Madaktari leo kujadili sakata la Ulimboka

Waseme tu hili Jeshi sio la kuliamini kabisa hili bora mtu ujulinde mwenyewe tu.

skuizi wanauwana wenyewe kwa wenyewe! wamemuua mwenzao morogoro wanasema kajinyona! shame on them! siwapendi hawa jamaa! yani kule mpakani kutokee vita hata ya masaa 4 tu! alafu hawa mafala wapelekwa kama chambo wafe wote.
 
dr.ulimboka sema ukweli kuficha mambo kutakuletea matatizo kumbuka mwakyembe alificha mambo walichomfanyia ni kumuua taratibu.....ukweli ndio pona yako
 
Kwani wewe umekuwa gazeti? Mbona maneno haya yanaonekana wazi umetoa kile ulichokisikia tu mitaani? Familia ya Ulimboka haina msemaji wa Familia mpaka Madaktari waongee kwa niaba yao, kwa sababau naona kama kikao hicho ni cha familia.

Kawaida yako kupotosha, haikusaidii kwani ukweli utajitenga tu.
 
Monday, 06 August 2012 22:04


Fidelis Butahe
WAKATI kukiwa na taarifa za kurejea nchini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka viongozi wa Jumuiya hiyo na Umoja wa Madaktari Tanzania (MAT), wanatarajia kukutana leo kujadili mkanda mzima wa sakata lililomkumba kiongozi huyo. Baada ya kikao hicho, madaktari hao watakutana na familia yake na kisha kumuuliza Dk Ulimboka kama angependa kilichomtokea kiwekwe wazi kwa jamii.

Dk Ulimboka ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari uliokuwa ukiendelea nchi nzima, alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumatato ya Juni 27 mwaka huu na kupelekwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji a Dar es Salaam, ambako aliteswa na kujeruhiwa vibaya.

Katika tukio hilo daktari huyo aling’olewa meno mawili na kucha za mkono mmoja na baadaye kulazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI). Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya Juni 30 mwaka huu, alisafirishwa kwenda Afrika a Kusini kwa ajili ya vipimo na matibabu.

Kusafirishwa kwake kulifuatia taarifa ya jopo la madaktari lililokuwa linamhudumia kutoa taarifa kwa madaktari bingwa kuhusu abadiliko ya afya.

Taarifa za kurejea kwa Dk Ulimboka zimezagaa katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, huku baadhi ya watu wakizijadili katika mitandao ya kijamii. Akizungumza na gazeti hili Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwin Chitage, alisema kuwa hali ya Dk Ulimboka inazidi kuimarika lakini alisita kueleza wazi ni lini kiongozi huyo wa madaktari atarudi nchini.

“Tukiwa tayari tutatoa taarifa katika vyombo vya habari juu ya suala zima la afya ya Dk Ulimboka,” alisema Dk Chitage. Alisema leo au kesho viongozi mbalimbali wa MAT na Jumuiya ya Madaktari, watakutana kujadili suala la kiongozi huyo.

“Ndani ya siku mbili hizi (leo na kesho) viongozi tutakutana na kujadili ripoti ya matibabu ya Dk Ulimboka na tutajadili kama tuvieleze vyombo vya habari ama laa,” alisema Dk Chitange. Hata hivyo Dk Chitange alisema hatua hiyo itategemea na kauli ya familia ya Dk Ulimboka na yeye mwenyewe (Dk ULimboka) kwa kuwa na wao pia watashirikishwa.

“Dk Ulimboka na familia yake tutawashirikisha katika mambo ambayo tutayajadili,” alisema Dk Chitage.

Alipoulizwa kama kiongozi huyo wa madaktari sasa anaweza kufanya shughuli zake kama awali, alisema hana uhakika kwa kuwa hana taarifa za ndani zaidi .

 
kesho nitakua eneo ambalo nitapata news kinagaubaga,ha ha nitawaletea yatakayojiri
 
UGHONDU na wale wenzako tunawajua!! Habari za mwanahalisi zimetoka kwa DR mind you!!
TISS ni Majambazi period!!

Ni ukweli upi Watanzania tunaotaka kuusikia tofauti na ule aliousema Ulimboka mwenyewe kwenye ile clip ya mahojiano? Wahusika alishawataja labda kama ni details zaidi ambazo kwakweli sidhani kama zitatusaidia chochote zaidi yakupandisha hasira pasipo vitendo.
 
Pasiwekwe wazi taarifa hiyo kwani nani ataiamini sana sana itachochea mengine kutumia taarifa ambayo haiaminiki na wote. Cha busara ni kuwa na tume huru kuchunguza mambo yote halafu watuletee na hiyo ndiyo taarifa ya kuzungumza kama iwekwe wazi au la.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom