Madaktari na ukombozi wa tanganyika

Dec 5, 2011
78
93
Wanasiasa katika jamii yetu wamekuwa wakiwachukulia madaktari kama watu ambao muda mwingi wako na wagonjwa na wajui mambo ya kijamii yanayoendelea, imefika wakati hata sitahiki zao ambazo ziko wazi katika "goverment standing order' wananyimwa bila sababu ya msingi. mfano interns drs waliodai mshahara wao wa mwezi ambayo ni haki yao, baadae walipewa na kufukuzwa muhimbili!

Ukweli ni kwamba drs wamehusika sana katika ukombozi wa kisiasa wa tanganyika na dunia kwa ujumla.

Naomba nitoe mifano miwili.

Kwanza ni Dr. Vedasto Kyaruzi ambaye alikuwa president wa TAA mwaka 1950 na katibu wake akiwa Abdulwahid Sykes. Kabla ya kuingia kwa huyu daktari TAA ilikuwa ni chama cha kijamii ambacho hakikuwa na mwelekeo wa kudai uhuru.

Dr. huyu ndiye aliyeleta mapinduzi makubwa akiwa kama president wa TAA wakati Nyerere anakuja kujiunga na harakati za kudai uhuru msingi mkubwa ulishaandaliwa na huyu Dr. kyaruzi, kwa bahati mbaya watanganyika wengi hawajui/hawajaelezwa mchango wake i.e forgatten people.

Mfano wa pili ni Dr. Che Guevara huyu alikuwa ni daktari na mwanamapinduzi wa ukweli ambaye amepigana vita vya msituni na kufanikisha uhuru wa CUBA, ukombozi wa DRC etc.

Sasa hivi kuna harakati nyingi za ukombozi wa jamii yetu zikioongozwa na CHADEMA.

Madaktari nao sasa wameamua kujiunga katika vita hii. Mfano mzuri ni Mh. Zitto leo alivyojitokeza bungeni kajitokeza kuwatetea ingawa inaonekana anaweza kupata upionzani mkali kutoka vyama vingine.

Kwa vile fikra za madaktari hawa zinaendana na fikra za CHADEMA ni ukweli usiopingika kwamba madaktari watapambana bega kwa bega kama alivyofanya dr. Che Guevara na Fidel Castro.

Drs are people of their words, when they say it they mean it. When they are ready to die for something, they know know what death is, because they have been seeing dead people everyday!

Hii ndio tabia ya Drs (people of their words) ambayo pinda alikuwa haijui, alifikiri akipiga mkwala , kesho watakuwa wanakanyagana kuwahi ofisini.
 
Dr. Kyaruzi amefariki juzi jijini DSM, mwili wake umesafirishwa leo, mazishi ni J.5 kwao Bukoba.
 
tukatae ila madokta wana influence kubwa kwenye chochote ndani ya jamii pamoja na umskini wao
 
Back
Top Bottom