Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,539
- 19,390
Jimy P Analysis yako ni bomu kabisa. Kama nchi ni maskini kiasi cha kutoweza kuwalipa mishahara hiyo madaktari basi serikali ingekuwa imepunguza matumizi yake ikiwa ni pamoja na mishahara ya vi9ongozi wa serikali kama wabunge, mawaziri na watu wa aina hiyo. Vile vile serikali isingekuwa inatumia pesa hovyo hovyo kama kununua rada isiyofanya kazi. Marekani mshahara wa Senator ($180,000) kwa mwaka ni karibu sawa na huenda ukawa chini ya mshahara wa daktari ambao huanzia $150,000 hadi $400,000 kwa mwaka; Tanzania mshahara wa mbunge ni zaidi ya mara tano ya mshahara wa dakatri, haki iko wapi hapo?
Vipaumbele vibovu vya serikali ndivyo vinavyofanya watu waone kuwa ina pesa lakini haitaki kuwalipa wafanya kazi wake mishahara sahihi.
Vipaumbele vibovu vya serikali ndivyo vinavyofanya watu waone kuwa ina pesa lakini haitaki kuwalipa wafanya kazi wake mishahara sahihi.
Last edited by a moderator: