Madaktari watangaza kuendelea na mgomo, wasema propaganda haziwezi kufua dafu mbele ya ukweli

Wanaoendelea na mgomo wasiitwe madaktari - hawa ni wauwaji na mumiani wakubwa - madaktari vyeti hawa.

kwahiyo ni heri watu wafe kwasababu hamna vifaa wala dawa?, hawa watu (madaktari) wanakutana na vikwazo na shida nyingi huko mahospitalini am supporting them maana najua kama watapata wanavyo viitaji vitasave watu wengi sana kuliko wakitulia nawalivyo navyo sasa
 
Barnabas Shadrack
Au magonjwa ya kutibiwa kwa kutumia CT Scan ndiyo yamekuja mwaka huu?

Mkuu, wauaji wa wagonjwa kwenye hospitali zetu ni wengi kutokan na upungufu wa vifaa na vifaa tiba. Kutoa jibu tu kwamba maDr ni wabinafsi ni upuuzi wa hali ya juu. MaDr wamechoka kupuuzwa kwa kudhaniwa kwamba wanashindwa kutoa huduma bora kwa sababu zisizokuwa zao. Nimewai kutoa mfano hapa JF kwamba Dr anaweza vizuri tu kumuwekea mtu aliyezidiwa mashine ya kupumulia "ya Oxygen" na akaondoka ili aende kuwahudumia wagonjwa wengine. Kule kuondoka tu, TANESCO wakakata umeme na kusababisha mashine kuzima. Kisa? Hali halisi, ni mgao! Mtu anakufa. Au ili aweze kumfanyia upasuaji mgonjwa aliye mahututi lazima kuwe na vipimo vingi tu vya kufanyia uchunguzi na tahadhari na kama havipo ni vizuri kumuacha tu "liwalo na liwe" au kumwachia Mungu. Kitu kama hicho maDr wanaona shida sana. Masuala ya akiba ya damu kwa mfano, benki ya damu hakuna, sasa watu wanaotaka huduma ya haraka ya damu watapata wapi? Hospitali ziko hoi kiasi kwamba mgonjwa akipelekwa hospitali na hakuna ndugu wa karibu wa kugharimia matibabu au dawa kutoka famasi, hata kutoa damu, basi inakuwa ni bahati mbaya, anakufa wakati angeweza kuokolewa maisha yake kama huduma za afya zingeboreshwa. Hivi kwa nini serikali hailisemei swala hili na kubakia kung'ang'ana na kusemea kushindwa kuwalipa maDr mishahara mikubwa? Mgonjwa wa meno kwa mfano tu anapotibiwa meno Dr anapaswa avae "mask" kujiziba mdomo na pua angalao kuchuja hewa au tuseme moja kwa moja "mnuko" na uambukizo kutoka kwa mgonjwa (wengi wa wagonjwa wa namna hii hawajui afya ya meno na kinywa na mswaki kwao ni marafuku). Sasa walishaua viwanda vyetu na hizo "mask" tunaagiza kutoka nchi za nje. Sasa anapodai hiyo "mask" anaambiwa hakuna, akikataa kufanya hiyo operation munamwambia hana huruma, siyo mzalendo, mbinafsi, anaringa, anataka rushwa nk. MaDr wanajua kinga ni bora kuliko tiba. Angalao basi boresheni vitendea kazi vyao tu ili wajikinge na uambukizo, na wagonjwa hata kama wakikosa vipimo kama x-ray, hiyo scanner, huko laboratory nako nasikia hata "petri-dishes" hakuna, wanatumia maganda ya viberiti-we yaani waTz kweli tunaidharau tiba yetu na maDr wetu. Swala la kitaalamu linageuzwa la kisiasa. Na hao maDr wa kukodi watanufaika nini kwa kutusaidia sisi kama siyo kutufanya sisi ni simbilisi wa kufanyia mazoezi ya tiba zao? Mi naona afadhali tutibiwe na maDr wa kwetu hata kama watakosa uzalendo namna gani maana tukiumia tutalia sote na kuangamia sote pamoja kuliko kuletwa maDr wa kukodi. Namkumbuka sana Raisi Mkapa alipowahi kusema kwamba nanukuu, "Maradhi na Umasikini ni maadui wawili mapacha wanaowatesa waTz na Ujinga ndiye mama yao mzazi" Kwa watu kushindwa kuwaelewa maDr wetu ni sawa na kumpiga jeki mama huyo mzazi wa hao hao maadui wetu mapacha.
 
Wanaoendelea na mgomo wasiitwe madaktari - hawa ni wauwaji na mumiani wakubwa - madaktari vyeti hawa.

Usipate shida mkuu, humu humu JF kuna uzi unaitwa "Tamko la SIKIKA", humo umefanywa utafiti wa kina huduma ktk hospitali zetu kuanzia ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa hadi rufaa. Kwakweli hali inasikitisha. Mazingira ni magumu sana madaktari wanayofanyia kazi. Tuwaunge mkono huduma hizo ziboreshwe ndipo tuwanyooshee vidole wakigoma.
 
Siwaungi mkono kabisa maDr.

Mama yangu alivunjika mkono akafanyiwa operesheni ya kulipua pale MOI mkono ukaunga vibaya . Afu Dr mmoja kijana akatuambia tuchange laki saba anaweza kumsaidia. Mwingine akasema tumhamishie Fast Track . Tukaamua kwenda zetu Kibaha kwa Dr Barke. Wataalamu hawa sku hizi wanapenda noti kuliko madalali.

Sekta ya afya ni mojawapo ambayo imejaa rushwa hasa kwenye hospitali za umma.

Ninachoona hapa ni UBINAFSI mkubwa wa wataalamu wetu hawa na dharau kwa taaluma za watu wengine wasio matabibu.

Kelele hizi ni kwa vile madaktari wengi wameajiriwa sekta ya umma. Siku si nyingi sekta binafsi itashika hatamu na kila mtu atalipwa kwa nguvu ya soko.

Nawaomba maDr warudi kazini . Hawataki waache kazi. Serikali lazima iheshimiwe bila kujali nani anatawala. Acheni siasa. Au mnataka kufanya mapinduzi ya uongozi wa nchi? Semeni wazi kama ishu ni chuki dhidi ya serikali kwanini waadhibiwe watanzania masikini.
Anzisheni chama cha siasa basi au mkasajili MAT kwa Msajili wa vyama vya siasa muwaahudi waTz kuwa CT Scan zitakuwa za kumwaga mpaka kwenye dispensary tuwape nafasi kupitia sanduku la kura.

Vinginevyo mimi sioni logic ya kung'ang'ania mgomo ambao sasa hivi umeshakuwa nongwa wala hauna tija.
 
Back
Top Bottom