Ruppy karenston
JF-Expert Member
- Jun 5, 2011
- 412
- 73
Mambo ya Liwalo na Liwe,ndo yashaanza kupamba moto. Aisee,serikali dhaifu inayaona haya?
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.
Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.
Nilishasema na naendelea kusema Watanzania/Tanganyika tusipoelekeza hasira zetu pahala sahihi tutaendelea kuumizwa, hii ndio nafasi ya ku vent hasira zetu na concern zote tulizonazo. Jamani time is now, Dr Ulimboka katuonyesha jinsi ya kudai haki na maslahi ya madaktari na Watanzania kwa ujumla.....lets follow suit
Mimi naamini ukombozi wa Mtanzania/Tanganyika utapatikana kwa roho za ujasiri watu kama Dr Ulimboka Kamanda Godbless Lema na wengine wote waliopoteza maisha au wanaoweka maisha yao hatarini ili tupate kushuhudia na kuikomboa nchi yetu
Ndio hayo alipanga kuyasema bungeni ila la Olimboka likaingilia mikakati
Hili ni moja ya udhaifu katika Muungano. Tunahitaji kuwa na Serikali ya Tanganyikana waziri wa afya atakaye shughulikia matatizo ya madaktari wa Tanganyika ndio maana unaona migomo hii ni Tanzania Bara(Tanganyika)Hivi kwa mwendo huu miaka ijayo mbeleni wenetu watasomea udaktari kweli? Labda kama watakukuwa na uhakika wa ajira za Botswana
Tunakokwenda au tulikofika?Hivi mwisho wa haya yote nini jamani? sasa inahitajika kufanya maombi na mafungo kwajili ya Taifa letu tunakokwenda ni kubaya hali inazidi kuwa ngumu tuu kwa mlala hoi na inazidi kuwa nzuri kwawalio nacho.
Acha uendeleeeee nani aliwapa KURA....!!??? mnashangaaa nini!!??
Taarifa ambazo zimethibitishwa zinatabanaisha kuwa madaktari wanaandaa mass resignation.
Mass resignation ni nzuri sana. Nashauri madaktari wajiuzuru kabla hawajafukuzwa wote ili waende jangwani tufanye uwanja wa tahariri ili serikali ione hasira yetu watanzania.
sasa hv tujifunze zaidi tiba asili na dawa za kienyeji kwa mwendo huu twafa woteee maskini!!
Mkuu naomba kufahamu umesomea nini ambacho unakimudu katika maisha yako. Yaani mchango wako mkubwa kwa Taifa ni nini?Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.
Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.
Bado tunahitaji kujifunza namna ya kutatua migogoro!!!! Nchi hii inakoelekea ni kubaya!!!!!!
taarifa ambazo zimethibitishwa zinatabanaisha kuwa madaktari walio katika uzoefu kazini,intern doctors wameanza kufukuzwa katika hospitali mbalimbali ambapo katika hospitali ya dodoma madaktari 11 kati ya 33 wamefukuzwa na madaktari wote 70 waliokuwepo hospitali ya rufaa mbeya chini ya ulinzi mkali wa polisi wameambiwa waondoke kufikia saa 11 jioni ya leo wakati huo huo mkurugenzi wa hospitali ya bugando amewafukuza madaktari wote 44 na kuwataka warudi wizarani wakati madaktari waliosajiriwa wameamuriwa kufika kesho wawe kazini au la wanafukuzwa.
Wakati huo huo madaktari wakazi waliitwa na senate ya bugando na kulazimishwa kurudi kazini lakini walikataa mbele ya senate hiyo hivyo wakaambiwa watafutiwa udahili wao na wote kwa pamoja wakapiga makofi wakisema wako tayari kwa hilo.
Habari zaidi zinazidi kupasha kuwa hospitali ya mwananyamala wameletewa fomu za kujaza kama wako tayari kuendelea na kazi au la,ila madaktari wamesimamia msimamo wao huo kuwa mgomo uko pale pale.
Katika hatua nyingine chuo cha tiba bugando na kile cha muhimbili viko mbioni kufungwa kutoka na walimu wao ambao ni madaktari kugoma na mazingira kutokuwa rafiki kwa kujifunzia.
Wakati hayo yakiendelea taarifa zinasema hsopitali ya tanga bombo imeingia rasmi kwenye mgomo na ile ya mount meru
habari zaidi madaktari wanajiandaa kwa mass resignation muda wowote
\
Mkuu Mlachake,Wenzetu wakipata mafua Breki ya kwanza Airport.