MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
- Thread starter
- #21
Mkuu, pole sana kwa yaliyokukuteni!
Binafsi imenisikitisha sana.
Jumapili nilimpeleka mgonjwa aliyekuwa amevunjika mguu hapo.
Nikalipia 15,000 mapokezi kama gharama za kufungua faili na kulazwa..Cha ajabu daktari mmoja akaja akanivuta shati na kunipeleka kwa nesi mmoja sehemu ya faragha, akaniambia mbele ya nesi huyo kuwa nitoe elfu 5 za kumdungia sindano ya maumivu mgonjwa wangu, la sivyo sindano hiyo(diclofenac inj.) isingepatikana...nikacheka na kumpigia simu Dr ninayemfahamu, mambo yakaenda fasta!
Wasiojua taratibu na wasio na ndugu wanaumizwa sana hospitali ile!
Sidhani kama Mganga Mkuu Dr Toure anajua kinachoendelea hospitalini hapo, maana muda mwingi yuko Ofisini, Warsha, Kongamano, symposium, workshop, na kwenye LandCruiser la DFP(Hisani ya Merikani)...
I did'nt even waste my time to find Dr. Toure kwa sababu ni hao hao na siwaamini kabisa hawa kwani wote ni watoto wa mama mmoja. kama ulivyosema always Dr. toure yuko busy na Landcruiser lake la DFP hisani ya Wamarekani. Kwa ufupi PJ kama huna Dr. unayemfahamu hapo Mt. Meru hospital ni sawa na kujaribu kuomba huduma kuzimu.
They are extremely brutal utafikiri hawatakaa waugue. Ila niko sure kwamba maadam waliapa basi hicho kiapo ni sala kwa mungu na Mungu atawalipa kwa jinsi wanavyokiuka kiapo walichoapa kwa hiari yao wenyewe.