Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

CCM oyeeee, sisi watawala tunasema punda afe mzigo ufike. Maisha bora kwa kila Mtanzania ndio haya. Tumejaribu, tumeweza, tunasonga mbele. Usisahau kuipigia CCM kura, mafiga matatu hapo 2015
 
Kama hayo kweli yapo, kwa nini msingegoma toka mwanzo kwa ajili ya kupatiwa hivyo vifaa? Badala yake mnadai hayo baada ya kuona kuwa mngegoma kwa ajili ya maslahi yenu tu msingeeleweka. Madaktari acheni kuua watu na badala ya kuendelea na mgomo wa kipuuzi, sasa mrudi kuchapa kazi.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.

Kwa hiyo kwa maoni yako, kwa kuwa hawakugoma tangu mwanzo, basi waendelee kukubaliana na mazingira haya. Kwa maana rahisi, kwamba wewe unaridhika na hali ilivyo sasa ktk hospitali na vituo vyetu vya afya, siyo? Huenda ikawa wanatumia njia mbaya kujaribu kubadili hali hii, je wewe kwa upande wako umetumia njia gani bora kubadili hali hii, au ndio vile umeridhika nayo, siyo?
 
Kama hayo kweli yapo, kwa nini msingegoma toka mwanzo kwa ajili ya kupatiwa hivyo vifaa? Badala yake mnadai hayo baada ya kuona kuwa mngegoma kwa ajili ya maslahi yenu tu msingeeleweka. Madaktari acheni kuua watu na badala ya kuendelea na mgomo wa kipuuzi, sasa mrudi kuchapa kazi.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.

Mkuu mimba hutunga na kujifunguwa wakati wake ukifika baada ya mama kupata uchungu, hapa walipofika ndo mahala pake hata uvumilivuvu hufikia hatua ikashindikana. Sasa niwangapi wanaokufa kwa kukosa madawa? kukosa tiba sahihi kwa kukosa vetendea kazi sahihi kugundua ugonjwa halisi kwa tiba sahihi? kwa makosa yanayotokana na msongo wa kiwawazo ndani ya vichwa vya madakitari wakifikilia watapata wapi fedha kukidhi mahitaji ya familia zao kupelekea kufanya operations za makosa na kuuwa bila kukusudia,wangapi wanakufa kwa kuambukizana magonjwa hospitalini kwa kupagwa kama ndizi mawodini? Je ni waheshimewa wangapi wakizidiwa huendelea kubakia humhum nchini kwa matibabu bila kuenda india kwanini ........

Mkuu hakika wengi mno wanapoteza uhai kwa uzembe wa serikali, imefika wakati tuibane serikali tupate huduma bora mbona kodi tunalipa au wewe mkuu hulipi? naimani unalipa na pia unandugu na jamaa ambao ungependa siku moja waipate haki ya kupata huduma bora kwa afya zao
 
Kipindi hiki serikari ina mkakati wa kupeleka wagonjwa wote India kama mgomo utatokea. Serikari imejipanga kwa udhaifu utakaojitokeza, ndio sababu Mwinyi kapewa hiyo wizara.
 
Daktari wangu vimon upo wapi? Wakati wa mgomo wa kwanza ulitupa update za ukweli Kamanda wangu. Come up again.
 
Kama hayo kweli yapo, kwa nini msingegoma toka mwanzo kwa ajili ya kupatiwa hivyo vifaa? Badala yake mnadai hayo baada ya kuona kuwa mngegoma kwa ajili ya maslahi yenu tu msingeeleweka. Madaktari acheni kuua watu na badala ya kuendelea na mgomo wa kipuuzi, sasa mrudi kuchapa kazi.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.

unayajua madai ya madaktari kuanzia mwanzo au unadamdia treni kwa mbele?
 
Haya sasa! Maisha bora kwa kila Mtanzania ndiyo hivyo sasa!
Halafu unamkuta mtu anaifagilia ccm..........!
 
Haya sasa! Maisha bora kwa kila Mtanzania ndiyo hivyo sasa!
Halafu unamkuta mtu anaifagilia ccm..........!

Mkuu ni vilaza wa ushabiki kwa ccm, sidhani kama hawayaoni haya ila hujifanya sintofaham na wengine hujikuta kuchanganya madawa vichwani kwa kuingiza udini kwenye maada wazi kabiasa kama hii.

PENYEUKWELI UONGO HUJITENGA
 
Sasa mbona waziri wa afya siku ile Bungeni hakugusia kabisa mapungufu ktk hiyo hospital badala yake alizungumzia madaktari wanadai maslahi yao tuu!

Hakuna anayeonyesha viraka vya makalioni bana, unasema kwa mbele tu kuwa kulichafuka na tomato sauce na kumeshafutwa
 
Kwa Madaktari kugoma kwa sababu ya maslahi yao ni sawa kwakua silaha ya mwisho walionao wafanyakazi katika kudai haki yao ni Mgomo,wasiwasi wangu ni je madaktari walishaanza mazungumzo na Serikali,kwanini mara hii wamekataa mazungumzo? au labada serikali haitaki kutekeleza makubaliano yao? Kama inawezekana anayejua makubaliano hayo ya Madaktari na Serikali atuwekee hapa pamoja na yale ambayo Serikali imeyakubali.
 
Sasa mbona waziri wa afya siku ile Bungeni hakugusia kabisa mapungufu ktk hiyo hospital badala yake alizungumzia madaktari wanadai maslahi yao tuu!
hayo mapungufu atayaonea wapi wakati hajawahi kuingia wodini ,hao si wanatibiwa india,tena wangegoma kuandika rufaa kwa viongozi wa serekali ili watibiwe hapa bongo
 
Kama hayo kweli yapo, kwa nini msingegoma toka mwanzo kwa ajili ya kupatiwa hivyo vifaa? Badala yake mnadai hayo baada ya kuona kuwa mngegoma kwa ajili ya maslahi yenu tu msingeeleweka. Madaktari acheni kuua watu na badala ya kuendelea na mgomo wa kipuuzi, sasa mrudi kuchapa kazi.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.

ndugu kadakabikile, huwezi kuwalaumu madaktari kwa kutogoma hapo hawali, kumbuka kila jambo na wakati wake, km wewe usingeweza kuamrisha uzaliwe ulaya, hata mgomo haukuwezekana hivyohivyo, wakati wake haukufika. Serikali inafahamu mapungufu yaliyopo ktk hospitali zetu ndo maana wao wanaenda kwa first consultation nje. Waache madaktari wagome km siri kali hawataki mgomo watekeleze madai ya madokta maramoja. Mkuu wa kaya ahamuru maramoja uone km hayajatekelezwa.
 
Mkuu mimba hutunga na kujifunguwa wakati wake ukifika baada ya mama kupata uchungu, hapa walipofika ndo mahala pake hata uvumilivuvu hufikia hatua ikashindikana. Sasa niwangapi wanaokufa kwa kukosa madawa? kukosa tiba sahihi kwa kukosa vetendea kazi sahihi kugundua ugonjwa halisi kwa tiba sahihi? kwa makosa yanayotokana na msongo wa kiwawazo ndani ya vichwa vya madakitari wakifikilia watapata wapi fedha kukidhi mahitaji ya familia zao kupelekea kufanya operations za makosa na kuuwa bila kukusudia,wangapi wanakufa kwa kuambukizana magonjwa hospitalini kwa kupagwa kama ndizi mawodini? Je ni waheshimewa wangapi wakizidiwa huendelea kubakia humhum nchini kwa matibabu bila kuenda india kwanini ........

Mkuu hakika wengi mno wanapoteza uhai kwa uzembe wa serikali, imefika wakati tuibane serikali tupate huduma bora mbona kodi tunalipa au wewe mkuu hulipi? naimani unalipa na pia unandugu na jamaa ambao ungependa siku moja waipate haki ya kupata huduma bora kwa afya zao

Mkuu nafikiri umeeleweka sana, watakao bisha ni ujeuri tu.
Hawakumbuki yule mgonjwa alopasuliwa kichwa badala ya mguu muhimbili?! yale ndo matokeo halisi ya frustration za kazini ingawa wenyewe wanaita uzembe.
Watuulize waalimu, ukiingia class ukiwa na msongo-mawazo kinachotokea huwa ni nini! fikiria natakawa niwafundishe vijana wa MBA au MSc Entrepreneurship kuhusu strategic planning huku nawaza mwanangu leo atatibiwa kweli?! maana nina bima ya afya tena ya kijani lakini upuuzi ndio huo, unakutana na daktari hapa, X-ray unaambiwa kapige ahmadiya, unafika pale wanakwambia bima hatupokei inatucheleweshea malipo, unalipa mfukoni mwako, unarudi na Tax kwa dr pale moro mkoa, unaambiwa sijui nini
Mke wangu alifanyiwa upasuaji kwaajili ya uzazi oct 2011, haaaaaaa!! Mungu bariki nilikuwa nimejiandaa mfukoni, pia nikawa na matumaini ka kakadi kangu ka kijani ka bima ya "chafya" maana si afya tena, eti imagine kuanzia sijui kitu gani cha kupokelea mkojo, mpaka drip za baada ya upasuaji unanunua, na duka la dawa liko nje tu pale getini unapoingia hosp mkoa (moro), Mungu wangu, kufika pale, unaambiwa kuna dawa zinazopokea bima na nyingine ambozo ndo muhimu sana unaambia hazipokei bima, KHAAA nikachanganyikiwa, my wife wangu mpenzi yuko theatre,
bado unakuta Dr analalamika hajanywa hata chai, tangu saa 10 usiku anapiga upasuaji tu, na Mrs ndo kaingia kama emergency maana alidevelop severe bleeding. Maskini, kidogo tu mtoto wangu wa kiume angefariki, maana walikuja kukuta mji wa mimba umeshachanika, na mkono wa mtoto ulikuwa unavinjari nje ya tumbo la uzazi, Imagine!!
Mungu saidia ni baada ya kujieleza na kwa kuwa nilisomaga Mzumbe A-Level, nina madaktari nafahamiana nao ambao tulikuwa class moja. so angekuwa asiyefahamika, anakosa my wife wake, na my baby boy wake.
kinachosikitisha, kila mwezi wanakula kama 37,500 hivi za bima ya afya kwa afya ambayo siyo afya hata kidogo, p.u.m.b.a.v.u zenu serikali, ebu waboresheeni kwanza maslahi, pili vitendea kazi madaktari weeeeeetuuuuu eeeeeeeeeeee
natamani kuingia barabarani kuondoa serikali madarakani
 
MGOMO WA MADAKTARI DAWA YAKE NI MABADILIKO YA SERA NA MFUMO WA TIBA NCHINI NA WALA MABAVU KAMWE HAUTOMSAIDIA MTU WALA SERIKALI YETU

Mgomo wa madaktari hauwezi kuzuiliwa kwa mabavu isipokua ni kwa njia moja tu ya kubadilisha sera na mfumo wa uendeshaji wa sekta zima ya tiba nchini.

Kama mtu alijidanganya mahala kwamba hili la madaktari ni upepo tu utapita basi itakua ni masikitiko makubwa sana jinsi gani mambo yatakavyoanza kuzorota mahospitalini.

Hali hii isiposhughulikiwa vema na kwa wakati pengine makundi mengine ya wafanyakazi kama vile walimu nao kuamua kuunga tera - safari hii nao kwa kufanya hivo hadharani badala ya ule mgomo baridi tunaofahamu kwamba unaendelea hadi hivi sasa.
 
hebu tembelea hospitali za mikoa au wilaya ujionee.kwa mfano kanda ya kaskazini hauna kipimo cha CT scan,kilikuwepo KCMC lakini kimekufa.ukienda kanda ya ziwa ni hayo hayo na ukirudi muhimbili vilevile.
hakuna anayeshtuka wala kushughulikia swala hili kwa sababu kiongozi anayehitaji huduma hii mara moja hukwea pipa na kwenda appolo india wewe mlala hoi utajijua mwenyewe!!
 
kadri mda unavyosonga mbele ndivyo tunavyozidi kuona vimbwanga kati ya serikali na madaktari.sasa madaktari wameamua kuweka hadharani madhambi ya serikali.wameamua kuwaambia wananchi ukweli kwa nini huduma za afya ni mbovu.una mfano huu hapo chini halafu pitia blogs mbalimbali ujionee

No insults but does anybody else smell a rat?! Public being used as a bargaining chip! Who really has the general public interests at heart? Please guys I really want to know, I am kind of confused.
 
hebu tembelea hospitali za mikoa au wilaya ujionee.kwa mfano kanda ya kaskazini hauna kipimo cha CT scan,kilikuwepo KCMC lakini kimekufa.ukienda kanda ya ziwa ni hayo hayo na ukirudi muhimbili vilevile.
hakuna anayeshtuka wala kushughulikia swala hili kwa sababu kiongozi anayehitaji huduma hii mara moja hukwea pipa na kwenda appolo india wewe mlala hoi utajijua mwenyewe!!

.............Hii serikali kwa kweli itatufikisha pabaya sasa kwa hali inavyoonyesha.

Ingali wameshatufikishaga kitambo lakini kwa sasa wanataka ku2zamisha Watanzania ktk dimbwi la umaskini ambalo hata serikali nyingine ikija chukua madaraka hakika itakutaga wizara zote zimebaki magofu tu!

Juzi ktk kusoma ile bajeti ya mafisadi mbona wizara hii cjasikia waziri mlengwa akilizungumzia hili la kutokuwepo ama kuharibika kwa hz vyombo ktk hosptal hz?

Kweli hawa ccm ni janga lililowazi kwa Watanzania!
Mabadiliko yanawezeka hakika............haiwezekani tukaachiwa majengo tu!
 
Mgomo sasa inaanza kuzooleka masikioni mwa wananchi wa Tanzania. Jambo ambalo nadhani lapaswa kuangaliwa ni kwanini kuna migomo, Mfano madaktari wadai kugoma, TUCTA, walimu n.k. na maandamano ya wazee wa Afrika mashariki na wanafunzi vyuo vikuu. Najiuliza hivi watawala wanayaona haya? Kama ndiyo hatua gani wanachukua? Au ni funika moto kwa makuti? Migomo na maandamano yasiyoisha ni dalili za serikali kushindwa, ni dalili za viongozi kutokua makini, kushindwa kazi na uzembe. Nadhani ipo haja watanzania kuacha utani, waamke kujitazama upya, walikotoka, walipo na waendako. Migomo na maandamano isiwe za kutishia nyau, msimamo wa dhati uonekane wa kuwaajibisha viongozi, wananchi kuacha ushabiki badala yake palipo na madai ya kweli km haya madaktari, walimu, TUCTA, wanafunzi na wazee wa EAC yaungwe mkono kwa nguvu zote kushinikiza watawala kuwajibika kama hakuna utatuzi, wajuwe maamuzi ni wananchi na kama hawawezi kuleta mabadiliko(wananchi) waache kulalamika. Poleni madaktari kwa madai yenu yamsingi yanayofanyiwa mzaa.
 
Back
Top Bottom