Mti mkavu,
Nakuunga mkono sana.. Hali ilifikia kuwa mbaya sana kwa wagonjwa nchini na hakika wanaotetea Madaktari wa serikali kufanya kazi private wanashindwa kuelewa mfumo mzima ulivyokuwa mbovu. KJama hawa madaktari wanataka kuendesha biashara zao binafsi wafanye kazi huko full time na sio kuchukua wagonjwa wa hospital za serikali, kuwaghiribu kisha kuwalipisha gharama kubwa ktk Hospital zao binafsi ati ndiko kwenye huduma nzuri..The same person atakuwaje anahudumia vizuri kwake na siko alikoajiriwa?
Hapa hawa Madaktari wanachezea maisha ya binadamu kabisa, na kulipwa mishahara midogo sio sababu ya kutoa huduma hafifu ktk hospital za serikali..,mshahara mdogo acha kazi fungua yako na ufanye kazi vizuri sio kwenda Muhimbili ili mradi upate kuiba wateja baada ya kazi. Swala la walimu na viongozi ni swala linaloweza kutazamwa pia lakini kwa uangalifu zaidi ya madaktari kwa sababu hawa madaktari wamefikia kucheza na Uhai wa watu.
Hawakatazwi na mtu yeyote kufungua biashara zao binafsi na kutotegemea mshahara wa serikali lakini unapoajiriwa na serikali kisha muda mrefu unautumia ktk hospital yako hii inapunguza huduma za hospital za serikali na matokeo yake kila hospital ina pungukiwa madaktari. Yanayotokea leo hospitali za serikali hayatokani na ukosefu wa Madakari au madawa isipokuwa ni UFISADI wa Madaktari unaoharibu kabisa huduma nzima ya Afya nchini..
Kwa uhakika huduma za Hospital za serikali zmepungua kuliko wakati wowote toka tupate Uhuru.. Wanawake wajawazito wanakugfa kuliko wakati wowote, Malaria, Kufia kikuu ni magonjwa yanayotibika lakini yanaua kuliko hata Ukimwi.
Wanataka ushindani wafungue za kwao na watafute wateja na sii kuwachukua wale wasio na jinsi na kuwahadaa kwa maradhi yasiyoponyeka isipokuwa ktk hospital zao. Halafu sii kweli daktari anaweza kukutibu vizuri ktk zahanati yake kuliko Muhimbili hali kule hana vifaa vya kutosha, huu ni wizi mtupu na maranyingi wanaiba hata madawa na vifaa toka hospital za serikali.
Ikiwa shule au mwalimu sii mzuri unaweza kuondoka sahule hiyo at least mhudumiwa ana choice lakini sii ktk Maradhi. Hao viongozi wetu kufanya biashara ni swala la muda tu...Hili linaangukia ktk miiko na maadili ya viongozi (Siasa) na kama sikosei JK tayari alikwisha piga marufuku viongozi wa serikali kujihusisha na Biashara.. Aliwaomba wachague aidha siasa au Biashara, hivyo kama unamjua Kiongozi yeyote ngazi ya juu serikalini akijihusisha na biashara nadhani bila shaka huyu kiongozi anavunja sheria..Mahakama ya miiko na maadili imeshafunguliwa hivyo ni swala la ku report tu mtuhumiwa.
Generally speaking,tulipofikia ni pabaya mno..hali ya maisha sijui au ni kuendekeza(maana sisi wengine hatujaanza kuingia rasmi kwenye misukosuko ya life)imetufanya tu develop roho ya paka kiasi cha kutothamini kabisa utu na maisha ya mtu.For me,ni bora nisichukue hiyo dhamana ya kuajiriwa na yoyote kuliko ku play around na life ya mtu,ni hatari sana.
Nakumbuka lile sekeseke la mgomo wa ma daktari pale muhi2..dah,yaani jamaa walikuwa wanaenda kukusanya maiti tu wodini.Ni mtihani kwa kweli,mamlaka zote husika zinatakiwa kuwa makini,otherwise sisi vijana tuliopo mashuleni tunaanza kupata fikra za kushika njia kuliko kwenda kuingia kwenye lawama za kuua ndugu zetu