwa kwa Taifa jipya lililotengana - A Devided society - Mfumol uliopo tunatengeneza kundi la MATAJIRI na jingine la MASKINI kwa kugawana umaskini ambao mwenye nguvu ndiye anayekula nyama ktk sinia hili la biriani..
Madaktari wameshindwa kuelewa hivyo kwamba tupo kt process, transition of making millionaires in a poor country tofauti kabisa na nchi tajiri ambazo kuna utajiri na The rich getting richer through their investment and the poor getting poorer for not having Capital.
Sasa in the making ya Matajiri ndani ya umaskini hapa ni uwanja wa fisi..hakuna mtu anayejali profession ya mtu wala elimu bali nguvu ya kunyakua na obvious Politician are winners maan wako jikoni wao! Huwezi kushindana nao kwa madai kama ilivyo nchi za magharibi ambao wanajali profession ili kuboresha na kuimarisha investment zao ktk dunia hii ya ushindani.
Sisi bado tupo ktk Ujamaa wa kisiasa wakati wananchi wanaibiwa na hivyo Madaktari walitakiwa kutumia elimu zao kutambua kwamba njia pekee wanayoweza kushinda mgogoro huu ni kutumia vigezo vya HUDUMA..Kuonyesha hali za Wagonjwa na Mazingira mabaya ktk kutoa huduma za Afya na hapo kupata support kubwa ya wananchi walalahoi wakati mawaziri, makatibu wakuu na Wabunge wanatumia mabillioni ya fedha kwa posho na mafuta ya magari.
Na hakuna madai yoyote yanayoweza kuwekwa dhidi ya serikali yasiwe Political.. Hakuna. Unapoilaumu serikali ktk uongozi wake hata iwe mishahara ni lazima iwe political maana serikali ndio siasa yenyewe haiendeshwi bila sera. Let them say Chadema na CUF wamehusika kuweka madai ya huduma bora lakini mnapiga pale panapoumiza zaidi. Kam serikali itashindwa kukata matumizi yake yasiyokuwa ya lazima, kujipangia mishahara mikubwa na anasa za posho za vikao visivyokuwa lazima, safari zisizokuwa lazima, chai na kadhalika tunaweza kabisa kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi..
Bila shaka wananchi watajiunga nanyi, walimu, Polisi na watumishi wote nchini watagundua kumbe tunaliwa kiasi hiki! Hapo ndipo mwanzo wa mabadiliko ya jumla na sii mabadiliko ya kundi moja moja la watu kwa sababu uwanja wa fisi hauchaguwi profession ya mtu.
Na ndio maana kuna walalahoi ambao wanaona mshahara wa daktari wa Laki 9 na posho juu za Ths 20,000 kwa kikao ni mkubwa sana maana wao wanakula wali mkavu. Na mkisema Viongozi mbona hivi maa vile wanashindwa kuwaelewa kwa sababu wao wanajua viongozi ndio wako jikoni.. utauliza kweli shibe ya mpishi? au ugonvi wetu ni sisi tulokuwa janvini tukigombania nyama walizotuletea. Waheshimiwa ni wa kuheshimiwa na jukumu lao kubwa kuliko daktari kwa sababu ndio wanaogawa chakula, kwani hujasikia CCM wakitangaza kwamba wao ndio wanapeleka maendeleo kwa wananchi sio Chadema wala CUF?.
Narudia kusisitiza siku zote tazama WATU na MAZINGIRA kisha jenga PR yenye kulingana na sura kamili inayojitokeza mbele yako..Na kikubwa zaidi never underestimate power of the people!