Madaktari Waliogoma Kukutana Leo Jumamosi- Tafsiri Yangu

Mbona sijawahi kusikia tafsiri ya Maggid kuhusu viongozi kutibiwa nje? Hawa waandishi wetu wana matatizo sana wanajadili vitu basic na kuviita tafsiri zao.
 
Nashindwa kuelewa unafiki ama huenda niite fikra finyu za baadhi ya waTanzania ktk kutathmini hali halisi ya mambo yanayotukabili ktk sekta zetu mbali mbali hapa nchini.

Hukumu inayotolewa na viongozi wa nchi pamoja na baadhi ya waTanzania kwa madaktari wetu kutokana na mgomo wao eti wanasababisha vifo kwa wananchi wasio na hatia, naona ni hukumu potofu tena iliyokosa mantiki kabisa. Hebu tutafakari kwa kina hiyo idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha ktk kipindi cha wiki tatu za mgomo wa madaktari kwa kukosa huduma na tuijue idadi hiyo ni watu wangapi. Nadhani inasemekana kuwa ni wagonjwa 250 ndio walipoteza maisha kwa kukosa huduma. Ni jambo la kusikitisha sana hata mimi silifurahii kabisa.

Lakini kwa upande mwingine, hebu tuangalie ni idadi ya wagonjwa wangapi hufa mikononi mwa madaktari, hata wakati mwingine madaktari bingwa kwa sababu tu ya kupata huduma isiyotosheleza na sio kwa muda wa wiki tatu tu kama walizogoma madaktari, bali kwa miaka nenda, miaka rudi, kwa miaka yote 50 ya uhuru, na kuwa mbaya zaidi siku hadi siku. Idadi yake inatisha. Nenda wilayani ukaone huduma za matibabu wanazokosa wagonjwa kwa sababu tu pengine eti mashine ya xray imeharibika na ni kwa muda mrefu, yaweza kuwa hata miezi minne iliyopita kama siyo sita kabisa.
Nyuzi za kushonea baada ya upasuaji, gloves za kuvaa mikononi, gouze za kutumia wakati wa upasuaji kuzuia damu, mpaka hata bandage za kufungia vidonda.
Zahanati zinakosa hata taa za fanusi na vibatali vinakosa mafuta ya taa mpaka wakina mama wanazalia gizani. Usiliguse kabisa swala la dawa, maana karibu zote za muhimu hazipatikani.

Unategemea madaktari wetu wafanyeje kazi ya taaluma yao? Hivyo wanavyojitahidi hata maisha ya baadhi ya wagonjwa yakaokolewa niseme ni miujiza tu na kudra za Mwenyezi Mungu.

Amani haiji ila kwa ncha ya upanga. Wanachokifanya madaktari wetu sasa, ni kuwatoa muhanga watu wachache ili watu wengi zaidi wapone. Kila jambo zuri lina gharama zake, ndiyo maana hata nchi zingine zimegombania uhuru kwa kumwaga damu. Badala ya kuwahukumu na kuwalaani madaktari wetu, ingefaa kuwapongeza na kuwasifu kwani kitendo chao ni cha kizalendo na cha kishujaa. Mfumo mbovu wa wizara ya afya na watendaji wake ndivyo vya kulaumiwa.
 
Mkuu JouneGwalu, tunawaheshimu sana madaktari ila kwa wengine wetu mimi nikiwemo, tunathamini zaidi uhai wa binadamu yoyote na uhai wa Mtanzania ndio unatakiwa uthaminiwe na Mtanzania mwingine yoyote achilia mbali yule aliyekula kiapo cha to "save lives" no matter what!.

Wengi wanasupport madakitari na hata mimi binafsi nakiri madai yao ni genuine but there are many routes to Rome, hiyo njia waliotumia kuleta siasa na kutaka kutumia human shield ya innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali, is a wrong way!. Yes wadai haki zao but not at the expence of poor ordinary innocent Tanzanians!.

Hapo umenena;kwa mahana wanachokifanya madakatali akina tofauti na magaidi walioteka watu wasio na hatia wanaua mmoja mmoja mbaka watimiziwe madai yao,utalatibu huu wa madai haukubaliki watafute njia nyingine ya kuibana serikali siyo kwa kuwaua binadamu wenzao
 
Mkuu JouneGwalu, tunawaheshimu sana madaktari ila kwa wengine wetu mimi nikiwemo, tunathamini zaidi uhai wa binadamu yoyote na uhai wa Mtanzania ndio unatakiwa uthaminiwe na Mtanzania mwingine yoyote achilia mbali yule aliyekula kiapo cha to "save lives" no matter what!.

Wengi wanasupport madakitari na hata mimi binafsi nakiri madai yao ni genuine but there are many routes to Rome, hiyo njia waliotumia kuleta siasa na kutaka kutumia human shield ya innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali, is a wrong way!. Yes wadai haki zao but not at the expence of poor ordinary innocent Tanzanians!.

Kwani hao viongozi wetu, wanaotumia ujinga wetu kama mwavuli wao kujinufaisha hawajaapa? Heri ungesema shetani na ibilisi wamekutana ningekuelewa bro!
 
Madaktari waliopata gahwa na juisi ya tende Ikulu, watawaita tu wenzao na kuwaambia tukubali yaishe na zitakazobaki ni porojo nyingi, unafikiri kuna nini zaidi? umewaona wamekaa kimya.

Kikwete kasitisha mkutano na wazee kuona matokeo ya maongezi yake na madaktari yatazaa nini. Na akiwaita wazee kuongea nao ujuwe ni maamuzi.

Nakuhakikishia kisa cha madaktari kugoma na kususa kimefikia "where the buck stops". Na itakuwa ni historia kama ilivyokuwa kwa magwanda, walipotoka Ikulu, mpaka leo wameufyata.
mgonjwa wa akili mara nyingine huna haja ya kuambiwa ili umjue kwani anajionesha kwa matendo yake.....hizi siasa maji taka hakika zinaiangamiza TZ.......hakika miafrika ndivyo tulivyo.......where is that guy with this important signature?
 
Back
Top Bottom