Madaktari wamuweka JK kikaangoni! Ni kuhusu uamuzi wa kumfukuza kazi Dr Mponda

Status
Not open for further replies.
Kwa hali ilivyo sasa inabidi JK achukue maamuzi magumu, vinginevyo akiwafukuza mawaziri kwa shinikizo la ma-Dr, ataendelea kupata mashinikizo kama haya kila wakati na kutoka nyanja tofauti.

Uamuzi mgumu ni; iwapo watagoma, awape ultimatum, wakipuuza awapige chini wote. Kisha atangaze nafasi za kazi za udaktari - dunia nzima iruhusiwe ku-apply kwa mkataba wa miaka miwili. Fedha za dharura (kama inavyokuwa wakati wa hali ya hatari) zitatumika kuwalipa hadi mawaziri wazalendo watakapopatikana kwa malipo ya kawaida. Wale waliofukuzwa wanaweza kuomba kurejeshwa kazini na watarejeshwa baada ya kukubaliana na masharti yatakayowekwa.

wataomba kazi, na watagoma tena.... it can be done, mwambie ajaribu
 
Nakubaliana na wewe lakini ujue ULIMBOKA sio MGAYA! Na kama ndio mnamshauri mh. rais hivyo mjue wananchi watamfukuza pale ikulu!

Halafu ujue tackling ya mgomo wa madokta ni tofauti na migomo ya kisiasa unajua kuwa nitaandaa polisi au hata jeshi kuhakikisha kesho hakuna maandamano!

Madokta wakishapitisha maamuzi yao wao wanabaki majumbani kwao na kusikilizia fukuto likoje huko nje hujui umkamate nani na umwache nani!!!!

Ok, unaweza ukasema utawalob viongozi wao lakini mpaka saizi bado wanaonyesha wapo ngangari kabisa.
 
Ni mategemeo yetu wananchi kuwa hatua madhubuti zitachukuliwa bila kuathiri huduma mahospitalini. Hili ni shinikizo na siku zote serikali haifanyi kazi zake kwa kushinikizwa na kundi fulani la watu.

VGL ni hatua zipi madhubuti ambazo zilishindwa kuchukuliwa kipindi kile saizi zinategemewa kuchukuliwa?
Tuache kujifariji, tusolve tatizo badala ya kuendekeza malumbano. Mponda na Nkya wang'oke, tukubali shinikizo hilo lakini liwe angalizo siku zijazo.
 
Kwa hali ilivyo sasa inabidi JK achukue maamuzi magumu, vinginevyo akiwafukuza mawaziri kwa shinikizo la ma-Dr, ataendelea kupata mashinikizo kama haya kila wakati na kutoka nyanja tofauti.

Uamuzi mgumu ni; iwapo watagoma, awape ultimatum, wakipuuza awapige chini wote. Kisha atangaze nafasi za kazi za udaktari - dunia nzima iruhusiwe ku-apply kwa mkataba wa miaka miwili. Fedha za dharura (kama inavyokuwa wakati wa hali ya hatari) zitatumika kuwalipa hadi mawaziri wazalendo watakapopatikana kwa malipo ya kawaida. Wale waliofukuzwa wanaweza kuomba kurejeshwa kazini na watarejeshwa baada ya kukubaliana na masharti yatakayowekwa.

Awapige chini madaktari wote kwa ajili ya kuwalinda wateule wake wawili? Wewe mtu wa ajabu sana au wewe ni Kikwete mwenyewe maana Mtanganyika wa kawaida hawezi kutoa ushauri wa namna hii.
 
Ukweli ni kuwa serikali ya JK ipo kikaangoni kuhusu madai yaliyotolewa jana na madaktari kumpa hadi Jumatano awe ameshawafukuza waziri wa afya Dr. Haji Mponda na naibu wake Lucy Nya kwa madai hao ni wabaya wao na bila kiburi chao labda mgomo ule usingefika pale ulipofikia na tayari waziri mkuu alishatekeleza wajibu wake wa kumfuta kazi katibu mkuu wa wizara hiyo na kumtupia kiporo kilichobaki JK.

Huo unaonekana ni kama mtego endapo rais atatii maagizo hayo baada ya madokta kusema hivyo. Ni bora rais angemfukuza kipindi kile kile Dr. Mponda na naibu wake hali ingekuwa shwari lakini tabia ya kusubiri kupima upepo ndiyo iliyomfikisha hapo JK kupewa shinikizo!

Hivi sasa kauli hiyo ya madokta inajadiliwa na maafisa usalama ili waone jinsi watavyomshauri rais vizuri. Katika majadiliano hayo bado chanzo cha madaktari kufikia hatua ya kutoa shinikizo kama hilo hakijajulikana ni nini hasa? Wachambuzi hao wanachelea kusema isije leo ikawa kwa waziri wa afya na naibu wake kisha rais akawafukuza halafu kesho wakasema tutagoma endapo waziri mkuu hataondolewa madarakani kwani nae ni mchawi katika mgogoro wetu!!!

Hilo ndilo linaloiimuza serikali ya JK.

Mgomo wa madaktari sasa utazidi kuwa shubiri katika wakati huu ambayo mambo hayajatengamaa serikalini kifedha.

Madai ya madaktari ni mengi na karibu yote yanahitaji fedha jambo ambalo linazidi kuongeza ugumu.

Nawasilisha.

Hawa wana-usalama walikuwa wapi siku zote? Nadhani kama wangekuwa wanafanya lazi zao vizuri, kwanza hata huu mgomo usingetokea, na hata baada ya kutokea na kufikia muafaka, walikuwa wapi kufahamu kuwa haya maamuzi ya madaktari lazima yangefika hapa ikiwa kama mambo kama ya kuwawajibisha hao mawaziri hayakufanyika? Napata shida sana na hao wanaoitwa wana usalama, na ninaona pia kuna uwezekano mkubwa kabisa nao wakawa wameingia ktk vita hii ya makundi ndio maana mambo hayaendi.

Kwa vile Serikali imeonekana kulegea kabisa, basi hakuna ujanja ni lazima ipate shinikizo kama hilo ili itoe maamuzi, na kila siku bila mashinikizo Serikali nyingi za Africa zinakuwa hazieleweki. Na kama madaktari watakuja na mashinikizo mengine, sawa tu, ili mradi yana manufaa kwa watanzania.

Pili, ktk kila historia ya mabadiliko, huwa kunakuwa na Agent of Change, na kwa Tanzania, kutokana na historia yetu ya kimaisha na jinsi Mwalimu Nyerere alivyotukuza na kutufunza, sisi wananchi kuwa change agent ni kazi kidogo.

Kwa nchi kama yetu, professions can be agent of change, na hapa nazungumzia fani kama hawa madoctor wetu, walimu na kadharika. Kwa hapa tulipofika, naona kabisa, madaktari wanaweza kuwa agent of change kwa Tanzania.

Mimi nilisema mwanzo na naendelea kusema, nawaunga mkono, nawaomba wabebe jukumu hili la kuwa Agent of change kwa niaba ya watanzania wote, bila kujali itikadi zao. Nawaomba madaktari, wakisha inyosha serikali kwa masuala yaliyopo ktk sector ya Afya, wahamie na sector nyingine kama Walimu nk. Watusaidie kuleta haya mabadiliko, wanaweza kuja na hoja kuwa wao kama madoctor wamefika hapo walipo kwa ajili ya walimu, sasa kama walimu wasipotekelezewa maslahi yao basi wao wanaitisha mgomo tena.

Wakimaliza hapo waje kwa watumishi wazembe na hasa mafisadi Serikalini, waseme, haiwezekani watu wachache watumie rasilimali za nchi kwa manufaa yao pekee, wakati watanzania wengi wanakufa kwa kukosa dawa na hospitali za kutosha, basi waseme wanataka watu wote waliotuhumiwa kwa ufisadi wafukuzwe kazi na wakamatwe na wafikishwe ktk vyombo vya sheria, na waitishe mgomo kama Serikali haitaka kufanya hivyo.

Wakimaliza hapo waende katika sector nyingine, mpaka wamalize zote. Nadhani Madaktari wanaweza kututoa hapa na kutupeleka mahali pengine bila hata kutumia vyama vya siasa.

Tena wanapotoa hayo mashinikizo watoe na timeframe, kama vile wanavyo-prescribe dawa zao kwa mgonjwa, 2X3 kwa Wiki Moja, au 1x1 for two weeks au etc etc. Basi waipe serikali time frame kama dozi za dawa, kama walivyofanya hili la sasa, kwamba mpaka J5 hao mawaziri wawe wameondoka - dozi safi sana kama ya dawa ya siku tatu.

Hongereeni Madaktari na naomba mlifikirie wazo langu la ninyi kuwa agent of change na watanzania tuwape support hawa. Aluta continua!....
 
Kwa hali ilivyo sasa inabidi JK achukue maamuzi magumu, vinginevyo akiwafukuza mawaziri kwa shinikizo la ma-Dr, ataendelea kupata mashinikizo kama haya kila wakati na kutoka nyanja tofauti.

Uamuzi mgumu ni; iwapo watagoma, awape ultimatum, wakipuuza awapige chini wote. Kisha atangaze nafasi za kazi za udaktari - dunia nzima iruhusiwe ku-apply kwa mkataba wa miaka miwili. Fedha za dharura (kama inavyokuwa wakati wa hali ya hatari) zitatumika kuwalipa hadi mawaziri wazalendo watakapopatikana kwa malipo ya kawaida. Wale waliofukuzwa wanaweza kuomba kurejeshwa kazini na watarejeshwa baada ya kukubaliana na masharti yatakayowekwa.
umeongea kirahisi sana mkuu, wewe unafikiri kwa nini ule mkwara wa bwana pinda wa ultimatum ya 48hrs haukufanya kazi?akitumia ubabe tu kaumia vibaya mno. We unafikiri kuwafukuza madokta ni kitu rahisi kama unavyoongea?
 
Kuna namna moja ambayo imebakia kulinda heshima ya Rais ni kwa wahusika kujiuzulu kabla ya jumatano.
 
taarifa za ndani kabisa za kikao zinasema madaktari wamesikitishwa na vitendo vya serikali kutoa taarifa za upotoshaji dhidi ya madaktari.mfano uliotolewa ni ile taarifa ya ofisi ya waziri mkuu iliyosema madaktari walisusia kikao.

Nadhani kwa sasa serikali haina ujanja zaidi ya kufanyia kazi mahitaji ya madaktari.propaganda hazitaondoa tatizo!
 
Hawa wana-usalama walikuwa wapi siku zote? Nadhani kama wangekuwa wanafanya lazi zao vizuri, kwanza hata huu mgomo usingetokea, na hata baada ya kutokea na kufikia muafaka, walikuwa wapi kufahamu kuwa haya maamuzi ya madaktari lazima yangefika hapa ikiwa kama mambo kama ya kuwawajibisha hao mawaziri hayakufanyika? Napata shida sana na hao wanaoitwa wana usalama, na ninaona pia kuna uwezekano mkubwa kabisa nao wakawa wameingia ktk vita hii ya makundi ndio maana mambo hayaendi.

Kwa vile Serikali imeonekana kulegea kabisa, basi hakuna ujanja ni lazima ipate shinikizo kama hilo ili itoe maamuzi, na kila siku bila mashinikizo Serikali nyingi za Africa zinakuwa hazieleweki. Na kama madaktari watakuja na mashinikizo mengine, sawa tu, ili mradi yana manufaa kwa watanzania.

Pili, ktk kila historia ya mabadiliko, huwa kunakuwa na Agent of Change, na kwa Tanzania, kutokana na historia yetu ya kimaisha na jinsi Mwalimu Nyerere alivyotukuza na kutufunza, sisi wananchi kuwa change agent ni kazi kidogo.

Kwa nchi kama yetu, professions can be agent of change, na hapa nazungumzia fani kama hawa madoctor wetu, walimu na kadharika. Kwa hapa tulipofika, naona kabisa, madaktari wanaweza kuwa agent of change kwa Tanzania.

Mimi nilisema mwanzo na naendelea kusema, nawaunga mkono, nawaomba wabebe jukumu hili la kuwa Agent of change kwa niaba ya watanzania wote, bila kujali itikadi zao. Nawaomba madaktari, wakisha inyosha serikali kwa masuala yaliyopo ktk sector ya Afya, wahamie na sector nyingine kama Walimu nk. Watusaidie kuleta haya mabadiliko, wanaweza kuja na hoja kuwa wao kama madoctor wamefika hapo walipo kwa ajili ya walimu, sasa kama walimu wasipotekelezewa maslahi yao basi wao wanaitisha mgomo tena.

Wakimaliza hapo waje kwa watumishi wazembe na hasa mafisadi Serikalini, waseme, haiwezekani watu wachache watumie rasilimali za nchi kwa manufaa yao pekee, wakati watanzania wengi wanakufa kwa kukosa dawa na hospitali za kutosha, basi waseme wanataka watu wote waliotuhumiwa kwa ufisadi wafukuzwe kazi na wakamatwe na wafikishwe ktk vyombo vya sheria, na waitishe mgomo kama Serikali haitaka kufanya hivyo.

Wakimaliza hapo waende katika sector nyingine, mpaka wamalize zote. Nadhani Madaktari wanaweza kututoa hapa na kutupeleka mahali pengine bila hata kutumia vyama vya siasa.

Tena wanapotoa hayo mashinikizo watoe na timeframe, kama vile wanavyo-prescribe dawa zao kwa mgonjwa, 2X3 kwa Wiki Moja, au 1x1 for two weeks au etc etc. Basi waipe serikali time frame kama dozi za dawa, kama walivyofanya hili la sasa, kwamba mpaka J5 hao mawaziri wawe wameondoka - dozi safi sana kama ya dawa ya siku tatu.

Hongereeni Madaktari na naomba mlifikirie wazo langu la ninyi kuwa agent of change na watanzania tuwape support hawa. Aluta continua!....

Heshima yako mkuu. Natambua kiu iliyopo moyoni mwako ya mabadiliko lakini ukweli ni kuwa kila kada inapaswa kuwa agent of change.

Hebu fikiria mwalimu analipwa chini ya Tshs 200,000.00 na siyo hao tu hata hawa walinzi wetu kama polisi nao wapo hoi kimalipo lakini mfumo wao wa kudai haki zao ni mgumu kuliko madokta. Nakumbuka Kenya askari Magereza waligoma na madai yao yalisikilizwa mara moja.

Huku kwetu polisi kila siku wapo na rais lakini hawajaliwi na siyo hao tu bali tabia hii imekwenda mpaka kwa madokta ambao wao wameamu kusema No.
Tukisema No kwa pamoja inawezekana,
 
Kwa hali ilivyo sasa inabidi JK achukue maamuzi magumu, vinginevyo akiwafukuza mawaziri kwa shinikizo la ma-Dr, ataendelea kupata mashinikizo kama haya kila wakati na kutoka nyanja tofauti.

Uamuzi mgumu ni; iwapo watagoma, awape ultimatum, wakipuuza awapige chini wote. Kisha atangaze nafasi za kazi za udaktari - dunia nzima iruhusiwe ku-apply kwa mkataba wa miaka miwili. Fedha za dharura (kama inavyokuwa wakati wa hali ya hatari) zitatumika kuwalipa hadi mawaziri wazalendo watakapopatikana kwa malipo ya kawaida. Wale waliofukuzwa wanaweza kuomba kurejeshwa kazini na watarejeshwa baada ya kukubaliana na masharti yatakayowekwa.
kama wanakosa laki saba za mainten wa nje atawamudu kweli? Kumbuka ma dr. Kutoka nje watadai zaidi ya 3.5m ambazo zimependekezwa na ma dr. Wa hapa na selikalikali haina pia hao wa nje watadai nyumba,usafiri na bima za afya
 
Kuna namna moja ambayo imebakia kulinda heshima ya Rais ni kwa wahusika kujiuzulu kabla ya jumatano.

Mkuu hata mimi nashangaa kabisa! Na mshangao mkubwa uko sio kwa Rais bali kwa hao mawaziri wanaong'ang'ania ofisi kana kwamba wamezaliwa kuwa mawaziri. Waachie ngazi kulinda heshima ya serikali na Mkuu wa Nchi.

A very simple statement isiyozidi hata dakika mbili mbele ya waandishi au vyombo vya habari inatosha kabisa kumaliza mzizi wa fitna na kutuepusha na kadhia hii. Mbona hata enzi za Mwalimu ilikuwa hivyo? Leo inashindikana nini? Ya nini kusubiri hadi wafukuzwe? Hebu watumie hekima watuachie nchi yetu salama.
 
naomba kuuliza .Hivi JK anaogopa kuonana na madaktari? Kwa nini asitoke ikulu aende moja kwa moja muhimbili wakafanye mazungumzo ya ana kwa ana na hisi hii itaweza kusaidia.kwa wakati mwingine mbinu hii huwa inasadia.kuliko kusubiri taarifa muda wote.watawala wetu bwana taabu kweli yaani.
 
Kwa hali ilivyo sasa inabidi JK achukue maamuzi magumu, vinginevyo akiwafukuza mawaziri kwa shinikizo la ma-Dr, ataendelea kupata mashinikizo kama haya kila wakati na kutoka nyanja tofauti.

Uamuzi mgumu ni; iwapo watagoma, awape ultimatum, wakipuuza awapige chini wote. Kisha atangaze nafasi za kazi za udaktari - dunia nzima iruhusiwe ku-apply kwa mkataba wa miaka miwili. Fedha za dharura (kama inavyokuwa wakati wa hali ya hatari) zitatumika kuwalipa hadi mawaziri wazalendo watakapopatikana kwa malipo ya kawaida. Wale waliofukuzwa wanaweza kuomba kurejeshwa kazini na watarejeshwa baada ya kukubaliana na masharti yatakayowekwa.

Sijawahi kusikia ushauri wa ajabu namna hii! Watapatikana wapi madaktari ambao leo wamekaa bila kazi ili wawe recruited at short notice kuja Tanzania kuziba pengo la hawa unaopendekeza wafukuzwe (na kwa lengo la kipumbavu kabisa la kuwalinda useless people)?
Katika hali ya kawaida unaweza tu kumtoa mtu kwenye ajira aliyopo kwa kumlipa mshahara mkubwa zaidi ya anaolipwa. Sasa kama unashindwa kuwalipa posho ya elfu 30 madaktari ulionao utaweza kulipa dola elfu 30 ukiachilia mbali relocation costs?
 
Mimi nilisema hao madaktari wakikubaliwa kila wanachokisema mwisho watasema hatumtaki waziri, na wakikubaliwa watasema hatumtaki waziri mkuu au Rais.

Fukuza wote hao, leta wa cuba na wachina na wahindi, wamejaa kibao.
wanashindwa kulipa laki saba za maintern wataweza kuwalipa hao madaktari wa cuba au unaropoka tu?
 
Nimekuwa nikifuatilia sana mgogoro wa madaktari na Mh Pinda,alipo kuwa pale cpl aliwapa ahadi kuwa baada ya week mbili atakuwa wamepata majibu ya madai yote,madaktari kwa kuheshimu na kuzingatia utu walikubali kwa sharti lakutimiziwa madi yao kwa maana kuwe na makubaliano ya pamoja na kwa yale ambayo hayataweza kutatutliwa kwa sasa basi pawe na muda maalum.
Moja ya madai ambayo nilishtuka ni hawa wataalamu wetu walikuwa wanataka wapewe chanjo ya Hepatitis ugonjwa hatari sana unao shambulia ini (liver),nikajiuliza hivi hata kuwakinga hawa wataalamu unahitaji mjadala? Tunao madktari wangapi katika nchi hii.
Nchi yetu ni kati ya nchi zenye wataalamu wachache sana angalia hapa ,Tanzania kwa tanzania ni 2 per 100,000. (mwaka 2006)

DOCTOR TO PATIENT RATIO IN AFRICA

whereas the recommended (tunashauriwa kufikia by WHO) rate is 1 : 7,500.

Mwaka 2007 Tulikuwa wa mwisho angalia hapa http://bigthink.com/ideas/21237

Sasa Mh Pinda unapowazungusha hawa wataalamu unamaanisha nini kwa Taifa hili,umekuwa ukisema wewe ni mtoto wa mkulima hivyi ndivyo watoto wa wakulima wenzako unvyowafanyia. PMO wako mbona anaibuwa matatizo mapya badala ya kuwapa waraka wanouhitaji wewe unasema wamewabagua kada nyingine.

Mbona madai ya madaktari yalikuwa kwa maandishi sas kwa nini serikali haitaki kuwa majibu kwa maandishi?

Ndugu wa JF natoa ahadi kuleta mambo yaliyo jificha nyuma ya pazia, Wizara ya Utumishi wana kashfa kubwa nitaileta nikipata habari kamili.

Tukiendelea hivyi na pata wasiwasi na mstakabali wa Taifa.
 
Huitaji kuwa na PHD kuliona hilo lakini kulitolea uamuzi linaweza kuwa na vikwazo kwa sababu ya kulindana. Nasubiri kuona hekima ya JK kama atakubali kuona nchi inaingia tena katika mgomo wa madokta kisa watu wawili.

We unaongelea watu wawili, kwa JK hata mtu nusu yuko tayari nchi iangamie ili huyo mtu nusu abaki salama!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom