Madaktari na serikali kuanza mazungumzo wiki ijayo

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
kuna taarifa nimezipata kuwa madaktari na serikali wataanza mazungumzo ya kina mapema wiki ijayo.hii imekuja baada ya maombi ya madaktari kutaka mazungumzo ya dhati na serikali.

Napenda kuwapongeza madaktari kupitia kamati yao kuruhusu meza ya majadiliano pamoja na machungu ya kutekwa,kuteswa na kuumizwa kwa dr ulimboka.nategemea serikali itakuwa makini ili kumaliza mgogoro huu.

Ikumbukwe kuwa mgomo wa madaktari haujaisha kama tulivyoaminishwa na vyombo vya habari na pia kuna wimbi kubwa la madaktari kukimbia nchi na kutafuta maslahi bora hasa baada ya mgogoro huu wa muda mrefu.
 
Anaesema mgomo umeisha ni ccm kama ilivokawaida ya ccm hawana huruma na watanzania wao kazi yao ni kwa manufaa ya matumbo yao 2
kuna taarifa nimezipata kuwa madaktari na serikali wataanza mazungumzo ya kina mapema wiki ijayo.hii imekuja baada ya maombi ya madaktari kutaka mazungumzo ya dhati na serikali.
Napenda kuwapongeza madaktari kupitia kamati yao kuruhusu meza ya majadiliano pamoja na machungu ya kutekwa,kuteswa na kuumizwa kwa dr ulimboka.nategemea serikali itakuwa makini ili kumaliza mgogoro huu.
Ikumbukwe kuwa mgomo wa madaktari haujaisha kama tulivyoaminishwa na vyombo vya habari na pia kuna wimbi kubwa la madaktari kukimbia nchi na kutafuta maslahi bora hasa baada ya mgogoro huu wa muda mrefu.
 
I hope Iddi simba hatakuwa mmoja wa negotiators.

hivi kumbe huyu fisadi alikuwemo? Kama nani serikalini? Ndo maana muafaka ulikuwa mgumu maana nilisikia kila siku alikuwa anakuja mtu mpya na kuanza kubisha asichokijua. Inabidi muanze kumuelezea badala ya kwenda mbele.
 
Njia mojawapo nzuri ya kurudi mezani kuzungunza na madaktari, ni kuhakikisha kwanza matakwa yote ya madaktari yanatekelezwa (kuboresha mazingira ya kazi, vifaa vinavyokosekana mahosptalini vinapatikana n.k) ila linabaki moja la mishahara ambalo za sasa wakae meza moja kulizungumzia lakini baada ya kuwarudishia leseni zao za kazi.

Wanajanvi: Kuna tetesi kuwa vifaa vingi 'basic' vya mahospitalini vimeibwa na madaktari wenyewe hasa wale ambao wanaendesha bihashara ya kliniki pamoja na maduka ya dawa. Je hii ina ukweli wowote?
 
Madaktari wenye uzalendo na nchi yao hawatakimbia katu ,na hao wanaokimbia huko waendako hawatakuwa na thamani ,bado wataitwa ni wakimbizi.Na zaidi watadharauliwa tu na kutupiwa maneno ya kejeli utabibu utapoenda kombo.
 
Tunadanganyana tuu hapa, kesi ipo mahakamani na selikali ilishafanya conclusion ya kuwanyang'anya leseni ila wajifunze na next month new interns imeshakula kwao wao si waligoma waendelee kugoma na wanaotaka kwenda nje waende mambo yatakwenda tuu na wanaendelea kupata ugumu mtaani
 
mkuu hivi hujui kama kuna mgomo wa specialist kukataa kuwasupervise interns watarajiwa?
 
Yule jamaa anayeishi kwenye Nyumba yetu bure kule magogoni,
si alishakataa sasa hayo mazungumzo ni ya nini tena?
 
Back
Top Bottom