Madaktari wa hospitali ya Temeke nao WAGOMA

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Hospitali ya Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam !
Kwa takribani wiki Tatu za mgomo wa madaktari wa Tanzania , hospitali hiyo ilikua ikiendelea na HUDUMA, hadi ilifikia hatua ya madiwani wa manispaa ya Temeke kuwatunuku Tuzo maalumu kwakujali afya za wagonjwa kuliko maslahi ya kipato cha madaktari hao.
Mchana huu, Tangazo limetolewa na kuungwa mkono na madaktari wote wa hapo kuingia katika Mgomo kuunga mkono harakati za wenzao.

SOURCE,
MIMI mwenyewe nilikuwapo eneo la tukio muda wa saa 7 mchana leo.
 
hapa ndio Temeke Hospitali kwa ambao hamjafika
100_4117.jpg
 
ninavyofahamu temeke hupokea wagonjwa kutoka dar na mkuranga.kwa hiyo slowly mgomo umeanza kusambaa.
 
Mods, pls do the needful... huyu jamaa ametumia lugha ya kukera sana. Waislam hawana huruma? toka lini? Huu mtandao unaheshimika sana, ni zaidi ya habari kwa wengi wetu...

acheni kupiga kelele , hamjui namna ya kuripoti kwa Mods, nyie vipi ?
 
Jamani kama mnataka Kureport kuna Link hapo juu Imeandikwa REPORT ABUSE kelele zenu hazimfikii mod on time.
 
Kuanzia sasa siwaheshimu tena madaktari wa Tz.

Hawa ni mamluki, wanaongozwa na pesa si wito.

Hawana tofauti na wauaji. Wamekalia ubinafsi na kutetea matumbo yao.

Mishahara mikubwa wanayoipata inazidi watumishi wengine wa umma.

Hata hivyo hawaridhiki, tamaa imewajaa, wanataka kuikamua serikali mpaka umma ukose hata aspirin mahospitali???

Waishie kuzimu.
 
  1. Kuanzia sasa siwaheshimu tena madaktari wa Tz.
  2. Hawa ni mamluki, wanaongozwa na pesa si wito.
  3. Hawana tofauti na wauaji. Wamekalia ubinafsi na kutetea matumbo yao.
  4. Mishahara mikubwa wanayoipata inazidi watumishi wengine wa umma.
  5. Hata hivyo hawaridhiki, tamaa imewajaa, wanataka kuikamua serikali mpaka umma ukose hata aspirin mahospitali???
Waishie kuzimu.
  1. lini madaktari wa tanzania waliheshimiwa,umeshawahi kusikia daktari anaitwa mheshimiwa?
  2. mamluki wa nani?umewahi kusikia elimu ya mtoto wa daktari ni bure,umewahi kusikia daktari anapewa sukari bure?hivi daktari akipanda daladal ni bure?.....dunia ya leo tunaongozwa na pesa.
  3. kama ni wauaji iweje mjisifie afya ya watanzania inaboreka?anayeboresha ni nani?acha wateteee matumbo yao kwani wakisubiri muwatetee watakufa njaa.
  4. mkuu hivi BOT,TRA,AICC,TANAPA sio watumishi wa umma?
  5. hata msipowalipa vizuri madaktari mbona hizo asprin na vifaa hatuvioni mahospitalini?
  6. sasa wakiishia kuzimu nani atatibu....mbona unaonekana wewe ni muuaji mkuu?
 
Hawa madaktari ni waislam nini? Mbona hawana huruma?

mkuu wewe si ndo umeanzisha thread ukitaka tuchangie mabati na hela kwa ajiri ya kujenga msikiti na ukaweka picha ya huo msikiti? kumbe ulitaka wakuchangie hela ukale na hadija uliye msema!. inawezekana hata goba hukai wewe. ban ni halali yako kwa kupotosha uma. ova
 
kama hii serikali itaendelea kuwa Kiziwi, natabiri jambo baya sana kutokea, USINIULIZE NIMEANZA LINI KUWA YAHYA HUSSEIN wa magomeni
 
Hawa madaktari ni waislam nini? Mbona hawana huruma?

Kaka unakosea kusema hivyo. Hivi unajua wapo waislamu wenye huruma kuliko hata wakristu?
Kwenye maslahi hakuna huruma, mbona bungeni wanadai maslahi makubwa kwani hakuna waislamu?? Wakrsitu nao si wapo?? Ni wangapi wameonesha huruma kwa kuzikataa posho?? Tafakari kabla ya kusema braza
 
MUNGU atusaidie mgomo huu usizidi kusambaa mawilayani, ni hatari sana
 
Kuanzia sasa siwaheshimu tena madaktari wa Tz.

Hawa ni mamluki, wanaongozwa na pesa si wito.

Hawana tofauti na wauaji. Wamekalia ubinafsi na kutetea matumbo yao.

Mishahara mikubwa wanayoipata inazidi watumishi wengine wa umma.

Hata hivyo hawaridhiki, tamaa imewajaa, wanataka kuikamua serikali mpaka umma ukose hata aspirin mahospitali???

Waishie kuzimu.

Kuanzia sasa siwaheshimu tena wana ccm pamoja na raisi wa Tz.

Hawa ni mamluki, wanaongozwa na pesa si wito.

Hawana tofauti na wauaji. Wamekalia ubinafsi na kutetea matumbo yao.

Mishahara mikubwa wanayoipata na ufisadi wanaouendesha unazidi watumishi wengine wa umma.

Hata hivyo hawaridhiki, tamaa imewajaa, wanataka kuikamua serikali mpaka umma ukose hata aspirin mahospitali???

Waishie kuzimu
 
Back
Top Bottom