Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,268
- 17,097
Watatumia lugha gani kuongea na wagonjwa?
Katika mgomo huu SLAA ni mtuhumiwa numba moja. Asijifanye kukaa kimya kana kwamba wananchi hawajui hilo.
Mambo yakizidi kuwa mabaya asifikiri atapona , wananchi wataanza naye si alishasema kwamba nchi haitatawalika? kwa nini abaki? Kwanza yupo au kishakimbilia Karatu.
Tumelalama mgomo mgomo, umeanza sasa wasiwasi wetu nini Malengo yetu si yametimia? Tusiisakame tena Serikali. Tuliotaka kuwafurahisha tumeshawafurahisha. Nilifikiri sasa humu JF tungekuwa tunashangilia mgomo kuanza kwa akili zetu finyu tulivyokuwa tukiunga mgomo bila hata haya. Sasa mbona tunachangia kama tumeingia na hofu fulani? kwa nini tusiwe na ujasiri uleule?
Hizi akili kama vile nazi za pale magogoni..Walikuwa wanadai Mawaziri wajiuzulu. Yaani Madaktari bwana thehe thehe thehe, kwa hiyo wasipojiuzulu watoto wa Madaktwari haya hawatakwenda choo? Kazi kweli kweli. Daktari acheni hizo bwana. Mnajua kazi yenu kama kazi nyingine tu. Hivi Daktari ukipewa kazi ya kutengeneza hata stuli utaweza kweli? ukiambiwa umfundishe mtoto wa miaka mitatu hadi ajue kusoma utaweza? ukiambiwa kazi yako ni kuimba kwenye jukwaa ili watoto wako wapate kula utaweza? ukiambiwa ukatembee na viatu unauza mitaani kutoka Igoma hadi Nyakato, Ghana hadi Kirumba utaweza kweli Daktari? Basi hivyo wenzenu tunavyoteseka kuhakikisha familia zetu zinaishi. Kazi yenu kama kazi zingine
Ndugu zangu,
Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Serikali ipo kwenye hatua ya mwisho ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuleta madaktari kutoka nchi za Cuba, India na Cihina ili kuziba pengo kubwa lililoachwa na madaktari watanzania ambao wamegoma. Ninachojiuliza ni je, madaktari hao wa nje watalipwa na nani na watakaa hapa nchini kwa muda gani? Na je, manesi nao wakiamua kuwasindikiza madaktari, Serikali itafanya nini? Italeta manesi wengine kutoka nje?
Maswali haya na mengine mengi, yananielekeza kuamini kuwa suluhisho la suala hili ni kwa Serikali kuamua KUSHUKA kwa rais kukubali kuwastaafisha mawaziri wake kwa maslahi pana ya umma. Wapo wanaosema kwamba rais akifanya hivyo, atakuwa amejishusha sana. Lakini tujiulize, hivi ni nani mkubwa kati ya rais na wananchi kwa ujumla wao? Kwa nchi inayoheshimu utawala wa demokrasia kwelikweli, rais lazima atajiona kuwa yeye ni mtumwa wa wananchi wake. Kwa hiyo, inapotokea kelele za wananchi wake ambao ndiyo waajiri zimezidi, lazima achukue hatua hata kama wakati mwingine hafurahi kufanya hivyo. Asipofanya hivyo, kama ilivyo sasa kwa kikwete, ataendelea kuwatesa wananchi na kuwasababishia vifo ambavyo kimsingi vingeweza kuepukika.
Kauli ya anayejiita 'Mtoto wa Mkulima' Bw. Mizengo Pinda kwamba madaktari wanafanya makosa kumpa masharti BWANA MKUBWA yaani kikwete, imeniudhi sana. Ni kauli inayoashiria kibuli cha viongozi wa kiafrika. Kwamba rais ni bwana mkubwa asiyeweza kulazimishwa na mtu yeyote kufanya jambo fulani. Hili ndiyo tatizo la msingi la viongozi na hasa wa ccm kujiona kuwa kama MIUNGU MTU. Kwangu mimi, kiongozi anayefuata MATAKWA YA WANANCHI huyo ndiye kiongozi mzuri. Asipofanya hivyo, atuambie anafanya kwa maslahi ya nani!
Du,hii imekaa vizuri,ngoja nijiandae kuomba post ya ukalimani muhimbili,maana najua nafasi zitakuwa nyingi kwa sisi ambao ni billingual,hao madaktari wa Cuba na China kila mmoja atahitaji mkalimani wa kukaa naye wakati anamsikiliza mgonjwa wa kibantu,pia prescription ya Kichina manesi na watu wa Pharmacy watahitaji wa kuwatafsiria.Nadhani ahadi ya kuongeza ajira kwa watanzania itakuwa imetimia.Kidumu chama cha mapinduzi.
Sidhani kama umeelewa point yangu kamanda wangu, ni yaleyale tu gari laenda Pugu, we waenda Kimara unalipanda. Utafika lini kwenu?!!! Kwa ufupi mnauza ng'ombe kwa kesi ya kuku? Au unachinja ng'ombe kwa order ya maini?Kadandia vipi sasa? asitoe maoni yake? hao madaktari wasiwe kama watoto wadogo ambao wana demand kitu papo kwa papo,, naunga mkono serikali kuleta madaktari mbadala, tuone watakula wapi. Tusitake kunyanyasa wananchi hapa kisa eti daktari!! Na sisi wabeba zege tukigoma nani atawajengea majumba yenu? acheni upuuzi. Piga chini hao
Hapo penye rangi nadhani swali hilo linawahusu sana madaktari ambao eti kwa madai yao, wanaweka rehani maisha ya watu!! Hivi nani hana madai Tanzania hii? Watu wafe ili wewe upate unachotaka?? si ndiyo kuchinja ng'ombe upate maini?? Wee hii methali unaijua au umei copy tu?? Rudi darasaniSidhani kama umeelewa point yangu kamanda wangu, ni yaleyale tu gari laenda Pugu, we waenda Kimara unalipanda. Utafika lini kwenu?!!! Kwa ufupi mnauza ng'ombe kwa kesi ya kuku? Au unachinja ng'ombe kwa order ya maini?
Watanzania hawajaelewa ukweli kuhusu madai ya Madaktari. Its not about the money. Kuna recognition ya mchango wao kwenye taifa. Kupotea kwa thamani ya profession ya Udaktari. Ilifikia kiwango yule Mama anawaambia eti Nani aliwatuma mkasomee udaktari. Its about time the country places priority and value to this special and rare profession. From working environment to supportive facilities Waache siasa wasolve matatizo yanayo wakabili madakatari kitaalamu. Kwani
Hilo si tatizo,, kwanza elewa kwamba si mikoa yote wamegoma. Morogoro, KCMC, Singida, Tabora etc madaktari wanachapa kazi kama kawaida. Sasa hapo ndipo serikali itayumia divide and rule,, kwamba wanaotaka kazi apply upya kushirikiana na hawa wanaotoka nje. Na pia si taabu maana tunao madaktari wanajeshi ambao watatoa ushirikiano mzuri tu kwa wataalamu wa "UKWELI" toka nje. Karibuni sana wataalamu nchini kwetu. Unauliza kwa gharama ya nani?? wee unaijua gharama ya uhai wa watu wanaoathirika na mgomo huu?? mbona hilo unalifumbia macho? ni gharama ya nani? Unauliz kwa faida ya nani?? Hapa napata mashaka kuhusu uelewa wako.Hivi hiyo orientation hao wahindi na wacuba watapewa na nani?. Nasikia wajeshi wenyewe walizimia walipoingia Muhimbili. Na je wataweza kuwaleta katika kila kituo cha mkoa? kwa gharama ya nani? kwa manufaa ya nani?
Walete vipi?? kwani wanasheria wamegoma au wahandisi?? Hao ni watu makini hawwajiingizi katika migogoro hasi kwa TaifaTatizo la nchi hii hatuna viongozi wenye uwezo wa kufikiri. Basi na walete walimu, wanasheria, wahandisi na wengineo kutoka huko wanakosema.
manesi wataazimwa hospitali ya apolo, india.
Na pia watafunza wengine kwa crush program.
Ila hawa viongozi wetu, sidhani kama ni wazima.
Ndugu zangu,
Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Serikali ipo kwenye hatua ya mwisho ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuleta madaktari kutoka nchi za Cuba, India na Cihina ili kuziba pengo kubwa lililoachwa na madaktari watanzania ambao wamegoma. Ninachojiuliza ni je, madaktari hao wa nje watalipwa na nani na watakaa hapa nchini kwa muda gani? Na je, manesi nao wakiamua kuwasindikiza madaktari, Serikali itafanya nini? Italeta manesi wengine kutoka nje?!
Ndugu zangu, Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Serikali ipo kwenye hatua ya mwisho ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuleta madaktari kutoka nchi za Cuba, India na Cihina ili kuziba pengo kubwa lililoachwa na madaktari watanzania ambao wamegoma. Ninachojiuliza ni je, madaktari hao wa nje watalipwa na nani na watakaa hapa nchini kwa muda gani? Na je, manesi nao wakiamua kuwasindikiza madaktari, Serikali itafanya nini? Italeta manesi wengine kutoka nje?!
Too late. Ushabiki wa Wanaharakati, wanasiasa na hata baadhi ya watu wengine wa kawaida kabisa hata ambao hawana uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya Kata zao hatukuliona kama hilo ni tatizo lililochangia kukua kwa hamasa ya madaktari kugoma. Tuache Serikali itekeleze majukumu yake. Tukianza kuhoji kama Serikali itaweza hayo sasa majungu. Suala la wageni watalipwa shilingi ngapi , ni lazima tukubali hizo ndizo gharama zenyewe hasa pale wazalendo wanapokosa uzalendo. Ikibidi sasa hata mishahara ya Watumishi ipunguzwe zaidi ili kukabiliana na tatizo , hii ni kama vita huwezi kukwepa uwe unaunga mkono mgomo au la. Letu sote.