Polisi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,082
- 639
Nimekuwa nikisumbuliwa na ugonjwa ambao unanichanganya sana na nimedumu nao kwa miaka 12 sasa. Mwili kuwaka moto na maumivu kwenye kifua. Mara nyingi huanza maumivu makali kwenye kifua, si kubana bali ninavyosikia ni dhahiri kama kuna vidonda maana wakati fulani panaweza kupoa kabisa, lakini labda ukipata chakula fulani au hata kinywaji maumivu yanaanza. Hapo viungo vingi vya mwili huanza kuwaka moto ikiwemo mikono, miguuni kwenye nyayo, sehemu yote ya kichwa pamoja na maumivu kwenye mgongo. Wakati mwingine nasikia maumivu makali kwenye kifua lakini baadhi ya viungo hususani mikono huonekana kama inauma lakini kana kwamba ina ganzi.
Mwanzoni ilibainika ni ulcers, nikatumia sana dawa za hospitali na nikapima vipimo pale muhimbili na kuendelea na dawa za hospitali na kienyeji ikiwemo ya dr . rahabu. Hivi karibuni nimepima mara mbili na kuambiwa ulcers imepona. Cha kushangaza bado maumivu makali kwenye kifua.
Nimeona niulize hili maana wiki hii nina appointment na dr. mmoja ambapo nataka nimwombe anipige x ray.Naomba mnisaidie kuutambua ugonjwa huu ili niwe na input ya kutosha kumsimulia daktari. Kuna daktari mmoja alishawahi guess kuwa yawezekana ini likawa na tatizo na akanishauri nitumie mitishamba. nilitumia kwa siku 7/15 nikakatisha dozi baada ya maumivu kuzidi kuliko kawaida.
Naombeni msaada wenu wakuu
UPDATE 13/09/2011
Nilikwenda hospitali ya muhimbili kama watalaamu humu walivyonishauri na kufanyiwa kipimo cha endoscopy. Majibu ni kwamba hakuna vidonda vya tumbo bali kuna fungus kwenye kifua na nikapewa dawa inaitwa fluconazole kwa siku 14. Baadaye nikaenda regency kwa ajili ya x ray na majibu hakuna tatizo.
Hali yangu baada ya kumaliza dozi
Kwa kweli najisikia vizuri ingawa bado maumivu nayasikia wakati fulani ingawa si makali kama awali. Nadhani fungus hazijaisha. So naombeni ushauri nirudie dozi au nitumie dawa gani tena.
Wasalaam