Madaktari waliofukuzwa sasa kuhojiwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MADAKTARI waliofukuzwa kazi na wale waliositishiwa leseni za muda wanatarajia kuanza kuhojiwa wakati wowote na Baraza la Madaktari Tangayika (MCT).
Katibu wa Jumuiya ya Madaktari inayoshughulikia madai ya madaktari ambayo pia iliratibu mgomo huo, Dk Edwin Chitage aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam kuwa madaktari wanasubiri utekelezwaji wa hatua hiyo.

Alisema Jumuiya pamoja na Chama cha Madaktari nchini (MAT) watachukua hatua zaidi baada ya kuona utekelezaji wa hatua hiyo ambayo itatoa mwanga juu ya mwelekeo wa Serikali katika kutatua mgogoro baina yao na Serikali.

“Tuna taarifa kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inakusanya ushahidi na kila daktari kwa waliofukuzwa na waliositishwa usajili wataitwa na kuhojiwa mmoja mmoja na Baraza”, alisema Dk Chitage na kuongeza:

“Kufuatia hatua hiyo Jumuiya ya Madaktari imejipanga kukabiliana na tukio hilo kwa kufuata taratibu za kisheria.

(MCT) ina sura ya mahakama na kimsingi inastahili kufanya kazi kwa sura hiyo, sisi tumejipanga, yapo mambo ya kisheria itabidi tuyafanyie kazi”alisema.

Akizungumzia afya ya Dk Stephen Ulimboka anayeendelea na matibabu nchini Afrika Kusini alisema kwa sasa imezidi kuimarika ingawa siku rasmi ya kurejea nchini haijajulikana.

“Afya ya Mwenyekiti wetu (Dk Ulimboka) inaendelea vizuri, lakini tarehe ya kurudi bado haijajulikana,tukipata taarifa hizo tutasema,”alisema.

Katika hatua nyingine katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Rodrick Kabangila alisema madaktari hawana imani na MCT kwa kuwa haiwezi kutenda haki katika shauri hilo.

Alisema sababu ya kukosa imani inatokana na baraza hilo kuundwa na Serikali.

Baraza la madaktari Tanganyika (MCT) ndilo linaloshughulika na usajili wa madaktari na mwenyekiti wake kimuundo ni Mganga Mkuu wa Serikali.Madaktari waliofukuzwa sasa kuhojiwa
 
Back
Top Bottom