Madaktari Waitishe Mgomo usiokoma kudai maslahi! Simameni Pamoja!

wagome tu ili mabadiliko yapatikane, maana hata wasipogoma, watu wanaendelea kufa tu, hawathaminiwi na serikali. Lazima heshima ya msomi ionekane sasa kwa nguvu zote
 
Kwasababu serikali hii inaonyesha kutowajali professionals wake kwa kiasi kikubwa huku wakishabikia wapuuzi,wezi wa mali za umma na wapiga siasa feki, ni wakati muafaka sasa kwa nchi hii nao professionals wa ngazi zote wasimame sasa na kuhesabiwa kwa kudai haki zao zinazoporwa na walafi wachache kwenye utawala huu.Ni wakati wa madaktari wooote nchini kugoma kwa hakika kwani ni wao ambao wanaweza kuwa organized kimsimamo kwenye kudai haki zao.Nasema wagome madaktari haswa wale walioko kwenye hospitali zote za rufaa nchini ambako huduma muhimu hazitaenda bila wao kuwepo .Wasimame wagome haswa maana wamezidi kudharauliwa na watawala....Nchi hii migomo huwa inaishia kuumizana kwa kuwa mara nyingi watu wanasalitiana na pia vyama vyao havikai nao kuwapa support.....mara zote migomo tunayoona inaleta mabadiliko duniani ni ile inayokuwa pasi na kikomo mpaka shida zinapopatiwa majibu.....huu ndio msingi wa mgomo, lakini hapa tz watu wanagoma kikondoo (tunaona kwa waalimu,wanafunzi etc etc...).....wanatishiwa nyau then wanafarakana na kuwapa watawala ushindi......hii si migomo....mkiamua kugoma gomeni haswa.......hii ni sacrifice yaani(mnatakiwa kuwa sacrificial lambs)....unaweka nyanga zote pembeni unaitafuta haki.......hapa tz sijaona migomo ya namna hii........chondechonde madaktari......na wataalam wengine watafuata maana ni professionals wengi nchi hii ambao wanataabika na utawala huu........wengi hawasemi kwa kuwa hawana jinsi lakini professionals tz hawana thamani mbele ya watawala...wenye kuthaminiwa nchi hii ni mafisadi na wanasiasa feki wanaocheza ngoma ya watawala......time to wake up.....kumbukeni JK alitukana wafanyakazi kabla ya uchaguzi uliopita...akionyesha dhairi namna gani hajali wafanyakazi nchi hii......
 
Maskini madaktari wa Tanzania...kila mmoja anapigania nafasi ya utawala: DMO,RMO,...wanapigana vikumbo kupata nafasi kwenye departments zenye semina na marupurupu wamesahau wao ni nani(waone wanavyopeana michongo semina,vikao vya bajeti n.k)....ni aibu kwa daktari kuwa machinga...eti 'nina temporary jobs kwenye hospitali 4' njaa zitawatia vilema,kwani hamfahamu jinsi ubongo ulivyo na limitation katika ku-concentrate? Dr.mzima afisa utumishi anakuchimba mkwara usidai marupurupu yako unaufmyata?
 
Nimefurahishwa na makala yako umefanya kazi nzuri ku highlight mambo ya muhimu na umechukua muda kuyaelewa matatizo ya madaktari wa Tanzania. Nitoe mchango mdogo.....Madaktari wa Tz wanafanya kazi katika mazingira magumu mno (natambua kuwa wafanyakazi wote wa umma wanafanya kazi katika mazingira magumu Tz) Hebu tazama mifano hii: Mosi,daktari anapokuwa kazini pamoja na kumtibu mgonjwa lakini yeye pia anakuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa kama TB, VVU/UKIMWI, Hepatitis nk haya ni magonjwa yanayoleta kifo! Katika hospitali zetu nyingi hakuna vitendea kazi vya kutosha kumkinga daktari/na wauguzzi dhidi ya hatari hizi. Madaktari wanalowa damu kila siku katika kuokoa maisha ya watu (kwa kipindi cha UKIMWI) hii ni hatari kubwa! Hakuna miwani mikubwa kuzuia damu kuwarukia machoni madaktari wakati wa upasuaji(kama zipo ni muhimbili na katika miji mikubwa hapa Tz) nina experience ya kuzamisha mkono katika uke wa wa mama aliyejifungua huku nikiwa nimevaa glovu inayoishia katika kiganja cha mkono ilihali mkono wangu ulizama hadi kwa kufika katika kiwiko (watawala wanakuambia hakuna glovu ndefu) ukifikiria sana unajiona mjinga kwa kujiweka katika risk ya UKIMWI nk (ambao hata ukiupata utaishiwa kuitwa kiwembe, malaya nk) lakini unafanyaje mgonjwa yuko mbele yako...Niwambie wanaJF, madaktari tunowaona wanaenda kazini kila siku ni kwasababu ya mambo yafuatayo:
1. Hii ndio kazi inayowapa kula ya kila siku (they have to)
2. Wana mapenzi/wito na kazi yao
3. Wako motivated na satifaction inayotokana na kuona wagonjwa wanapona, ndugu wanafurahi, wanajifunza vitu vipya katka kutibu wagonjwa
4. Rushwa..nafasi waliyopo inawapa nafasi kupata hela kirahisi kwa njia ya rushwa (Mara nyingi hii huja kama asante, kwa madaktari wengi)

Najua humu kuna madaktari wengi...mnaweza kuni challenge pia.
...mkuu pole sana,hilo la glove ndo hasa lililonigusa,mke wangu ni muuguzi ktk hoptali za jiji la Mwanza,kila anapotaka kwenda kazini inamlazim ajinunulia glove kwa pesa zake kutokati ktk hako kamshahara-kake kadogo,inambidi anumue glove kwajili ya kwenda kufanyia kazi kwani kwenye kituo anachofanya kazi hakuna glove ilihali uduma zinatolewa kituo hapo ni pamoja na kuzalisha mama wajawazito...Hivi ni haki kweli serikali inampeleka kiongozi akatibiwe India kwa mamilio ya pesa zinazotoka ktk kodi za huyo anayekosa ata tsh500 ya kununuli glove!?...
 
Mzee Mwanakijiji!
Muda wetu unapishana nadhani sijachelewa kuchangia hii thread. Wewe ni mtu mzima unatakiwa kutii sheria. Kabla hujawahamasisha wagome nenda kaisome vizuri sheria ya kazi ya Mwaka 2004. Imeainisha vizuri kwamba Madaktari hawaruhusiwi kugoma! Kama ukitaka wagome peleka hoja yako kwa Waziri wa Kazi ili sheria ibadilishwe ndipo wagome. Kwa kuwa sheria inakataza mgomo na hivyo Kama hawana CBA na waajiri wao basi ni kusuka au kunyoa waache kazi ila mgomo marufuku sio mimi ni sheria aliyoridhia Benjamin William Mkapa.:A S 465:
 
Mkuu naona umechanganya hapo,wenye fani yao watakuja kunisahihisha na mimi.Nadhani medical officers ndiyo MD,na wengine ndiyo hao medical assistants na clinical officers kama sikosei

kaka kama ilivyo initials ndio kirefu chake, MD ni M-medica na D- doctor,
 
Fani ya udaktari imedharaulika sana hapa nchini ni wakati sasa wa hawa wataalamu kujua kuwa tunahitaji mabadiliko katika sekta nzima ya afya.
 
Hivi, Tanzania ina madaktari wangapi ambao wanatoa huduma ya kuangalia binadamu (Full MD siyo Medical Assistants au Medical Officers)? Na kati ya hao ni wangapi HAWAKO Dar-es-Salaam wako mikoani?
Amini amini nakwambia selikali yako haina taarifa za watu inao waanda ktk taaluma yoyote ile achilia mbali madaktari, hawajui wamehitim wangapi, wameajiliwa wangapi nawapo sehemu gani, pamoja kuwa selikali ndo mlipa mshahara leo hii haifaham idadi ya waajiliwa selikalini ndo maana ninapo andika ujumbe huu kuna zoezi la kuhakiki watumishi wa umma linaendelea ktk walaya mbalimbali. Ikumbukwe kuwa kila wilaya inao maafisa utumishi, wakurugenzi na wakuu wa idara ambao watumishi wengine wapo chini yao, nao uhakiki pay roll kabla ya kupelekwa benki kwa ajili ya malipo ya mishahara kwa mwezi husika. Maafisa hao mwisho wa siku huandaa ripoti na kuituma tamisemi, ajabu ni pale selikali inapo simama na kusema tunalipa watumishi hewa!
 
Tuna tatizo la ukosefu wa vifaa hasa vya uchunguzi (Diagnostics) pia kuna fani ambazo hatuna wataalamu, sio kwa sababu waTZ hawana uwezo wa kusomea lakini ni kuwa hata wakisoma kwa kuwa hakuna facilities hawataweza kufanya kazi hapa TZ..Chukulia mf; mtu asomee upasuaji wa mishipa ya damu (Vascular surgery). Dakatai bingwa ni yule ambaye baada ya kusoma degree ya kwanza anasoma tena masters kwa miaka 3-4 na kuwa binga katika eneo fulani mf: watoto, Upasuaji, Macho nk...pia wengine hsoma tena kwa miaka 3 na kuwa super speacilists mf daktari bingwa upasuaji wa mishipa ya fahamu (Neuro surgeons)

Nadhani nimekusaidia
Zitto Zuberi Kabwe alipelekwa india kwa tatizo la chronic sinusitis, bila shaka kama alifanyiwa oparesheni ilikuwa ni ya kawaida mno (cud-well luk, sina uhakika na speling) ambayo ingefanyika hapa tena katika mazingira ya kawaida.
 
Kwa jinsi maisha yalivyo magumu kwa wafanyakazi, hasa wafanyakazi wa chini, migomo ingeedelea kwa wafanyakazi wote. Madaktari kazeni buti serikali imezidi kuwadhalilisha.
 
Hivi, Tanzania ina madaktari wangapi ambao wanatoa huduma ya kuangalia binadamu (Full MD siyo Medical Assistants au Medical Officers)? Na kati ya hao ni wangapi HAWAKO Dar-es-Salaam wako mikoani?

Ili kujibu swali lako wataitisha sensa ya madaktari wote (MD), iliwapate pesa za kumalizia miradi yao.
 
Kizimkazimkuu,

Hapo nilipoweka bold ndipo panawarudisha nyuma. Ni kitendo cha aibu kuona eti daktari analalamikia mshahara mbuzi anaolipwa na serikali. Kwani hata wakiongeza wakaanza kuwalipa 5,000,000 TSh/month bado soon itakuwa haitoshi kwa jinsi inflation inavyokwenda na pia matumizi yenu yanatazidi kuongezeka. Binafsi naona nyie madaktari ndio watu wenye opportunity ya kujiajiri wenyewe na kutoka kwenye hizo hospitali za serikali na kuanzisha za kwenu binafsi.
Ni aibu kwa best brains zetu kulia njaa kwa serikali inayoongozwa na wagonjwa wa akili. Nyie mkilia njaa na hao wengineo kama walimu na wale waliokuwa wanakuwa wakatikati na wamwisho darasani hivi sasa hawana ajira za kueleweka wafanye nini? Hawa madaktari wetu wajue kuwa vyeti vyao ndio mitaji yao. Hata hizo Apollo huko India zimeanzishwa/zinamilikuwa na vikundi vya madoctors "Medical Groups" ambao wamechukua mikopo kuanzisha na kukuza hizo institutions mpaka zilipofikia. Nyie doctors kazi kulalamika serikali serikali...mmeshawahi sikia serikali gani inalipa mshahara mkubwa? Serikali ni huduma kwa umma.
Mwanakijiji ameulizia kuhusu statistics za Doctors holders wa Doctor of Medicine degree mpo wangapi..yaani hakuna hata muwakilishi wa chama chenu aliyekuja hapa mtandaoni kutupa hizo statistics. Inaonyesha how pathetic and disorganized bunch of "m$@##*s" you are ...kazi kulalamika bila kuweka concrete action plans na strategy za kufanikisha mnapata good working conditions. Msisubiri mpaka tuwatukane humu JF ndio muanze kutushutumu. Msione Wayahudi wamefikia hapa walipo (kushikilia the Only SuperPower)...ila waliplan kwenye Zionist conference 1887 kuwa wanahitaji kuwa na nchi yao. Phase 1 ikawa achieved 50 years later. Phase 2 consolidation in another 50 years ndipo hapa walipo. Waarabu na pesa zao zote "Petrodollar" wameishia kupiga kelele kama debe tupu. Binafsi ninahasira sana na madaktari wa Tanzania... natamani niwahutubie kama JK alivyowahutubia wafanyakazi wa serikali na kuwaita MBAYUWAYU... NAMI PIA NIONGEZEE SPECIFICALLY KUWA MADAKTARI WA TANZANIA NI KAMA VILE KUNGURU wanauwezo wa kujitengenezea vipato na maisha mazuri kwa kujiajiri ila kazi kuililia serikali ambayo ni proven failure(Mnikosoe mniambie lini serikali ya TZ imeweza kudeliver anything on ime and within budget?). Mpaka hapo mtakapoacha tabia ya kukimbilia ajira wizarani (mjiheshimu na kuheshimu taaluma yenu) ndipo serikali itakapo waheshimu.

Doctors nawatakia malalamiko mema.
duh,naona umewalalamikia sana madaktari. kwa upande flani uko right madaktari wamekua nyuma sana ktk kujiajir,kitu ambacho kinaweza kua solution ya kuinua maisha yao. lakini kwa upande mwingine afya ni huduma ambayo ukiichukulia sana kama ni biashara,wapo watu wengi hawata afford hiyo huduma. kiukweli kama ukitaka kuanzisha hospitali ni gharama kubwa,hasa kwa mtu ambaye kipato chake ni kidogo hata serving hawezi kufanya.option ya kukopa ni nzuri but hiyo italazimu uwe kibiashara zaidi ili uweze kurejesha mkopo. je watanzania wangapi wataweze kuafford hizo gharama katika hospitali binafsi? angalia mfano wa shule.tulisoma shule za msingi tukiwa tunakaa kwenye vumbi darasa la watu200,hakuna walimu, na matatizo mengine mengi. leo hii shule binafsi ni nyingi sana......lakini wangapi wanaweza kulipa ada za mamilioni kwa mwanafunzi wa shule ya msingi? je ni vyema kwa waalimu wakajiunga vikundi waanzishe shule zao binafsi ambazo si wa tz wengi wataafford au serikali irekebishe maslahi ili watanzania wengi wapate elimu katika shule za umma?
 
Kizimkazimkuu,

Hapo nilipoweka bold ndipo panawarudisha nyuma. Ni kitendo cha aibu kuona eti daktari analalamikia mshahara mbuzi anaolipwa na serikali. Kwani hata wakiongeza wakaanza kuwalipa 5,000,000 TSh/month bado soon itakuwa haitoshi kwa jinsi inflation inavyokwenda na pia matumizi yenu yanatazidi kuongezeka. Binafsi naona nyie madaktari ndio watu wenye opportunity ya kujiajiri wenyewe na kutoka kwenye hizo hospitali za serikali na kuanzisha za kwenu binafsi.
Ni aibu kwa best brains zetu kulia njaa kwa serikali inayoongozwa na wagonjwa wa akili. Nyie mkilia njaa na hao wengineo kama walimu na wale waliokuwa wanakuwa wakatikati na wamwisho darasani hivi sasa hawana ajira za kueleweka wafanye nini? Hawa madaktari wetu wajue kuwa vyeti vyao ndio mitaji yao. Hata hizo Apollo huko India zimeanzishwa/zinamilikuwa na vikundi vya madoctors "Medical Groups" ambao wamechukua mikopo kuanzisha na kukuza hizo institutions mpaka zilipofikia. Nyie doctors kazi kulalamika serikali serikali...mmeshawahi sikia serikali gani inalipa mshahara mkubwa? Serikali ni huduma kwa umma.
Mwanakijiji ameulizia kuhusu statistics za Doctors holders wa Doctor of Medicine degree mpo wangapi..yaani hakuna hata muwakilishi wa chama chenu aliyekuja hapa mtandaoni kutupa hizo statistics. Inaonyesha how pathetic and disorganized bunch of "m$@##*s" you are ...kazi kulalamika bila kuweka concrete action plans na strategy za kufanikisha mnapata good working conditions. Msisubiri mpaka tuwatukane humu JF ndio muanze kutushutumu. Msione Wayahudi wamefikia hapa walipo (kushikilia the Only SuperPower)...ila waliplan kwenye Zionist conference 1887 kuwa wanahitaji kuwa na nchi yao. Phase 1 ikawa achieved 50 years later. Phase 2 consolidation in another 50 years ndipo hapa walipo. Waarabu na pesa zao zote "Petrodollar" wameishia kupiga kelele kama debe tupu. Binafsi ninahasira sana na madaktari wa Tanzania... natamani niwahutubie kama JK alivyowahutubia wafanyakazi wa serikali na kuwaita MBAYUWAYU... NAMI PIA NIONGEZEE SPECIFICALLY KUWA MADAKTARI WA TANZANIA NI KAMA VILE KUNGURU wanauwezo wa kujitengenezea vipato na maisha mazuri kwa kujiajiri ila kazi kuililia serikali ambayo ni proven failure(Mnikosoe mniambie lini serikali ya TZ imeweza kudeliver anything on ime and within budget?). Mpaka hapo mtakapoacha tabia ya kukimbilia ajira wizarani (mjiheshimu na kuheshimu taaluma yenu) ndipo serikali itakapo waheshimu.

Doctors nawatakia malalamiko mema.

Brother/sister..unachangia kuwa na staha halafu pia andika vitu unavyovifahamu...umetoa maelezo ya jumla mno na ya kuokoteza vijiweni...mengi uliyoandika yanaonyesha uelewa wako una "shoti"; Acha nijaribu kukujibu katika hili moja.......
1. Kujiajiri: Iliuanzishe biashara yenye mafanikio lazima kuwe na wateja wenye uwezo wa kununua huduma/bidhaa (in this case wagonjwa) Kwa hali ya uchumi wa watanzania/Tanzania nionyeshe wateja hao wako wapi? Nitajie ni Hospitali ngapi binafsi (yenye mafanikio) ambayo daktari anafanya kazi Full time; kama sio asubuhi anakuwa kazini jioni anapita hapo kuongeza kipato. Duniani kote (kwenye maendeleo) Huduma ya afya inalipwa kwa mtindo wa "Bima ya Afya" wana JF waliopo nje wanajua Kuna nchi ambazo baadhi ya hospitali haziwezi kukupokea kama huna Bima. Mf: Ulio hai ni Hospitali ya Upasuaji wa Moyo ya Dr. Massao, pamoja na kuwa ilikuwa ni pekee hapa Tz lakini "alikosa wateja". Tanzania hii ambayo 80% ya watu wako vijijini, zaidi ya 51% wanaishi kwa < tsh 1000 kwa siku hakuna mazingira yanayowezesha ustawi wa private health sector. Niambie ni majirani zako wangapi wanapo ugua wanaenda Aga Khan, Hindu Mandal au regency na wanalipa huduma out of their own pockets....watanzania ni maskini mno mpaka hatujitambui ni maskini kiasi gani!

Mtoa mada kwa kufupi umeandika Upupu....hoja uliyotaka kuijenga ya kujiajiri ndio kila siku wanasiasa wanadanganya majukwaani kuwa wastanzia wajiajiri...hili haliji hivihivi lazima mazingira yaandaliwe;m$@##*s like you should be the last to give advice on matters that you know nothing about.
 
Zitto Zuberi Kabwe alipelekwa india kwa tatizo la chronic sinusitis, bila shaka kama alifanyiwa oparesheni ilikuwa ni ya kawaida mno (cud-well luk, sina uhakika na speling) ambayo ingefanyika hapa tena katika mazingira ya kawaida.
......katika mazingira mbayo hakuna vitendea kazi (daktari ananawa na sabuni ya mshindi kbla ya OP) hata mimi leo siwezi kumpeleka mwanangu Muhimbili...nawaheshimu madaktari lakini mazingira yanatisha..I would rather meet the same profeessionals Aga Khan kwa huduma ilel ile.
 
Mzee Mwanakijiji!
Muda wetu unapishana nadhani sijachelewa kuchangia hii thread. Wewe ni mtu mzima unatakiwa kutii sheria. Kabla hujawahamasisha wagome nenda kaisome vizuri sheria ya kazi ya Mwaka 2004. Imeainisha vizuri kwamba Madaktari hawaruhusiwi kugoma! Kama ukitaka wagome peleka hoja yako kwa Waziri wa Kazi ili sheria ibadilishwe ndipo wagome. Kwa kuwa sheria inakataza mgomo na hivyo Kama hawana CBA na waajiri wao basi ni kusuka au kunyoa waache kazi ila mgomo marufuku sio mimi ni sheria aliyoridhia Benjamin William Mkapa.:A S 465:

........ Nisema kuwa kwa zaidi ya miaka 8 I am not in clinical medical practice; kwa hiyo sihusiki sana na haya yanayoendela lakini nayafuatilia kwa makini na I wish the best kwa madktari walioko katikati ya kadhia hii. Lakini tujiulize; kuna haja gani ya kuheshimu mkataba ambao tayari upande mmoja umesha udharau. Uhalali wa mkataba wowote unataka wahusika wa pande zote mbili kkuheshimu vifungu vyote vya mkataba. Hebu nielewesheni katika hili.
 
Kumbe na wewe ni mteja mmoja wa Private hospital! tuanzie hapo chagua death bed yako hapo Aga Khan na mtajilishe mhindi! kazi njema na malalamiko mema.
 
Kizimkazimkuu,

Asante kwa ujumbe murua. Umejenga hoja nzuri na kutoa mfano wa shule binafsi. Maswali ni machache tu ya kujiuliza. Je, umeshawahi kusikia shule binafsi zilizoanzishwa zinakosa wanafunzi na mwenye shule kuifunga? Unasema hakuna wateja...toka lini daktari anakosa wateja. Mtaje wa daktari ni mgonjwa na mazingira yetu jinsi yasivyomazuri wagonjwa hawakosekani ndugu.
Kwa jinsi ulivyoandika ndio inaonyesha namna gani tunamatatizo ya kifikra na business acumen. Dr.Masao kashindwa kwa kuwa serikali imeona bora kupeleka wagonjwa India kwa kuwa charging na billing structure yake haitoi value for money. Hiyo ndiyo premise ya kwanza kwenye business yeyote. Mteja anaangalia value for money! Kwa kuwa wewe sio daktari halafu hunijui lakini umekuwa happy kuona nilichoandika ni upupu, nashukuru. Sasa wewe ndio umeonyesha upeo mdogo hata kushindwa kuijali familia yako kuipeleka kwenye matibabu Aga Khan, pale hakuna kitu. Kidogo kuhusu mimi binafsi ili unishtumu zaidi. Ni qualified doctor nimefungua practice yangu Mwanza karibu na Nyegezi. Hakuna mteja aliyefika na kushindwa kulipia matibabu. Huduma tunatoa inalingana na value ya pesa anayochajiwa mteja. Pili sijawahi maishani mwangu kumrudisha/kumkatalia mteja huduma kisa hana pesa kwa kuwa natambua umaskini uliopo (Lawyers wanaita probono work).Kipato changu kwa mwezi kamwe siwezi kulalamika na nilianza nikiwa na mtaji wa TSH2,000,000.
Hao madaktari wakiondoka kuna kitu wachumi wanaita Demand/Supply theory kwanza wakiondoka serikali lazima itakuwa underpressure kuajiri wengine. Wengine watatoka wapi, likely India kwa hiyo mishahara yao lazima iwe juu. Basi na hata wao wazawa wataheshimiwa kupata wanachostahili. Hivyo basi nao madaktari wetu na watakuwa angalau sawa na nyie mnaotibiwa Aga Khan.
Nikusaidie..nawasilisha upupu wangu, hope kuna madaktari watakaousoma. Binafsi nimefanikiwa kwa kuamini kuwa mkombozi wa maisha yangu ni mie mwenyewe kujitafutia ajira. Unadhani serikali ghafla itajireform na kuwajali madaktari?

Brother/sister..unachangia kuwa na staha halafu pia andika vitu unavyovifahamu...umetoa maelezo ya jumla mno na ya kuokoteza vijiweni...mengi uliyoandika yanaonyesha uelewa wako una "shoti"; Acha nijaribu kukujibu katika hili moja.......
1. Kujiajiri: Iliuanzishe biashara yenye mafanikio lazima kuwe na wateja wenye uwezo wa kununua huduma/bidhaa (in this case wagonjwa) Kwa hali ya uchumi wa watanzania/Tanzania nionyeshe wateja hao wako wapi? Nitajie ni Hospitali ngapi binafsi (yenye mafanikio) ambayo daktari anafanya kazi Full time; kama sio asubuhi anakuwa kazini jioni anapita hapo kuongeza kipato. Duniani kote (kwenye maendeleo) Huduma ya afya inalipwa kwa mtindo wa "Bima ya Afya" wana JF waliopo nje wanajua Kuna nchi ambazo baadhi ya hospitali haziwezi kukupokea kama huna Bima. Mf: Ulio hai ni Hospitali ya Upasuaji wa Moyo ya Dr. Massao, pamoja na kuwa ilikuwa ni pekee hapa Tz lakini "alikosa wateja". Tanzania hii ambayo 80% ya watu wako vijijini, zaidi ya 51% wanaishi kwa < tsh 1000 kwa siku hakuna mazingira yanayowezesha ustawi wa private health sector. Niambie ni majirani zako wangapi wanapo ugua wanaenda Aga Khan, Hindu Mandal au regency na wanalipa huduma out of their own pockets....watanzania ni maskini mno mpaka hatujitambui ni maskini kiasi gani!

Mtoa mada kwa kufupi umeandika Upupu....hoja uliyotaka kuijenga ya kujiajiri ndio kila siku wanasiasa wanadanganya majukwaani kuwa wastanzia wajiajiri...hili haliji hivihivi lazima mazingira yaandaliwe;m$@##*s like you should be the last to give advice on matters that you know nothing about.
 
Kizimkazimkuu,

Hapo nilipoweka bold ndipo panawarudisha nyuma. Ni kitendo cha aibu kuona eti daktari analalamikia mshahara mbuzi anaolipwa na serikali. Kwani hata wakiongeza wakaanza kuwalipa 5,000,000 TSh/month bado soon itakuwa haitoshi kwa jinsi inflation inavyokwenda na pia matumizi yenu yanatazidi kuongezeka. Binafsi naona nyie madaktari ndio watu wenye opportunity ya kujiajiri wenyewe na kutoka kwenye hizo hospitali za serikali na kuanzisha za kwenu binafsi.
Ni aibu kwa best brains zetu kulia njaa kwa serikali inayoongozwa na wagonjwa wa akili. Nyie mkilia njaa na hao wengineo kama walimu na wale waliokuwa wanakuwa wakatikati na wamwisho darasani hivi sasa hawana ajira za kueleweka wafanye nini? Hawa madaktari wetu wajue kuwa vyeti vyao ndio mitaji yao. Hata hizo Apollo huko India zimeanzishwa/zinamilikuwa na vikundi vya madoctors "Medical Groups" ambao wamechukua mikopo kuanzisha na kukuza hizo institutions mpaka zilipofikia. Nyie doctors kazi kulalamika serikali serikali...mmeshawahi sikia serikali gani inalipa mshahara mkubwa? Serikali ni huduma kwa umma.
Mwanakijiji ameulizia kuhusu statistics za Doctors holders wa Doctor of Medicine degree mpo wangapi..yaani hakuna hata muwakilishi wa chama chenu aliyekuja hapa mtandaoni kutupa hizo statistics. Inaonyesha how pathetic and disorganized bunch of "m$@##*s" you are ...kazi kulalamika bila kuweka concrete action plans na strategy za kufanikisha mnapata good working conditions. Msisubiri mpaka tuwatukane humu JF ndio muanze kutushutumu. Msione Wayahudi wamefikia hapa walipo (kushikilia the Only SuperPower)...ila waliplan kwenye Zionist conference 1887 kuwa wanahitaji kuwa na nchi yao. Phase 1 ikawa achieved 50 years later. Phase 2 consolidation in another 50 years ndipo hapa walipo. Waarabu na pesa zao zote "Petrodollar" wameishia kupiga kelele kama debe tupu. Binafsi ninahasira sana na madaktari wa Tanzania... natamani niwahutubie kama JK alivyowahutubia wafanyakazi wa serikali na kuwaita MBAYUWAYU... NAMI PIA NIONGEZEE SPECIFICALLY KUWA MADAKTARI WA TANZANIA NI KAMA VILE KUNGURU wanauwezo wa kujitengenezea vipato na maisha mazuri kwa kujiajiri ila kazi kuililia serikali ambayo ni proven failure(Mnikosoe mniambie lini serikali ya TZ imeweza kudeliver anything on ime and within budget?). Mpaka hapo mtakapoacha tabia ya kukimbilia ajira wizarani (mjiheshimu na kuheshimu taaluma yenu) ndipo serikali itakapo waheshimu.

Doctors nawatakia malalamiko mema.

mwenye macho haambiwi tizama
na mwenye masikio sikia
gogomoka nakuunga mkono na mguu nikiangalia MUHIMBILI,AMANA NA MWANANYAMALA wagonjwa wanvyokufa kwa kutopata huduma kwa muda.natumai tukiwa na private hosp. nyingi ni rahisi huduma hizi kupatikana na kwa bei nafuu pia kwa ufanisi mkubwa kutokana na ushindani.
 
Ushindani siku zote anayefaidika ni mteja. Mifano ni mingi tukianzia na Bia, mobile etc
 
Back
Top Bottom