Madaktari live mlimani tv

Kwa hisani ya Henge: ''Kwanza, serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe''.BY JAKAYA KIKWETE.

Ina uwezo wa kuwashurtisha madaktari kibabe warudi makazini
 
ktk hili sakata, madaktari watashindwa.... Huwezi kucheza na serikali ukabaki salama.
Nawahurumia wale wenzangu na mimi wanaofuata mkumbo na mwishowe kupoteza ajira.
Rudini kazini.....otherwise ...very soon mtagundua kuwa mlikuwa mnapoteza muda na imeshakula kwenu.

pointless!!!!!!!!!!!!

Mbona nigeria wananchi wameshindana na serikali kuhusu ruzuki katika mafuta

na wananchi wameshinda kwani serikali imekubali kurudisha ruzuku.

Mizambwa
inaniuma sana!!!!!!
 
Mimi naunga mkono asilimia 100, mgomo wa Mdaktari. SErikali imezoea kutumia nguvu kila haki inapodaiwa. Na hii yote ni katika kurudisha nyuma harakati za kudai haki, ndio maana wanatumia vitisho. Kuwafukuza kazi madaktari wote ni ngumu sana kwani hata hao madaktari wa Jeshi ni wachache na ieleweke kuwa si kwamba Wanajeshi hawana kazi. nao pia wapo katika Hospitali zao wanatibu wagonjwa, hivyo maringo na kutamba kwa Serikali kuwa itawatumia Wanajeshi siyo suluhisho la matatizo.

Pia ieleweke kuwa hata Hospitali za jeshi madaktari bingwa wengine wanatoka hospitali za Serikali, hivyo kote kuna uhaba wa Madaktari.

Mh. Pinda acha Jazba tafuta suluhisho kama lilivyopatikana katika kuongeza Posho za Wabunge, mbona hamkuwa na jazba???????

MIZAMBWA
INANIUMA SANA
 
Zile operation za mguu badala ya kichwa na kichwa badala ya mguu is coming soon.
 
mnacheza na madaktari nyie? mtawafanya sehemu ya kuandikaklorokwini waandike panado mkafie makwenu. unaenda unaumwa wanakuambia hauumwi. bora wawasikilize kuokoa watu wasio na hatia. wakilazimishwa wanaweza kwenda kazini lakini wakawa wanafanya kazi isivyo, je pinda ataenda kumwambia doctor kwanini ameandika dawa isiyo?. nawaunga mkono madokta. naomba wasikilizwe. mia
 
Ktk hili sakata, Madaktari watashindwa.... Huwezi kucheza na Serikali ukabaki salama.
Nawahurumia wale wenzangu na mimi wanaofuata mkumbo na mwishowe kupoteza ajira.
RUDINI KAZINI.....otherwise ...Very soon mtagundua kuwa mlikuwa mnapoteza muda na imeshakula kwenu.

Katika hili watakaoshindwa ni wananchi.madokta hawana shida wala viongozi kwani wataenda kutibiwa India au UK.Hata kama wakirudi tutegemee rushwa zaidi na kuzorota kwa huduma....Hata siku moja mtu hawezi fanya kazi bila furaha halafu kuwe na tija.Katika hili tuache ujinga wa kushabikia siasa.serikali lazima iwe na maamuzi ya busara kama kweli inawapenda wananchi wake.
Kumbukeni Udaktrai ni Wito ..lakn jiulize wenye wito huo ni wangapi katika madokta wote wa bongo.
 
mnacheza na madaktari nyie? mtawafanya sehemu ya kuandikaklorokwini waandike panado mkafie makwenu. unaenda unaumwa wanakuambia hauumwi. bora wawasikilize kuokoa watu wasio na hatia. wakilazimishwa wanaweza kwenda kazini lakini wakawa wanafanya kazi isivyo, je pinda ataenda kumwambia doctor kwanini ameandika dawa isiyo?. nawaunga mkono madokta. naomba wasikilizwe. mia

Ni kweli..Madaktari wasikilizwe..
 
Ina uwezo wa kuwashurtisha madaktari kibabe warudi makazini

...Hivi mtu mzima anashurutishwaje kibabe? tena mwenye elimu yake?, ni aibu sana kwa madaktari kufyata mkia kama mbwa koko, wasomi gani hawa wasiojiamini?nazidi kuwa na mashaka na uweredi wao, isijekuwa tuna makanjanja tu kwa jina na cheti cha udaktari....
 
Mimi naunga mkono asilimia 100, mgomo wa Mdaktari. SErikali imezoea kutumia nguvu kila haki inapodaiwa. Na hii yote ni katika kurudisha nyuma harakati za kudai haki, ndio maana wanatumia vitisho. Kuwafukuza kazi madaktari wote ni ngumu sana kwani hata hao madaktari wa Jeshi ni wachache na ieleweke kuwa si kwamba Wanajeshi hawana kazi. nao pia wapo katika Hospitali zao wanatibu wagonjwa, hivyo maringo na kutamba kwa Serikali kuwa itawatumia Wanajeshi siyo suluhisho la matatizo.

Pia ieleweke kuwa hata Hospitali za jeshi madaktari bingwa wengine wanatoka hospitali za Serikali, hivyo kote kuna uhaba wa Madaktari.

Mh. Pinda acha Jazba tafuta suluhisho kama lilivyopatikana katika kuongeza Posho za Wabunge, mbona hamkuwa na jazba???????

MIZAMBWA
INANIUMA SANA

Na mimi nakuunga mkono 100%, PM jana alikuwa anacheza na takwimu sana ila alisahau kutuambia, jeshini kuna maMD wangapi. Maana kwa kuwahadaa wananchi, ametaka tuamini kwamba kuna idadi kubwa ya madaktari ambao wanahang hang tu hawana kazi, na hivyo itakuwa rahisi kuwapata. Anajiplacebo kwamba, kwa kuwa mikoa 13 haijaengia kwenye mgomo, basi hali itaendelea hivyo hivyo. Amesahau kuwa, kuna wale ambao siku zote, wanasubiri wengine waanze, then wanafuata.

Lakini pia amesahau kuwa mgomo baridi ni rahisi sana kuuendesha na ndio wenye impact kubwa hata kuliko kuandamana na mabango barabari. OK, fine si alisema yuko tayari kudeal na changamoto itakayotokana na mgomo huu, badala ya kusolve chanzo cha tatizo, kazi kwake.

Nashukuru tu kwamba jana ametangaza rasmi kwamba serikali yetu, kazi yake ni kushughulika na impacts badala ya kudhibiti causes. Bravo, PM.
 
...Hivi mtu mzima anashurutishwaje kibabe? tena mwenye elimu yake?, ni aibu sana kwa madaktari kufyata mkia kama mbwa koko, wasomi gani hawa wasiojiamini?nazidi kuwa na mashaka na uweredi wao, isijekuwa tuna makanjanja tu kwa jina na cheti cha udaktari....

Mimi Madaktari wakishindwa kwenye timbwili hili sitawalaumu kabisa maana ninaelewa kuwa pamoja na madai yao binafsi yapo madai ambayo ni kwa ajili yetu. Huduma na vifaa vya kufanyia kazi vinatuhusu sisi. Sasa wakifyata mkia nasi tufyate midomo yetu kwani tumeshindwa kuungana nao hata kwa hayo yanayotuhusu na sie.
 
Serikali za hizo nchi hazikuangushwa na ma dr vilaza, ziliangushwa na wananchi.
For your info, Wa tz wanawashangaa ma dr wanaogoma, majority hawakubaliani na madai yao ya kipuuzi.

Majority yako umeipataje? Hii ndio inayoitwa "ostrich philosophy", unawasemea watu ambao hata hujawauliza, unajizulia jibu ambalo ungependa liwe halafu unakiamini hicho ulichokizua!
 
Serikali ishindwe? waulize magwanda na wanafunzi wa mlimani.

Kukutana ni madaktari waliofanya dharau jana, Waziri Mkuu kawangoja hawakutokea, walitaka wabembelezwe? Mwanachi ataekuwa nyuma ya hawa na kuwaunga mkono huyo haitakii mema Tanzania.

nilitaka nijibu,nilivyoona ni wewe ngoja nikusalimie tu
 
PM amewasubiri kwa muda wa kutosha pale Karimjee jana, hawakutokea ili wasikilizwe.
Inavyoonesha, hawa ma Dr walikuwa wanadanganyana na kufanya uhuni tu kwenye vikao vyao.

kwani inapotokea kuailishwa huwezi kuwapa second chance mkuu mpaka utoe vitisho kama hivyo!
 
Serikali ya kijambazi ya CCM isiyokuwa na kichwa wala miguu,inawanyanyaswa watanzania waliokatika nchi yao,madaktari tupo pamoja na nyie katika kudai haki zenu,hi serikali dhaifu na legelege ya CCM siku zake zinahesabika.
 
Ingekuwa hamu yangu wangegoma wote then tungeona serikali ingefanyaje?
Bse hawa watu sio vichaa wana madai ya msingi sana,kutojitokeza kwao jana kulikuwa na sababu.
Kama serikali haiwajari kama madakatari basi ianze kuwajari kama raia wa Tanzania na siasa ziwekwe kando
 
Tatizo serikali yetu imeona suluhu siku hizi ni kutumia mabavu, mbona posho za wabunge hawakutumia mabavu?

viongozi wa nchi hii wapo kimaslahi yao tu,hawataki kusikiliza matatzo a wenzao,
naomba madaktari waendelee kugoma hadi kieleweke
 
Ktk hili sakata, Madaktari watashindwa.... Huwezi kucheza na Serikali ukabaki salama.
Nawahurumia wale wenzangu na mimi wanaofuata mkumbo na mwishowe kupoteza ajira.
RUDINI KAZINI.....otherwise ...Very soon mtagundua kuwa mlikuwa mnapoteza muda na imeshakula kwenu.

Halafu wakisharudi hao madaktari unategemea huduma itakuwaje? Hali hawana moral yakufanya kazi kutokana na kutotekelezwa kwa Yale wanayodai? Ubabe siyo dawa jamani kinachohitajika ni mazungumzo ambayo yataleta muafaka wakudumu
 
Back
Top Bottom