Madaktari kutoka Tanzania wapokelewa kwa heshima Botswana

Delegate

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
331
201
hapa tunapoongea sasa hivi wamepokelewa madaktari watano kutoka Mbeya tanzania na tayari residence permit zao zinatengenezwa ili kuanza kazi mara,
watakuwa wanafanya kazi hospitali za Gaborone city council na mishahara yao itakuwa allmost mara saba ya mshahara waliokuwa wanapata tanzania wa laki tisa

My take:
serikali ya tanzania isifikiri inawakomoa hawa madaktari ambao nchi za huku kusini zinaheshimika kuliko jambo lolote lile,kama walifikiri wanawakomoa kwa kutumia SADC ili wasipate kazi huku wajua serikali ya Botswana ni serikali imara na madhubuti na haiendeshwi kinafiki
 
Bravo.

Namkumbuka Dr. Kimaro (RIP) aliyekuwa Rais wa DARUSO miaka ya 1992, Rais Mwinyi aliapa kuwa hatafanya kazi yeyote Duniani, lakini Botswana alifanya kazi.
 
Hata katika hotuba ya kikwete aliwaruhusu waende popote ambapo mwajiri atawalipa hizo hela wazitakazo na aliwaombea mafaniko mema.
 
Kitu kimoja naipendea Tanzania,
inasomesha bure madaktari.
Inalipa fees,
inalipa boom,
ila inapofika kutumia matunda ya walichopanda hawana mda nacho,
"Ondokeni mkamtafute mwajiri anayelipa vizuri" Baba Mwanaasha aka Vasco de traveller
 
Bravo.

Namkumbuka Dr. Kimaro (RIP) aliyekuwa Rais wa DARUSO miaka ya 1992, Rais Mwinyi aliapa kuwa hatafanya kazi yeyote Duniani, lakini Botswana alifanya kazi.

Are you saying Dr. Kimaro ni marehemu kwa sasa? Alifariki lini? Alikuwa kiongozi wangu imara aliyewezesha maandamano kufanyika hadi kwenye geti la Magogoni!!!!

Tiba
 
kumbe uropokaji ulianza kitambo katika serikali hii ya ANGUKA(Ari Zaidi, NGUvu zaidi, KAsi zaidi)
 
JK hasira hasara!
Kumbuka hawa watu uliingia gharama kuwasomesha leo hii wanasepa!
Indirectly unaccerelate anguko la CCM 2015
 
Are you saying Dr. Kimaro ni marehemu kwa sasa? Alifariki lini? Alikuwa kiongozi wangu imara aliyewezesha maandamano kufanyika hadi kwenye geti la Magogoni!!!!

Tiba

Ni karibu miaka mitatu imepita. Kama utakuwa na taarifa ya kugombea mali zake ambapo hata Mch. Mtikikila alikuwemo kumdhulum mke wake(RIP). Kimaro was a good leader ambaye alifanya kazi na Katibu Rutashoborwa(RIP)
 
Mimi nawashangaa watu wanaosema Madokta waende.Hivi huwa mnatembelea Shule zetu kuona jinsi Wanafunzi wengi wanavyoyaogopa masomo ya Sayansi?.Hata hao ambao wanaenda huko wanenda kusoma nadhari kwani shule hazina Maabra kwa ajili ya Masomo hayo.Watanzania tumechanganyikiwa hata hatujui dunia ya sasa inaendeshwaje.
 
Sasa wafanyeje? Unataka wabaki ili wang'olewe meno na kucha kwa prize! Tulikimbilia UNGWINI basi tufe na ungwini wetu
 
mwanangu ndio anasema eti anataka kuwa dokta, nilikuwa namkazania sana sasa anajua sayansi na hesabu sana, ila na mimi nataka kubadili mawazo nisishabikie huo udaktari anaouota, nadhani asome siasa,
hivi huwa wanasoma wapi vile?
 
Nawatakia kila la Kheri huko walipo.

Mwenyezi MUNGU awazidishie afya na maarifa maradufu!
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom