Madaktari Walio Katika Mafunzo MNH Wapewa Barua ya Kufukuzwa Kazi

suluhisho la tatizo hili si kugoma, bali MAT wana nafasi kubwa sana ya kujadiliana na serkali ili kurekebisha hali hii; tufikirie pia maisha ya watu wagonjwa iwapo mgomo utafanywa nchi nizima
 
wao madenti na bado wanaleta siasa kazini!!!!! let them go to hell.


Bahati mbaya hujui hata unachokiandika hapa. Hujui kutofautisha mtu anayefanya intern na mwanafunzi!

Serikali inafanya siasa kwenye maisha ya wananchi halafu wanatokea watu vipofu kama wewe wanaleta upupu.

Hao madaktari ulitegemea waishije bila kulipwa posho zao? Siku nyingine ushirikishe akili yako kabla ya kuandika.
 
Haya ndiyo dr. Slaa alisema jana kwamba serikali yetu imekuwa ikifanya maamuzi ya kisiasa hata katika mambo yanayowahusu watanzania. Mimi naomba mat wawe na umoja ktk hili kama walivyofanya madaktari wa kenya juzi. Haiwezekani watu wakakaa ofisini na kufikiria kuwafukuza wengine wkt watu hao hawakulipwa kwa muda, je wangekula nini?
Hakika huu ni uonevu mkubwa sana kama unavyotokea hata kwa wanafunzi wetu.
 
suluhisho la tatizo hili si kugoma, bali MAT wana nafasi kubwa sana ya kujadiliana na serkali ili kurekebisha hali hii; tufikirie pia maisha ya watu wagonjwa iwapo mgomo utafanywa nchi nizima


Tunatakiwa kwa pamoja tuiambie serikali iache kucheza na maisha ya watu. Kutowalipa madaktari na baadae kuwafukuza kwakuwa wanadai chao ni dhahiri kwamba serikali imekurupuka.
Mimi niidhani Anna Abdallah pekee ndiye mkurupukaji kumbe wako wengi, Dr. Haji Mponda nae mkurupukaji!
 
wao madenti na bado wanaleta siasa kazini!!!!! let them go to hell.

kuongea ni dhahabu lakini wakati mwingine kunyamaza ni almasi. Yaani umeongea pumba kabisa ni bora ungenyamaza. Kudai haki (mshahara) sio siasa.
 
Nilitaka tu kujua nani ana uwezo mkubwa wa kunielewa ama yule bora liende. Zamani tuliokuwa mashuleni, tulikuwa na vitabu vilivyosema, 'someni kwa maarifa' yaani someni katikati ya mistari muelewe nini ujumbe uliokusudiwa, ndio maana vijana wetu wengi siku hizi vitabu kama 'kusadikika', 'mfalme juha', 'the river between', na 'malenga wapya' vimebaki kapuni kwa kuwa hawaelewi hata waandishi walikusudia nini, poleni mliodhani niko kinyume na madaktari.

Lets cut is loose, maana yangu ilikuwa ni hii, 'hakukuwa na haja ya madaktari kusitisha mgomo baada ya kulipwa haki yao, wangeshinikiza kurekebishwa kwa mikataba yao kwa kuwa wasomi kama hawa walijua kwa hakika madhara ya kugoma na kurudia matapishi. Serikali imeoza na wao kama watu maalum hawakutakiwa kulainika mapema hivyo kwa kuwa suala lao lilipaswa kutatuliwa kitaalam na sio kisiasa, ona kilichowapata sasa. Na kwa wale waliotoa 48 hrs nilikuwa nawapa ujumbe kwamba wenzao wamewaangusha msimamo wao hivyo na wao wajiandae kujua hatma yao if at all walipitisha upuuzi wa kusitisha mgomo, na mwisho kwa kuisifia serikali nilikuwa nawakejeli kwa kutochukulua masuala haya kwa uzito kwa kuwa suala la afya ni nguzo kuu ya ustawi wa taifa hivyo kusema wakaze kamba kuwatimua wengine ni kuwaambia instead 'mbona mnashindwa kujali afya za wananchi', ujumbe wa jumla ulikuwa ni kwamba haki lazima itendeke na kila mtu awe na fursa ya kuona haki ikitendeka.

Ni mimi,
Pangu Pakavu,
Nawasalimia.
 
Namala na Primus, MAT leaders tunaomba mtangaze mgomo wa madaktari wote nchini kama madaktari hawa hawataruhusiwa kuendelea na kazi bila masharti yoyote.
 
Nadhani ni wakti muafaka kwa watanzania wote bila kujali taaluma zetu tuingie mtaani kudai haki za hawa vijana!!
Wao wakipata mafua india, sisi hata huo wanaotutibu kimagumashi wanawatimua!!
Guyz work up, let fight for our right!!
 
Nadhani ni wakti muafaka kwa watanzania wote bila kujali taaluma zetu tuingie mtaani kudai haki za hawa vijana!!
Wao wakipata mafua india, sisi hata huo wanaotutibu kimagumashi wanawatimua!!
Guyz work up, let fight for our right!!
umeongea vizuri, hapo kwenye red umeongea kimagumashi
 
Nasikia hii timua timua ni amri toka Ikulu,....ikiwa ni adhabu ya JK kuzomewa pale UDSM siku
ya maadhimisho ya miaka 50 ya UDSM.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba adhabu hii haiwakuti wana-UDSM peke yao,.naona iko
extended kila mahari hadi pale "mfalme" atakapo furahi au pale hopefully zomea zomea
itakapo isha.

Juzi juzi St.John waligoma kwa sababu ya kucheleweshewa hela,wakafungiwa chuo(though ni private,
naskia ni amri kwa organization zote TZ iwe private au government).

UDSM ukigoma au kuongea kidogo tu,hauna chako.(wame fanikiwa kutuliza kwa silaha hiyo).
UDOM wame cheleweshewa hela more than a month,juzi wamegoma wakapewa hela na kuna watu kama 10 wame timuliwa
mazima kabisa.

MUHAS waligoma wakati wa graduation,kuna watu kama 30 wametimuliwa mazima,....hadi madaktari nao wanatimuliwa
tena?kaaaaazi kweli kweli.

Maoni yangu:
Kwa kua mitanzania ndivyo tulivyo,the only country you can oppress citizens and still they do nothing.
kesho utasikia umoja wa madaktari unaomba msamaha kwa kuwa "wamekosea sana" wakati walikua
wanadai haki zao.
 
Hivi hii nchi wanasi-hasa ndiyo bora kuliko wtz wote? Wabunge posho ya makalio kwa siku shs. 200,000 sawa. Wakuu Wa mikoa wakitembela wilaya hula na kulala bure, hulipwa posho sawa!

Madaktari kulipwa posho laki nne kwa mwezi dhambi. Tumeonewa na kudharirishwa vya kutosha, lazima sasa tuseme inatosha.
MAT semeni hapana. Wtz simameni na kusema hapana. Watawala wawe viongozi.
 
Ndiyo mambo ambayo sumaye alikuwa anasema kuwa wabunge wakiongezewa posho kila kundi litaanza kudai na watampa wakati mgumu rais lakini watu wenye akili fupi kama ndugai wanatoa majibu mepesi kwa maswali mazito
 
Muhimu hapa watu waangalie mambo yafuatayo
1. Je, wana haki ya kulipwa mishahara
2. Je, wnadai mshahara, nyongeza yake au posho?
3. Kwanini hawajalipwa

Hawa ni wafanyakazi mafunzoni kama walivyo wafanyakazi wengine wenye uzoefu, wana mahitaji na wana haki ya ujira.
Wanapogoma anayeathirika ni bibi, shangazi, kaka n.k.
Wanasiasa wana hospitali zao India, south Africa,London n.k.

Kama hakuna pesa Hazina, mbona wafanyakazi wengine wamelipwa? na fedha zinakosekana vipi ili hali kuna nyongeza za posho kwa wengine kwa aslimia 200.

Kama yupo aliyezembea amechukuliwa hatua gani.

Hatuwezi kukwepa siasa katika maisha yetu kwani wana siasa ndio wanaoleta matatizo yote haya. Hata barua za kufukuzwa kama zimetolewa basi ni mwanasiasa aliyeandika. Lakini pia tujiulize hivi ukitoa ushahidi umeingiza siasa? Je si kweli kuwa wabunge wameongezewa posho?Je si kweli wanalipiwa na serikali matibabu yao nje? wapi pesa zimepatikana zikakosekana hizo kidogo za ujira wa watu wanaohudumia taifa.
 
Hii ndio serekali isiyojiamin..sijui ni nani waliwachagua hawa,???
 
Ndiyo mambo ambayo sumaye alikuwa anasema kuwa wabunge wakiongezewa posho kila kundi litaanza kudai na watampa wakati mgumu rais lakini watu wenye akili fupi kama ndugai wanatoa majibu mepesi kwa maswali mazito

Kilichokuwa kinadaiwa ni mshahara wa kila mwezi ambapo interns wanachukua 80% ya mshahara kwa fani husika na wala kinachodaiwa sio posho wala nyongeza ya mshahara kama wabunge. Elewa mada husika kwanza kabla ya kuchangia.
 
Kwa hivyo viposho wanavyolipwa vinaweza kuwapeleka India kweli? Mwezi m1 tu hawakulipwa mgomo huo!!! Sasa watapata wapi fedha za kuwapeleka India?
Hujaelewa somo,atakayetibiwa India ni mfukuzaji siyo aliyefukuzwa!
 
Wao watatibiwa India (Appolo hospital) sisi sasa tutajuta kuzaliwa Tanzania
 
mbona adhabu hii ni kali mno kwa hao vijana? Si nasikia Tanzania tuna upungufu wa madaktari.
T anzania tatizo letu ni uongozi wa kuratibu matumizi ya nguvu kazi tulizo nazo Zambia wana uhaba mkubwa kuliko sisi isipo kuwa wao wanatambua umuhimu wa wana taaluma na uratibu wao pia ni mzuri.
 
Back
Top Bottom