Madaktari Waliogoma Kukutana Leo Jumamosi- Tafsiri Yangu

Nje ya mada kidogo mkuu, samahani kama nitakuwa nimekukwaza lakini hivi ndivyo mawazo yangu yanavyonituma, sijawahi kuona jina la Mggid Mjengwa hapa jamvini ukishiri kwenye mijadala mbalimbali zaidi ya wewe kuleta topic zako tu na huchangii nje ya thread zako, je kila member akiwa achangii thread za wenzake za maana unadhani kutakuwa na maana yoyote kwa wewe kupost kitu hapa?

Nampa hongera Mzee Mwanakijiji licha ya kuwa Mwandishi nguli lakini anachangia mijadala mingi katika thread nyingi sana za maana.
Huu ni ushauri wangu wa bure kwako.
 
Mimi naunga mkono mgomo huu kwani ni mgomo unaotoa wito kwa Jamii ya Watanzania kuheshimu taaluma badala ya Siasa.

Kwa kipindi kirefu masuala nyeti ya kitaalamu katika nchi hii yamekuwa yakiamuliwa na wanasiasa ambao wengi wao hawana ujuzi wa aina yeyote zaidi ya kuvaa unifomu za vyama na kuitana huyu ni mwenzetu.

Matokeo ya madhara ya kuendesha nchi kisiasa ni dhahili yako wazi kwa kila Mtanzania kuyaona kumekuwa na shortcut nyingi za kufanikiwa kimaisha kwa Wanasiasa na kuwafanya wataalamu kukata tamaa.

Huu ni wakati muafaka wa kuacha kuwekeza raslimali za Taifa hili kwa wanasiasa na badala yake raslimali hizo zielekezwe kwenye taaluma mbalimbali ambazo zina tija na ukuaji na ustawi wa Taifa hili na watu wake.
 
Ukiona Serikali imekuwek na kufunga milango kuongea na wewe, ujuwe kuna madudu yako uliyoyafanya siku za nyuma na unaoneshwa halafu unaambiwa Jee, bado utaendelea na msimamo wako? Intelijensia ya Tanzania inajuwa inachokifanya.
 
Madaktari waliopata gahwa na juisi ya tende Ikulu, watawaita tu wenzao na kuwaambia tukubali yaishe na zitakazobaki ni porojo nyingi, unafikiri kuna nini zaidi? umewaona wamekaa kimya.

Kikwete kasitisha mkutano na wazee kuona matokeo ya maongezi yake na madaktari yatazaa nini. Na akiwaita wazee kuongea nao ujuwe ni maamuzi.

Nakuhakikishia kisa cha madaktari kugoma na kususa kimefikia "where the buck stops". Na itakuwa ni historia kama ilivyokuwa kwa magwanda, walipotoka Ikulu, mpaka leo wameufyata.
 
Angalau safari hii Kikwete katia heshima kidogo kwenye mgomo wa madaktari. Ungekuwa ni mgomo wa wafanyakazi wa kawaida tu, basi ungeona mkutano na wazee wa CCM wa dar es salaam na kusema hovyo hovyo tu. Lahaula kama ungekuwa ni mgomo wa waalimu basi ndiyo ingekuwa basi tu; wangeambiwa mara moja wamefukuzwa kazi. Ukosekanaji wa thamani kwa baadhi utumishi wa serikali kutoka ngazi za juu za uongozi ni sehemu kubwa sana ya tatizo la Tanzania leo hii.
 
Pasco,

Nimependa kuona kuwa unathamini uhai wa madaktari lakini wana siasa hawathamini, na wao wanategemea kuchukua mteremko wa kutotimiza maombi au matakwa ya msingi ya madaktari kwa sababu wanajua hawawezi kuacha watu wafe, kwahiyo naamini madaktari wameamua kutumia silaha ya mwisho ya kuwa litakalo kuwa na liwe kwa kususa au kugoma kufanya kazi.

Sijawahi kuona Serikali ya kidemokrasia inayoshindwa kuchukuwa hatua nyepesi ya kumaliza tatizo zito kama ilivyoshindwa serikali ya Tanzania kutatua tatizo hili la madaktari, kwani sijaona tatizo la kumsimamisha Waziri wa Afya kwa uhai wa wananchi wake.
 
Hivi kwanini tunapenda kujadili madai ya madaktari nusu nusu?ukipitia madai yao utaona kwamba huduma bora kwa wananchi ni dai la kwanza. Kuwaambia hawa mawaziri waondoke ni njia muhimu ya kupata mazingira mazuri ya mazungumzo yenye tija kati ya kamati ya pinda na madaktari.

Madaktari wameapa ku save life,lakini serikali yetu haijawajibika ipasavyo kuhakikisha hilo, isitoshe uongozi wa wizara ya afya hauthamini madaktari hii inapelekea kukosekana kwa ushauri wa kitaalamu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu afya ya mtanzania.
How can u save life if you prescribe oxygen unaambiwa hakuna, if u want to operate unaambiwa hakuna gauze au sterile gloves!
Leo hii mgonjwa wa asthma anaweza kufa kwa kukosa nebulizer!!.....how can u save life in harsh enviroment kama hii?

Tukirudi kwenye maslahi sitasema mengi but ni aibu kwa daktari kutiwa roba ya mbao mitaa ya uswazi wakati anatoka
kazini saa tatu usiku hapa akiwa ameteseka kwa usafiri wa daladala.

Maamuzi ya kugoma hayakufikiwa kimzahamzaha au kishabiki. Ukiona profesa wa neurosurgery na urology wanaingia kwenye mgomo ujue kuna tatizo kubwa na unatakiwa ulishughulikie kwa uangalifu na umakini wa hali ya juu sana.
Ukiwa muandishi wa habari wa vibahasha huwezi kutafuta undani wa mambo sana sana uta
fuata mkumbo tu.
asante mkuu japo sidhani kama huyu jamaa atagrasp kitu hapa!
Ukishakuwa biased km pasco(kwa sababu yoyote ile-vibahasha,kiitikadi,kidini,atittude,mindset......)ni vigumu kutoa analysis ya maana watu wenye akili wakakuelewa.Pasco hebu try to get outside your box for a minute,think big,give ur brain freedom of thinking.Jaribu kusoma post za mzee mwanakijiji..
 
Dear Pasco

You posses and command a lot of information as seen through your contribution.I am however not sure if this obsesses ion to draw judgement to other peoplescauses does not marginalise your contribution.

1. The manipulation of the public through media by the Govt in the issue or maybe by you; is it really fair to the Doctors and the public?

2. The underground acknowledgement by the govt to reconcile with Drs. is it notan indication that the parties involved have identified the problems?

I beg all great thinkers to focus on facts so that we are accurately informedand left to make our own greater thinkers judgement.

TO ME A BIASED CONTRIBUTION IS GERMINATING SEEDS OF DISCAUSE.
 
madaktari walitakiwa nao kuwa na roho ya huruma pamoja na kuhitaji maslahi,ukweli ni kwamba kila sekta inahitaji kuboreshewa maslahi lakini kusitisha huduma si kitendo cha uungwana .Basi ngoja tusubiri mazungumzo na mkuu wa nchi yatakuwaje,mimi ninachoomba wakubaliwe maslahi yao lakini nao vilvile wawajibishwe kwa kusababisha vifo vya watu wetu ambao wao wamekumbwa na maswaibu bila ya sababu yoyote.Wao hawana hati .Basi tusubiri muhafaka na mkuu wa nchi.

Ndugu Kipwa wa Dar es salaam
 
nisawa mkuu,mahakama wanatumia nguvu za sheri,ikumbukwe hawa si wabeba zege.wanahitaji kuombwa na kushauriwa ili waweze kurudisha mioyo yao ya huruma na umakini wa kazi,kinyume na hapo vifo vitaongezeka zaidi ya kugoma.
bora madocta wamekuwa wa wazi kuliko waalimu wanoenda shule bila kufundishaa watoto wetu wanapata div 0 kila siku zinavyo enda idadi ya failure inaongezeka

Mkuu JouneGwalu, tunawaheshimu sana madaktari ila kwa wengine wetu mimi nikiwemo, tunathamini zaidi uhai wa binadamu yoyote na uhai wa Mtanzania ndio unatakiwa uthaminiwe na Mtanzania mwingine yoyote achilia mbali yule aliyekula kiapo cha to "save lives" no matter what!.

Wengi wanasupport madakitari na hata mimi binafsi nakiri madai yao ni genuine but there are many routes to Rome, hiyo njia waliotumia kuleta siasa na kutaka kutumia human shield ya innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali, is a wrong way!. Yes wadai haki zao but not at the expence of poor ordinary innocent Tanzanians!.

Mkuu Pasco,

Siamini kama hayo maneno in RED yameandikwa na wewe!!!! Ingekuwa yametolewa na mwanasiasa, ningeelewa lakini kutoka kwako kama mwandishi wa habari, siamini. Labda tufafanulie kidogo ni siasa ipi inayoletwa na madaktari waliogoma!!!!

Tiba
 
madaktari walitakiwa nao kuwa na roho ya huruma pamoja na kuhitaji maslahi,ukweli ni kwamba kila sekta inahitaji kuboreshewa maslahi lakini kusitisha huduma si kitendo cha uungwana .Basi ngoja tusubiri mazungumzo na mkuu wa nchi yatakuwaje,mimi ninachoomba wakubaliwe maslahi yao lakini nao vilvile wawajibishwe kwa kusababisha vifo vya watu wetu ambao wao wamekumbwa na maswaibu bila ya sababu yoyote.Wao hawana hati .Basi tusubiri muhafaka na mkuu wa nchi.

Ndugu Kipwa wa Dar es salaam
madaktari waliwaheshimu watanzani na kusikiliza chonde chonde za pinda lakini ukweli baada ya kikao cha pinda cha tarehe tisa danadana ziliendelea.
Kwa nini mseme madaktari hawana huruma?wananchi hamjihurumii kwani wanachopigania madaktari kina matokeo mazuri kwa afya za wananchi.kutibiwa na daktari mwenye mawazo kuhusu afya yake,chakula na elimu ya watoto wake ni hatari sana halafu ujumlishe na mazingira mabovu ya kazi inakuwa balaa kubwa.
Huu ni wakati wa wanasiasa kutambua unapopewa dhamana ni lazima uwajibike.
 
Hamuoni kama rais anaingilia muhimili wa mahakama?
Mahakama nayo si ilitoa tamko
 
madocta wana madi makuu matatu ukinymbulisha unapata kama nane,
1.kuwajibishwa kwa viongozi walisababisha sekta ya afya kudorora<wizara ya afya
2.maboresho huduma ya afya nchini kwa kuhakisha madawa, machine za kuwapima waginjwa vikuwepo na vinafanya kazi mda wote, na vitendea kazi vingine vyote viwepo wakati wote ili mgojwa akifika hospiali asikose huduma ya kuokolewa maisha yake na kutibiwa akapone kabisa.
3.maslahi bora kwa wafanyakazi wa sekta ya afya kwa kazi ngumu wanayofanya na hapa nadhani kwa wale ambao tumewahi kuugua au kuuguliwa tunalewa na kulitambua, ili wawe na moyo na wasikimbilie nje ya nchi

my take-
huduma bora si ni kwa faida yetu sote?????????? au ni kwa ajili ya madocta????????, nadhani ni kwa ajili yetu sote so wanapodai mbona tunawabeza badala ya kuungana nao, hebu fikiria hatasikumoja hujawahisikia kuwa eti ziara ya rais au waziri imeeahirishwa kwa kuwa hakuna pesa ya mafuta au gari halijanyiwa repair, au semina imeahirishwa,
lakini utasikia hakuna dawa unaandikiwa ukanunue, au hakuna kipimo fulani, au operasheni imeahirishwa hamna bandage au vifaa havijachemshwa machine zimekufa wamama wajawazito wananunua vifaa vya kujifungulia hospitali,na kodi tumelipa, je ziara, semina, mikutano na warsha ndo muhimu kuliko afya zetu , mbona hatuwaungi mkono madocta??????katika kudai huduma bora tunakubali propaganda za serikali eti madocta wanataka maslahi tu siasa tuweke pemneni taaluma mbele.

hawa viongozi waandamizi wa wizara ndo wametuifkiisha hapa kwa nini wasijiuzulu ili pale paboreshwe na wengine wenye kuweza kufikiri zaidi yao, na kwa nini wanganganie watu wawili tu halafu madocta kama 2000 eti ndo hawako sahii, wanamagari mna majumba bora kama viongozi lakini vifaa hakuna na dawa na vikiwepo feki nnyingi kama vipimo vya HIV.

watanzania tusipojifunza na kuacha kuendekeza siasa tutakwisha tukiona kwa macho yetu

nawapongeza madocta kwa ujasiri wao utatugharimu wachache maisha yetukwa mda mfupi lakini tutapona wengi kwa mbeleni kwa maboresho yatakayofanywa katika seta ya afya chini kwa kuwa na huduma bora.
SHIMEEEEEEEEEEEEEEE TUAMKEEEE WATZZZZZZZZZZ
 
Nadhani watu wataelewa nini kinachopiganiwa kwa sasa ni siasa tu ndio inawaumiza,maboresho katika sekta ya afya ni jukumu letu sote,na ni lazima watu muyaunge mkono.
 
ni wakati wa wanataaluma kutetea taaluma zao sasa.
Tukizubaa hospitali za serikali zitakufa kama zilivyo shule na mashirika kama Posta,TTCL,TRC na mengine mengi.
 
Hapa mbona kama vile gvt inaingilia shauri lililokuwa mahakamani? Separation of powers?! mahakama si ilishatoa amri?

we toka lini mahakama ikawa chini ya waziri mkuu? Maana tangazo walilotoa limetoka ofisi ya pm.
 
Mkuu JouneGwalu, tunawaheshimu sana madaktari ila kwa wengine wetu mimi nikiwemo, tunathamini zaidi uhai wa binadamu yoyote na uhai wa Mtanzania ndio unatakiwa uthaminiwe na Mtanzania mwingine yoyote achilia mbali yule aliyekula kiapo cha to "save lives" no matter what!.

Wengi wanasupport madakitari na hata mimi binafsi nakiri madai yao ni genuine but there are many routes to Rome, hiyo njia waliotumia kuleta siasa na kutaka kutumia human shield ya innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali, is a wrong way!. Yes wadai haki zao but not at the expence of poor ordinary innocent Tanzanians!.

Nakama wamepima hizo njia nakuona haziwezi kuzaa matunda je? be critical
Kwa TZ ipi ukatumia ambayo haki yako unatakiwa uinunue!
Not yet!
 
Mkuu JouneGwalu, tunawaheshimu sana madaktari ila kwa wengine wetu mimi nikiwemo, tunathamini zaidi uhai wa binadamu yoyote na uhai wa Mtanzania ndio unatakiwa uthaminiwe na Mtanzania mwingine yoyote achilia mbali yule aliyekula kiapo cha to "save lives" no matter what!.

Wengi wanasupport madakitari na hata mimi binafsi nakiri madai yao ni genuine but there are many routes to Rome, hiyo njia waliotumia kuleta siasa na kutaka kutumia human shield ya innocent Tanzanians kama bakora ya kuichapia serikali, is a wrong way!. Yes wadai haki zao but not at the expence of poor ordinary innocent Tanzanians!.
We pascal we mpiga propaganda we!!!we unayedharau madaktari we.....we unayejifanya msemaji wa serikali we.....we unayewaamulia mambo yao madaktari we.....we unayejifanya kuwajali watanzania...mnafiki we....haki ya nani kwa hulka yako we..kama ungenyimwa haki yako kikazi leo we..considering your character here..ungetoa hata tigo we..i can bet on this....waache watu wenye akili zao wafanye mambo yao bana....we endelea kupotosha umma.........
 
Naona kama vile pande zote za mgogoro zinahama kutoka kwenye msingi wa mgogoro na kuweka uzito zaidi kwenye vijambo vidogovidogo vilivyotokana na kiini cha mgogoro huku jambo la msingi likiachwa kando. Mfano kiini cha mgogoro ni maslahi duni ya Madaktari, upungufu wa vifaa mahospitalini na mazingira mabaya ya kufanyia kazi . Hii imesababisha madaktari kugoma na wagonjwa kukosa huduma mahospitalini. Madaktari wanaahirisha hili mpaka Waziri na Naibu Waziri wajiuzulu.
Serkalini inaona Waziri na Naibu Waziri akijiuzulu itapungukiwa hadhi kwa sababu hoja hii imetokana na Madaktari, hivyo inaona itakuwa isinikizwa na Madaktri. Itaonekana legelege.
Wagonjwa waendelee kufa hadi Dr. Mponda na Lucy wawajibike kwa upande wa Madaktari halikadhalika wagonjwa waendelee kufaa ili mradi isionyeshe kuwa ni dhaifu.
Uhai wa waTZ una thamani kidogo kuliko umabavu wa serkali na kwa madaktari kuwajibika kwa waziri ni muhimu kuliko kuwajibika kwa madaktari kwa Afya za waTZ.

Watanzania ni watu wa ajabu wanaoweza kuacha nyumba inaungua mpaka kwanza wamkamate panya aliyekuwa anakula mahindi ndani ya nyumba inayongua, wakimkamata huyo panya watarudi kuokoa mali ilyomo ndani na ndipo waanze kuzima moto.
 
Back
Top Bottom