Madaktari watakiwa kusimamia maamuzi ya 3/3/2012; - Uongozi wa Mgomo wa Madaktari

Naona madr muweke wazi kwa nini hawa watu wawili mwataka wajiuzuru la Mponda tumeona kauli yake mbaya na mama Nkya mtujuze pls.
 
TAARIFA YA TATHMINI YA MGOGORO WA MADAKTARI TOKA TAREHE 03.03.2012
Uongoziunapenda kutoa taarifa kwa madaktari wote nchi nzima kuwa hali ya ushirikiano na umoja miongoni mwetu imeendelea kuimarika sana, hospitali mbalimbali zimeendelea kushiriki katika kushinikiza madai yetu kutekelezwa ili madaktari waweze kutoa huduma za afya.
Ni muhimu ikafahamika kuwa mpaka sasa Serikali haijatoa jibu la msing...i juu ya utekelezaji wa hatua muhimu ya kuendelea na mazungumzo, na hilo ni juu ya Kuwajibika kwa Waziri na Naibu Wazari wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa lengo la kupisha meza ya mazungumzo.
Pia tumepata taarifa kupitia vyanzo visivyo rasmi juu ya Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukutana na kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam, hivyo basi tuna imani Mhe, Rais atatumia hekima na busara katika kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu sasa.
Mwisho, tunapenda kutoa rai kwa madaktari wote kuendelea kusimamia maamuzi tuliyokubaliana tarehe tatu, kwa mabadiliko yoyote tutafanya sote kwenye kikao itakapobidi.

Imetolewa uongozi.
08.03.2012

Kwakuwa haya yalikuwa ni maazimio, ambayo hata Pinda aliutangazia umma kuwa ilikuwa sehemu ya makubaliano baina ya pande hizi mbili. Na kwakuwa Pinda alikuwa na taarifa kuwa mgomo utarejea endapo hilo kwenye "nyekundu" lilikuwa miongoni mwa yaliyopaswa kutekelezwa. Basi sicheleikusema, nami nawaunga mkono
 
Kudai haki ni kazi tukufu, na kuidai haki hiyo bila kuyumbishwa na tamaa ya kunufaika isivyo halali ni thawabu kubwa kwa Mungu. Sote tunajua Madiba alikuwa criminal no.1 lakini leo ni shujaa wa kila mtu, hata wale waliomdhihaki na kumuonea.
Vivyo hivyo kwa madaktari nawatakia heri katika mapambano yenu haya matukufu ili kesho dunia iwakumbuke kuwa mlisaidia kuimarisha sekta ya afya Tanzania, maisha yatakayopotea yatatumika kuboresha maisha mengi zaidi kwa sekta ya afya kufanyiwa marekebisho.
Mungu awasaidie msiyumbishwe na propaganda zinazoanza kupandwa kuwa hizi ni juhudi za kumdhalilisha rais Muislamu.
 
You are kidding yourself.

Ministers and other many government official are elected or apointed by President.They are people with regular minimum qualifications and many of them dont even qualify to be the bosses of their own families.
As far as CCM Government is concern my Dog of Chihuahua breed can make a very Good Minister of Health or even hold a position of Mr Pinda.
The biggest Job you have once you are elected to hold a position in any Ministry of CCM Government is To Do Nothing.
Just do nothing you will be hailed by all CCM comrades that you are "Mwenzetu" " Unakubalika" and "Umejipanga"
Hiiiiii! Hiiiii!
Who can not hold a position in CCM Government if the most important job is to do Nothing??

Who?

Even Emptiness of Vacuum can be apponted to hold a very important position in CCM Government and still do wonderful jobs.

Drs hassle and spend many sleepless night for many years to acquire their skills,know how and experience.
They have special and rare skills, that is a bitter truth which we have admit, they somehow Hold Mpini.

You can be in Jamhuri or Congo street right now and whistle so that the first 2 things to turn will be appointed Misters in the health Ministry. I am assuring you that the things will go there and do a better job more than 2 crooks we have right now in the Ministry.
However,the same is not True for Drs.
We dont elect or appoint Dr, I will say like Kikwete said about Teachers, Drs are Manufactured in a special foundry. Hiiiii! Hiiiii!

Mponda and Nkya can resign and Go to Hell and Rot nothing bad will happen to the Ministry of Health or our society.

But we can not afford to let Drs go because it is more than Too expensive.

At the same time we can not allow CCM to turn our government to a PLAYBOY CLUB.

Salute sire.......!
 
Mkuu,
Waziri na Naibu Waziri wa Afya wamezuia meza ya Mazungumzo kwa kitendo cha Waziri Mponda mwenyewe kutamka maneno haya kutoka kinywani mwake. Nanukuu: Mimi nawajibika kwa Wakulima na Wafugaji wa Jimbo la Ulanga wa Magharibi. Madaktari hawanihusu.

Sawa madaktari wameuliza kwa nni kasema hivyo?. Je, umefuatilia mfumo mzima wa utawala kulingana na madai ya madaktari kuona Huyu Waziri anahusika vipi maana ktk mchanganyiko wa Ujamaa na Ubepari wizara hasa za ELIMU na AFYA hazihusiki moja kwa moja na shughuli hizo. Simtetei waziri kwa maneno hayo lakini najua fika kwamba serikali imeshindwa swala hili kutokana na kuwepo wadau wengine katikati baina ya serikali na vyombo hivi vya huduma..Sio nyie mlosema serikali ilishindwa kuendesha Elimu na Afya ndio maana wakakabidhiwa CSSC kwa muafaka wa MoU iweje leo mnaitaka serikali iloshindwa ndio itoe suluhisho..

Hapa Canada tunategemea pia mgomo wa Ma pilot, lakini kuna mazungumzo yanaendelea baina ya wafanyakazi wa Air Canada wakiwakilishwa na Union na mwajiri wao Air Canada kwa muda wa miezi 18 hadi sasa hivi na yanahusu mishahara na mazingira ya kufanyia kazi. Waziri wa mawasiliano na Usafiri anachokifanya ni kuwa mediator tu, tena ni jana tu ktk taarifa ya habari alisema wazi kwamba bado anasubiri report toka pande mbili na ni matumaini yake watafikia maamuzi mazuri.
Waziri wetu hana mguu kabisa unless amealikwa na hata kama akienda kwenye meza ya mazungumzo hawezi kutoa maamuzi kwa sababu Air Canada ni shirika la serikali ndio, lakini lina mipango yake ya maendeleo na lina Board ya Wakurugenzi wake ambao ndio wenye maamuzi na nguvu ya kupitisha matumizi kutokana na bajeti waliyonayo. Waziri ataingilia tu ikiwa mazungumzo baina ya vyombo hivi yameshindikana na hivyo kuwa swala la Kitaifa. Mnataka waziri aingilie kati swala hili kama yale ya Lowassa na Richmond?

Nijuavyo mimi, ELIMU na AFYA kulingana na Muafaka wa MoU kimeundwa chombo kinachowakillisha serikali ktk swala hili na ndicho kinachotakiwa kutoa majibu kuhusu mishahara, posho na mikakati ya kuboresha huduma hizo kwa jamii. Rudi nyuma kasome muafaka ule halafu unambie nafasi wa waziri na naibu waziri na serikali iko wapi kama sio kuandika Policies tu za kuwezesha huduma hii iwafikie wananchi. Na hakuna kiongozi hata mmoja leo hii anaweza kuwagusa CSSC maana akijaribu ndio utakuwa mwisho wake. Sii JK wala nani wote wanakiogopa chombo hiki na ndio maana hakuna Mtanzania hata mmoja anakinyooshea kidole.

Juu ya yote haya, mliwachagua CCM tena mkitegemea kitu gani? madaktari wengi hawa ni pro CCM wao wenyewe walikipa kura zao na walichekwa matumishi wa serikali walipozimwa na JK kuhusishwa na siasa leo madaktari nao wanacheza karata ile ile ya kisiasa lakini hawataki Chadema, CUF, Bunge wala mahakama waingilie kama vile swala hili ni baina yao wao na serikali ya JK. Hakuna Umeme mnawasema Tanesco ili hali umeme wa dharura mipango yote imefanywa na JK na Lowassa, kaondolewa Msabah, na halaumiwi EL ila Tanesco ambao wanafanya kazi kwa hasara. Buzwagi mpango wa EL na Rostam kaondoka Karamagi yaani usanii mtupu kisha mnatafuta mabangusilo. Ebu msimame na kusema JK jiuzuru nitawaona wanaume kweli!
 
Mkandara,

Umeongea mambo ya msingi na umetoa mifano hai kushadidia hoja yako, well.

Lakini kuna mambo mawili ya kuzingatia katika mgogoro huu wa madaktari na serikali;

Moja, kujiuzulu ama kuondolewa wizarani kwa haji mponda na lucy nkya ni sehemu ya makubaliano ya awali kati ya madaktari na waziri mkuu, siku walipokutana na kukubaliana kumaliza mgomo ili mazungumzo yaendelee baina ya pande mbili, na siku ile ile pinda alitangaza kusimamishwa kazi kwa katibu mkuu blandina nyoni pamoja na mganga mkuu wa serikali deo mtasiwa, na akaeleza kwamba mamlaka ya nidhamu kwa waziri na naibu wake iko kwa raisi, atakaporejea nchini toka uswisi atamshauri awawajibishe ili kutekeleza makubaliano ya muafaka na hivyo kutoa nafasi ya kuendelea na majadiliano. Na kwakuwa katibu mkuu na mganga mkuu wameshawajibishwa, naibu waziri na waziri ni lazima wawajibike ama kuwajibishwa.

Pili, mkuu utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa serikali huku kwetu nchi za madongo kwinama ni tofauti sana na huko canada, sidhani kama huko marekani na ulaya waziri anaweza akatoa majibu ya kebehi kiasi hicho halafu aendelee kubaki katika ofisi za umma, sasa hapa kwetu wamezoea tu mtu anajisikia kuropoka tu lililomjia kichwani anaropoka. Kwanini waziri hakutafuta kauli nyengine ya kingwana dhidi ya madaktari, kwanini waziri alitoa taarifa ya uongo bungeni, kwanini waziri alipotosha umma kwa kutoa taarifa za uongo dhidi ya madaktari? je huko canada ndivyo mawaziri wanavyoshughulikia migogoro?

Mkuu katika hili, hakuna namna ya kulikwepesha ama kumtetea mtu, lazima mponda na nkya wang'oke kwanza kabla ya mazungumzo zaidi baina ya madaktari na serikali, hili sio shinikizo jipya ama dai jipya kama pinda anavyojaribu kuwahadaa watanzania, ni makubaliano ambayo yalitakiwa kutekelezwa na serikali tena yakisimamiwa na pinda!!
 
Mkandara....to cut you very short...umefanya vizuri kuja na parallel ya canada hapa....lakini umesahau kuzungumzia suala la msingi saaana kwa TZ la kujifunza toka kwa wenzetu walioendelea (e.g canada)..jambo hilo ni uwajibikaji wa viongozi pale wanapoonekana wamefanya kosa...Nasema uwajibikaji nikimaanisha kujiuzulu punde wanapoonekana kikwazo kwa mambo kufanyika au pale matatizo yanapoonekana kujitokeza kwa yale wanayosimamia....hili jambo(kujiuzulu)lipo nchi zoote zenye sense of responsibility kwa viongozi wao wanapoonekana kushindwa kufanya wajibu wao....iwe ulaya..iwe States,iwe Canada...Tukija hapa kwetu tunaona nini??.....kumekuwa na matatizo tele kwa baadhi ya mawaziri kuwajibika pale matatizo yalipotokea kwenye wizara zao...si afya peke...hili tumeliona kwenye madini na hata ulinzi...Kinachosimamiwa na madaktari hapa ni sehemu tu ya njia mojawapo ya kufikia utatuzi wa matatizo ya madaktari tz...madaktari wameona hawawezi kufanya kazi na viongozi ambao hawana imani nao na ili waendelee kufanya kazi wanataka hawa jamaa wawajibike wao wenyewe(bila kushinikizwa)na ikilazimika basi boss wao awawajibishe.....kumbuka asilimia kubwa ya watekelezaji wa sera za afya tz(na duniani kote) ni madaktari....wao ndio wenye kukabiliana na changamoto zilizoko kwenye ground zero.....sasa wao wamesema hawataki kusimamiwa na hawa mawaziri...waondoke kwanza ili kupisha hatua nyingine za utekelezaji wa demands nyingine na pia madaktari wakirejea kazini bila shida baada ya hatua hii....kitu hiki ndicho kinaonekana kigumu kwa watawala.....
Kama utakumbuka waziri mponda aliupotosha sana umma kwenye hotuba yake bungeni na hili lilithibitishwa na ile kamati ya bunge.....kwa hili tu kama angekuwa kwenye nchi zenye sense of responsibility kwa mawaziri wake mponda angeshajiuzulu.....ukijumlisha na jinsi yeye na dr.nkya walivyoshughulikia madai ya interns na ule mgomo wa kwanza...wote walitakiwa wawe wamejiuzulu....tena bila kusubiri kumweka rais kwenye stress zisizohitajika.....inasikitisha sana tz pale ambapo eti kujiuzulu kwa waziri kunategemea ridhaa ya rais....mimi naona hawa majamaa mawaziri wazembe wana take advantage saaana ya hii kitu......ifike mahali sasa viongozi wazembe wawajibishwe na wananchi bila kusubiri rais atoe ridhaa......kama ambavyo inafanyika nchi nyingine kama canada.......maana wananchi ndio walipa kodi na ndio wenye nchi.......na ndio wanaowaweka viongozi hawa madarakani(kwa njia ya kura)........
 
Mkandara,

Umeongea mambo ya msingi na umetoa mifano hai kushadidia hoja yako, well.

Lakini kuna mambo mawili ya kuzingatia katika mgogoro huu wa madaktari na serikali;

Moja, kujiuzulu ama kuondolewa wizarani kwa haji mponda na lucy nkya ni sehemu ya makubaliano ya awali kati ya madaktari na waziri mkuu, siku walipokutana na kukubaliana kumaliza mgomo ili mazungumzo yaendelee baina ya pande mbili, na siku ile ile pinda alitangaza kusimamishwa kazi kwa katibu mkuu blandina nyoni pamoja na mganga mkuu wa serikali deo mtasiwa, na akaeleza kwamba mamlaka ya nidhamu kwa waziri na naibu wake iko kwa raisi, atakaporejea nchini toka uswisi atamshauri awawajibishe ili kutekeleza makubaliano ya muafaka na hivyo kutoa nafasi ya kuendelea na majadiliano. Na kwakuwa katibu mkuu na mganga mkuu wameshawajibishwa, naibu waziri na waziri ni lazima wawajibike ama kuwajibishwa.

Pili, mkuu utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa serikali huku kwetu nchi za madongo kwinama ni tofauti sana na huko canada, sidhani kama huko marekani na ulaya waziri anaweza akatoa majibu ya kebehi kiasi hicho halafu aendelee kubaki katika ofisi za umma, sasa hapa kwetu wamezoea tu mtu anajisikia kuropoka tu lililomjia kichwani anaropoka. Kwanini waziri hakutafuta kauli nyengine ya kingwana dhidi ya madaktari, kwanini waziri alitoa taarifa ya uongo bungeni, kwanini waziri alipotosha umma kwa kutoa taarifa za uongo dhidi ya madaktari? je huko canada ndivyo mawaziri wanavyoshughulikia migogoro?

Mkuu katika hili, hakuna namna ya kulikwepesha ama kumtetea mtu, lazima mponda na nkya wang'oke kwanza kabla ya mazungumzo zaidi baina ya madaktari na serikali, hili sio shinikizo jipya ama dai jipya kama pinda anavyojaribu kuwahadaa watanzania, ni makubaliano ambayo yalitakiwa kutekelezwa na serikali tena yakisimamiwa na pinda!!
Hilo la kwanza, Pinda hawezi kusema atamfukuza waziri na Naibu waziri ktk mazungumzo ya mwanzo.. hana mamlaka hayo isipokuwa tuchukulie aliwaahidi atafikisha ujumbe huo...Lakini pia tuendelee kuamini kwamba JK alikataa kuwawajibisha Mponda na Nkya, kwa tuchukulie tena amefanya hivyo kwa sababu Mponda na Nkya wamewakilisha msimamo wa serikali...

2. majibu ya Mponda wala hayana ubaya kama utaelewa chanzo cha mazungumzo hadi yeye akafikia kusema vile. Je, ikiwa kama ni kielelezo cha kwamba yeye hana mamlaka ulitaka aseme nini?... anajua fika kwamba yeye ni mbunge na pengine hawezi kuwasaidia chochote ikiwa amri kutoka juu imekataa madai yao. Hii ndio niliposimama mimi lakini vijana wakachukulia kwamba yeye ana dharau. Na swala hili liliporudi kwa JK na Pinda pengine baada ya kuongea na waziri wakaona madaktari wetu ndio hawatumii busara..

3. Mfumo wetu unaweza kuwa tofauti na wa huku lakini ukweli unabakia kwamba kipo chombo kinachohusika na maendeleo ya AFYA na ELIMU nchini japokuwa serikali bado ina mguu ndani. Je, walifanya mazungumzo na chombo hicho na nini yalikuwa majibu yao!.. wamefikaje hapa sisi hatujui zaidi ya kusikia tu madaktari hawamtaki Mponda na Nkya hali utasikia madai haya yapo kwa miaka mingi.. Je Mponda na Nkya walikuwa mawaziri?..The all system sucks lakini sku zote tunatafuta mabangusilo.. Stand Up for your right - haitafuti bangusilo..

Na nimetoa mfano wa Tanesco, wamekabidhiwa kusambaza Umeme lakini bado serikali inawachagulia wazalishaji. Tanesco hawawezi kusema hatuwataki Symbion au IPTL, hawana maamuzi hayo na kutokana na ukweli huo hata yule jamaa yetu nani vile akaonekana jeuri na kuondolewa madarakani..Leo yuko wapi Ardhi na ni katibu mkuu maana hakuwa na kosa.

4. Sawa Mponda na Nkya lazima wajiuzuru lakini unachokitaka wewe kama Mtanzania ni nini? yaani madaktari warudi kazini? basi kesho watataka JK ajiuzuru pia na kila atakayekuja ambaye hakubaliani nao basi ajiuzuru. Siku zote meza ya mazungumzo ipo huru kwa pande mbili kuwa represented na watu wanaoweza kuwawakilisha. Madaktari hawawezi kuichagulia serikali nani awepo ktk meza ya mazungumzo, wameyafanya haya toka mwanzo wa mazungumzo ya awali wakiwataa Mponda na Nkya kuwepo ktk meza hiyo - WHY?..

Je, unataka kusema serikali nao wanaweza kusema hatuwataki mwakilishi wa madaktari namba 2,3 na 4 laa sivyo hakuna mazungumzo?. Jamani tumetoka ktk madai ya msingi leo tunaweka madai gani haya. Kama ingekuwepo kesi mahakamani au bungeni na huyu Mponda na Nkya ni washtakiwa ambao wametakiwa kujiuzuru ili kupisha uchunguzi ningeelewa na kuunga mkono madai hayo, lakini haya ni mazungumzo tu baina ya pande mbili kufikia suluhisho.. huwezi kumchagulia mtu mwingne nani amwakilishe, huu ni Upuuzi mtupu unafanyika. Watu watakufa kwa ushenzi wa madaktari kwa sababu kuwepo kwao ama kutokuwepo hakuwezi kubadilisha matokeo ya maamuzi ya serikili kuhusiana na swala hili, wala haitusaidii sisi wananchi kwa sababu tumeyaona huko nyuma.
 
nawasiwasi na ww kwenye hili la hawa mawaziri kujiuzulu labda una maslahi napo.
kadri unavyoeleweshwa hutaki kuelewa na unatumia utetezi ambao hauingii akilini,,,,,kuwa muwazi itakusaidia zaidi.
 
serikali na madaktari walikubaliana na kutia saini makubaliano kwamba mazungumzo baina yao yataanza pale wawili hawa watakapojiuzulu au kuwajibishwa.hivi ni sahihi kwa mgomo huu kwisha bila mtu kuwajibishwa?hata wakiendela kuwepo wizarani je watapata ushirikiano kutoka kwa madaktari?
 
Siku zote meza ya mazungumzo ipo huru kwa pande mbili kuwa represented na watu wanaoweza kuwawakilisha. Madaktari hawawezi kuichagulia serikali nani awepo ktk meza ya mazungumzo, wameyafanya haya toka mwanzo wa mazungumzo ya awali wakiwakataa Mponda na Nkya kuwepo ktk meza hiyo - WHY?

Je, unataka kusema serikali nao wanaweza kusema hatuwataki mwakilishi wa madaktari namba 2,3 na 4 laa sivyo hakuna mazungumzo?. Huwezi kumchagulia mtu mwingne nani amwakilishe, huu ni Upuuzi mtupu unafanyika.

Umeandika vizuri ila ulipofika hapa ukaanza kupoteza muelekeo! Madaktari hawajaichagulia serikali nani awepo kwenye meza ya Mazungumzo ila wamewakataa wajumbe wake (Mponda na Nkya) kwa sababu ya kukosa imani nao. Madaktari hawajataja mbadala wa Mponda na Nkya kwenye meza ya Mazungumzo kwa maana hiyo huwezi kusema eti wanaichagulia serikali muwakailishi wake.

Kukosa imani na Mponda na Nkya kulitokana na jinsi walivyokuwa wanaliposha Bunge na Umma kuhusu mgomo wa awali. Sasa kama toka awali tabia ya watu imejulikana kwamba ni wapotoshaji na mapropaganda, Je wakiendelea kuwepo kwenye meza ya mazungumzo una uhakika gani wataacha tabia hizo maana mueneza uongo mpropaganda ni kikwaza kwenye mazungumzo yoyote yale. Mtaongea mtakubalia Mshahara upandishwe hadi Tsh.1,900,000/= kwa mwezi yeye atatoka ataenda kuropoka kwenye vyombo vya habari Madaktari wanataka walipwe Tsh.10,000,000/= kwa mwezi. Sasa huyu ni mtu wa kufanya nae Mazungumzo??
 
Mkuu wangu kama Pinda atakuwepo ktk mazungumzo haijalishi kama Mponda na Nkya bado wapo madarakani, maamuzi yatatolewa ikiwa uwezo na fungu lipo/ halipo. Hawa mawaziri wamekatiwa fungu la bajeti na wao wakalipeleka kunakohitajika na hawana uwezo wa kuongeza fedha zaidi iwe ktk mipango ya maendeleo au matumizi ya ndani, hawana majawabu zaidi ya yale watakayo elekezwa.

Tabia yao haiwezi kubeza unachofikiria watasema nini baadaye, bali kimepitishwa nini ktk makubaliano. Hivyo hadi hapo watakapo kosea na kusema uongo ndipo utakapo wakemea kinyume cha ya hapo hizi ni tunzi za ngonjela.. Sisi wote hatujui serikali itafikia maamuzi gani ingawa tungependa sana waongeze mishahara na kuboresha sehemu za huduma. Nimesema toka awali kama madaktari wanataka kuweka mashtaka dhidi ya hawa mawaziri wafanye hivyo lakini sio kuipangia serikali nani abakie ktk madarakani ili mazungumzo yaendelee..Tuambieni makosa yao haswa ya maamuzi yao kinyume cha serikali tutawaelewa.

Hii kusema kweli ni chini ya mkanda wa majadiliano ya pande mbili..Na zaidi ya hapo hata wakiondolewa ktk nyadhifa hizo ndio itatusaidia nini sisi wananchi kama siii kutaka tu kuwakomesha. Hizi ni siasa za kukomeshana (majitaka) binafsi yangu sioni umuhimu wake hata kidogo hali maisha ya watu yapo hatarini. Aliondoka Msabah wizara ya madini tumeletewa Ngeleja hakuna jipya, mikataba ni ile ile na ufisadi wa CCM upo palepale...

Mimi nataka muwe wanaume kweli, msimame na kusema JK jiuzuru maana yeye ndiye mwanzo na yeye ndio mwisho aliyesema kwamba ndiye mwajiri wa wananchi ktk hotuba yake ya wazee mwka jana. Matatizo yote wanayodai madaktari majibu yake anayo JK sasa kwa nini mnashindwa kumwambia yeye ajiuzuru!..Maana ninavyoitazama picha hii inanipa wasiwasi mkubwa na shinikizo la kugoma madaktari, pengine CSSC inataka fedha zaidi na wanawatumia madaktari kugoma..Si waseme tu? My bad!.. who knows! Kifupi huduma za AFYA na ELIMU ni mbovu kupita kiasi, matokeo ya Form 4 mwaka huu na haya ya madaktari ni mavuno ya kile kilichopandwa..The all system ni mbovu ivunjwe!
 
Back
Top Bottom