MADAKTARI vs SERIKALI: Je, mimi nisiyekua waziri, mbunge au daktari?

Jul 3, 2012
92
13
Toka mgomo huu ulipoanza, nimekua nikijiuliza maswali mengi kadiri siku ziendavyo. Lazima nikiri kwamba na mimi nilitumbukia katika mtego wa kulaumu upande mmoja wapo kabla ya kujiuliza vizuri... Ama baada ya kutafakari kwa kina, nikagundua kwamba kwa vyovyote vila itakavokua, tunaoathirika ni sisi wananchi, bila kujali tunaunga mkono madaktari au serikali.


Nilianza kujiuliza hivi: Hawa wanasiasa wanaotupiana mpira, mara CHADEMA, mara CCM, bila kujali vyama vyao, wanatibiwa wapi kwa kawaida? Hawa kwani hawana madaktari maalum ambao wanawalipa binafsi? Hivyo basi, huyu kiongozi anayesema fukuza, hakutani na daktari wake binafsi ambaye huenda anatugomea sisi wananchi? Mimi mwananchi wa kawaida ambaye sijuani na daktari na wala sina pesa, nani atanitibia?


Je, nikisema serikali ifukuze madaktari wote, nani atanitibia? Nikisema pia wagome, kwani nikienda hospitali wataniuliza kama nawaunga mkono ili wanitibie? Au ndio yale ya "naunga mkono mgomo", lakini kwa sababu mimi sina jamaa daktari, au sio daktari, basi sina wa kunitibia. Lakini wao wanasema wananisaidia, ilihali wananiacha nateseka na wao wakitibia ndugu na marafiki zao!


Baada ya kuangalia hali yangu na hao viongozi wa siasa, bila kujali vyama vyao, nikajiuliza maswali mengine: Je, miongoni mwa madaktari wanaogoma, hawana wateja wao binafsi ambao ndio hao hao mawaziri wanaowatuhumu kufisidi sekta ya afya? Je, mawaziri hawa wakienda katika clinics zao binafsi wanawagomea? Je, ni kweli kwamba madaktari wote wanaoshiriki mgomo, hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kwa njia moja au nyingine kushiriki katika kufisidi sekta ya afya, iwe kwa kuiba panadol au vifaa vya malaki au hata mamilioni? Je, na wao wanahaki ya kusema kwamba wanagoma kwa sababu ya ukosefu wa vifaa?


Sikuishia hapo tu... nikajiuiza tena: vipi sisi wenyewe, ambao tunashangiia au kushabikia ama serikali kufukuza madaktari, au madaktari kugoma: Hakuna miongoni mwetu walioshiriki kuziibia hospitali zetu? Je, ni haki, kwa mwananchi mwenzetu, ambaye naye ameshiriki kufisidi hospitali, kunyoosha kidole, au kushabikia akisema serikali ifukuze, au madaktari wagome, wakati huyo naye ni sehemu ya tatizo?


Bado nikajiuliza maswali zaidi: Hivi tunaposikia serikali na madaktari wameshindwa kuafikiana, tunayachukua hivyo hivyo tu, au tunauliza kwa kina ni kwa nini wameshindwa? Tunaposikia serikali au madaktari wanasema wako tayari kwa majadiliano, tunawauliza ni hatua gani wanazichukua kwa ajili ya majadiliano, wakati upande mmoja unaendelea kufukuza na mwingine unaendelea kugoma? Tunapozikosoa taarifa zao, ni kwa sababu tumeamua kuchukua upande mmoja, au tunajua madhara ya mgomo huo kwetu sisi?


Maswali haya mengi yamenileta katika swai moja muhimu... Sisi wananchi, tusio wanasiasa, wala tusio madaktari au walau na ujamaa na daktari - tumekua tunatoa maoni yenye kuleta suluhu, au yenye kuchochea mgogoro? (bila kujali uko upande gani)


Watanzania wenzangu, katika hili, tunahusika wote. Kwa wale wanaosema madaktari wasigome, wasiishie tu hapo, watafakari sababu za matatizo ya sekta ya afya. Na kwa wale wanaosema wagome, wajiulize swai moja tu: Je, sababu kwamba ukosefu wa huduma bora kwa miaka kadhaa umesha sababisha vifo fingi, ni kisingizio haswa cha mgomo ambao na wenyewe pia unasababisha vifo na mateso?


Mimi na wewe tunafanya nini ili kurudishiwa huduma ya afya? Tuendelee kupiga siasa? au tutoe maoni ya suluhu?
 
Ukweli ni kwamba madaktari hawatapata huo mshahara wanaoutaka. Ili serikali iweze kuwalipa itabidi ichapishe hela. Jambo ambalo litadhoofisha uchumi, na kuharibu maisha ya madaktari na wagonjwa wao. Huu mgomo utayeyuka pole pole kama ulivyoanza. Kipigo cha Ulimboka kilitokana na watu waliojichukulia hatua zao wenyewe na sii kwamba walipewa amri za kumpa mkon'goto. Ninachofahamu ni kuwa kama lengo lao lingekuwa kumaliza, wangefanya hivyo.
 
Tatizo la serikali ya Tanzania ni kukosa vipaombele matokeo yake wanashindwa wafanye nini nini waache wamechukua mizigo mingi kwa pamoja ilhali hawawezi kuibeba na hawawez kuibeba kwa sababu ya kukosa uadilifu,kama toka tunaanza wangetambua kwambz afya ya Mtanzania ni ya msingi kuliko mambo yote ........ haya yote yasinge tokea lakini kwa kuamua kwao kwamba siasa ndio jambo la msingi kumepelekea yote haya kutokea leo hii madaktari nguli wanasheria waliobobea wanabinyana kuingia bungeni kwa nini wao hawajiulizi haya?.......
serikali ni lazima ibebe mzigo huu wa lawama sisi wanachi sio kazi yetu kujua kwa nini madaktari wamegoma tunachohitaji sisi ni huduma ya afya kama serikali ilivyoingia mkataba na sisi kama imeshindwa basi ni budi sisi wananchi tuvunje mkataba nao na kuuvunja mkataba ni kuiondoa madarakani..................
 
Naomba kuwa mchokozi, au "mdaku" kidoogo ndugu Gwankaja Gwakilingo... hivi, mfano tunaamua tuandamane kesho au hadi mpaka serikali itakapoeta huduma... hapa kati kati nani atakua anatutibia? Ni wazi kwamba wananchi wanapoweka serikali madarakani hua wanaingia katika "socia contract"... lakini ipi ni suluhu ya haraka ili tusipoteze watu zaidi? Kwani maisha ya kinamama wajawazito wenye kutaka kujifungua, au ajali, hazitosubiri harakati zetu za kisiasa...!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom