Madaktari waipa Serikali saa 72

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Iwarejeshe kazini wenzao 229 waliotimuliwa



Mponda(18).jpg

Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii, Dk Haji Mponda


Chama cha Madaktari Nchini (MAT), kimetoa saa 72 kwa serikali kuhakikisha madaktari waliotimuliwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wanarudishwa kazini.

Kimesema kinyume na matakwa yao kitaitisha mkutano mwingine mkubwa wa wanachama wote Jumatano ijayo (Januari 18) kutoa uamuzi wao.

Aidha, chama hicho kimemsimamisha uanachama Mganga Mkuu wa Serikali, Deo Mtasiwa, kwa muda wa mwaka mmoja kwa kosa la kusaliti fani ya udaktari na pia kwa

kushindwa kumshauri Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii, Dk Haji Mponda kuhusiana na mambo yanayohusu fani ya udaktari Tanzania.

Chama hicho pia kimemuomba Rais Jakaya Kikwete, kumwajibisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Blandina Nyoni kwa kuwa chanzo cha migogoro ya madaktari.

Tamko hilo la MAT, lilitolewa jana na Rais wa chama hicho, Dk Namala Mkopi, katika mkutano wao wa wanachama wote wa nchi nzima uliofanyika, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa chama chake kimelazimika kukutana kwa dharura kutokana na matatizo ambayo yamejitokeza na kuamua kujadili masuala mbalimbali.

Matatizo hayo ni pamoja na madaktari waliopangiwa sehemu nyingine za kutokubaliwa na kusababisha waendelee kukaa nyumbani bila kazi.

Hospitali walizopangiwa na kutokubaliwa ni pamoja na Amana, Temeke, Agakhan na Lugalo.
Hospitali nyingine walizopangiwa hazina madaktari bingwa wa kutosha ikiwemo hospitali ya Mwananyamala.

Alisema chama chake kimeridhia tamko hilo la kuwataka madaktari hao ambao wanafanya mafunzo kwa njia ya vitendo kurudi kazini .

“Ifahamike kuwa interns huomba kwenda kufanya internship katika hospitali fulani kutegemeana na malengo ya baadaye waliojiwekea na sio wizara kuwapangia maeneo,” alisema.

Alisema kuna baadhi ya madaktari hao wamepelekwa katika hospitali ambazo hazina madakatari bingwa hali inayowafanya kupoteza taaluma zao.

Dk Mkopi alisema kuna baadhi ya vifaa ambavo vinapatikana Hospitali ya Muhimbili tu na si katika hospitali zingine na kwamba madaktari hao watashindwa kupata mafunzo yao kwa ufasaha kama inavyotakiwa.

Alisema wamesikitika na uamuzi huo uliotolewa na wizara na wameshindwa kuelewa kwanini “intern doctors” waadhibiwe wakati walidai walipwe mishahara yao tu na serikali ilikiri kosa hilo.

Hata hivyo, alisema ni haki yao kwa madaktari hao kudai posho zao kwani wasingeweza kuwahudumia wagonjwa wakiwa katika mazingira mabaya.

“Wanachama wangependa kuona waliofanya uzembe huo wanawajibishwa mara moja na sio kuachwa waendelee kuwaadhibu madaktari wasio na kosa,” alisema Dk Mkopi

Alisema madaktari hao wamekuwa wakifanya kazi bila malipo katika kipindi cha muda mrefu hali ambayo ilisababisha kusitisha kazi na serikali kuamua kuwalipa mishahara yao.

Dk Mkopi, alisema kusimamishwa kwa madaktari hao kumesababishia huduma mbovu kwa wagonjwa na kusababisha madaktari bingwa kuwa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa hao.
Aidha, MAT imemtaka Dk Mponda afute kauli yake

inayoashiria kwamba “intern doctors” ni wanafunzi wa udaktari wa mwaka wa tano ambayo inamaanisha asivyoelewa maana na kuwepo kwa madaktari hao.

“Tumesikitika kuona waziri kama huyo haelewi maana ya Intern doctor na kusema kuwa ni wanafunzi mwaka wa tano hapo alipotosha umma na aliwadhalilisha madaktari hao,” alisema Dk Mkopi.

Dk Mkopi alisema hao ni madaktari kamili ambao wamehitimu mafunzo yao na kula kiapo rasmi cha udaktari na pia wanafanya kazi ya kumtibu mgonjwa na kupona.

“Ijulikane kwamba mjadala wa hivi ulishawahi kutokea mwaka 2005 na waziri wa afya kipindi hicho alikiri bayana kwamba intern ni daktari kamili aliyefuzu,” alisema Dk Mkopi.
Dk. Mkopi alisema mkutano unaotarajiwa kufanyika Jumatano watazungumzia ajenda mbalimbali ikiwemo hatma ya heshima ya

fani ya udaktari na mustakabali wa huduma za afya kwa Watanzania.
Aidha, watahoji posho ya kazi muda wa ziada (on
call allowance) kama ilivyopitishwa mwaka 1990 na kufanyiwa maboresho mwaka 2008.

Ajenda nyingine ni mshahara mpya wa daktari unaoendana na elimu, ujuzi, umuhimu,
hadhi, majukumu, na hali ya uchumi wa sasa na mfumuko wa bei. Alisema maslahi mengine ya madaktari kama nyumba, posho ya mazingira magumu, ufadhili wa masomo ya elimu ya juu na posho ya kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi( Risk allowance) na kuhamishwa hovyo hovyo kwa madaktari bingwa 61.

Mgogoro huo wa madaktari unafuatia kufukuzwa kwa wenzao 229 baada ya kudai posho zao na kulipwa na serikali na baadaye kupewa barua za kufukuzwa.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Nadhani safari hii wapo mafuta makali. Sema kibaya wanaohukumiwa ni walala hoi wapiga kura! Kazi kwelikweli!
 
yaan hii nchi inaendesha ki**nge sana,utafukuzaje madakatari bana?wakati waliopo hawatoshi?politics is full of sh*t
 
If they stand firm itakuwa poa sana, serikali imezoea magumashi ktk utatuzi wa masuala sensitive na yanayohusu taaluma. Wasirudi nyuma tu kama walimu ambao wamekuwa na kawaida ya kutishia kisha wanaufyata!
 
Ukitafakari kidogo tu, utaona kwamba mawaziri wa Afya ambao sio madaktari wanafanya kazi zao kwa ufanisi sana kuliko hao wenye utaalam wa afya. Angalia kina Megji na Anna Abdalla na kina Mwinyi Ruksa enzi zile. Hao kina Mwakyuusa, Sarungi, Mtulia, Chiduo na huyo aliyepo sasa na wengineo, vurugu tupu. Ni katika vipindi ambavyo wataalam wa afya wanashika nyadhifa za wizara ya aya kama mawaziri ndipo matatizo kama haya hutokea. They simply do not care sababu wao wamepata. Madai wanayajua uhalali wao lakini wanatunisha misuli makusudi waonekane kwa mabosi wao kama wanafaa. Wanaoumia ni raia wa kawaida ambao hawana uwezo kwenda private hospitals na India au Africa Kusini au Nairobi. Hizo siku 72 zitaisha na viburi vitabaki kuwapo wizarani. Lakini niwakumbushe hao wakubwa, sijaona aliyefanya kiburi cha namna hiyo akaishia vizuri. Wanatia huruma. Wengine wanaogopa hata kuingia mawodini kuwaona ndugu zao waliolazwa, kwa kuwa ikigundulika undugu na mgonjwa upo basi hasira za watumishi wa afya zinaanza kupitia kwa mgonjwa. Uwe mzuri kwa watu wote unapopanda juu, kwani hujui nani atakuwa mzuri kwako utakaposhuka chini. Kuna haja ya madaktari hao wanapopata vyeo wizarani kupitia mafunzo ya uongozi bora.
 
we need your support people.wao wanatibiwa nje,waliowachagua hawana uwezo huo inabidi watibiwe na sisi.kama hatuna hela mnafikiri tutaweza watibu vizuri kwa asilimia 100?its time for change
 
Back
Top Bottom