Madaktari kukutana kesho kufanya tathmini ya makubaliano na serikali, kuna harufu ya mgomo kuendelea

Madaktari kuweni waangalifu sana. Safari hii kazi mtakosa. Mliweza kusimama pamoja kwa sababu mlikuwa na uhakika wa mishahara yenu kuikuta Bank. Kila mtu ana shida zake na si kila mtu anaweza kufanya kazi private, hapo ndipo mtakapogeukana na kusambaratika kila mmoja na njia yake. Utashangaa maombi ya kurudi kazini yatavyokuwa mengi. Ikifika suala la kuona watoto wanalala njaa in the name of solidarity forever ndo tutaona mshikamano wenu.

Safari hii laaaazima watawaangukia. Ngoja tuone...
 
Habari za kuaminika zinadai kuwa Serikali haina fedha completely, kuna sekta hazijapata mishahara ya mwezi Februari mpaka leo. Kwa hiyo JK anaposema ngoma nzito ana maanisha kuwa hsta akiyakubali madai ya madaktari je atatosa wapi fedha za kuwalipa.
ajitokeze aseme sasa kama ana sababu za kufirisika watamwelewa kama hana ajiandae kueleza huko anakopata pesa za kuandaa hizo maulidi za kiselikali
 
Kama kada nyingine za afya nazo zina madai yake basi ni muda muafaka kuungana na madaktari, nurses, phamacists, radiologists,.......
 
ulimboka ana degree ya udaktari namaanisha doctor of medicine ukigraddduate chuo cha udaktari wewe ni daktari hata usipo fanya internship,bwana mpona na bwana pinda hili walikuwa hawalijui,nakwambia hivi kwa sababu hata ukiwa unaenda kufanya internship wizara inakuadress kama doctor,na kuna madaktari wengi ambao hawajafanya internship na wanafanya mambo mengine.
Ngoja niwahi water front kwa maamuzi magumu

updates please, nipo katavi...
 
Mbona hao mafamasia na mafundi maabara hatujawasikia? Au wao wanasubiri maswala yanyooke ndiyo wafaidi vya bwelele
 
Madaktari kuweni waangalifu sana. Safari hii kazi mtakosa. Mliweza kusimama pamoja kwa sababu mlikuwa na uhakika wa mishahara yenu kuikuta Bank. Kila mtu ana shida zake na si kila mtu anaweza kufanya kazi private, hapo ndipo mtakapogeukana na kusambaratika kila mmoja na njia yake. Utashangaa maombi ya kurudi kazini yatavyokuwa mengi. Ikifika suala la kuona watoto wanalala njaa in the name of solidarity forever ndo tutaona mshikamano wenu.

Safari hii laaaazima watawaangukia. Ngoja tuone...

Ndiyo maana ya mapambano hiyo!
Huwa hatupambani kwa ajili ya nafsi zetu mjomba... Tunapambana kwa ajili ya msingi bora wa Taifa,leo na kesho...
Kwa hiyo,ku-sacrifice,kazi,uhai,ama chochote kile kingine,ni mojawapo ya mbinu ngumu za mapambano! Na yeyote kwenye uwanja wa mapambano anayerudi nyuma kwa kuogopa kazi,au uhai wake wakati huo hujulikana "msaliti"...
Na vitani,dawa ya msaliti(traitor),inajulikana ...... KIFO tu...!

Qoute: Revolution is not an Apple that falls when it is ripe... You have to make it fall!
 
Madaktari wametimiza wajibu wao, serikali iwape haki zao. Nasema jambo moja tu hapa ni kwamba for the first time hapa nchini endapo serikali itawashiti tutafanya kitu cha ziada na ni dalili njema kuelekea kwenye kuheshimiana. wenzetu Kenya hapo hawana utajiri kama tulionao sisi hapa uchumi wao mzuri ni viwanda vyao ambavyo mostly wameingia ubia na ama wamarekani au waingereza na sana sana utali sisi kila kitu Sir God katupa shida yetu hapa uongozi big zero, tutawafundisha kazi this time, Madaktari kazeni buti. hatuwezi kuendelea kuishi huku tumepiga magoti, ni bora tufe tukiwa tumesimama
 
Pendekezo:tuamsishane kuandamana pindi selikali iwapo reluctant tusisubiri vifo vingine.
 
Madaktari wasikilizwe kwa KINA na waletewe mabadiliko ya kweli kama walivyotaka na wala kusionekane USANII WALA DANGANYA TOTO wa aina yoyote ile hadi hapo. Tukifanyia mzaha madai ya madaktari na manesi watu tutakua tumekwenda na maji.
 
haya ndugu watazamaji wa kituo chetu bora cha habari,ile mechi kali kati ya serikali na madaktari karibia kipindi cha pili kinaanza. HALF TIME ndo inaisha leo,timu zote zinajitaarisha kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Naona REFA(wananchi) anakagua kiwanja,kwenye goli la serikali refa anakuta kuna vitu vimefukiwa(manesi,wauguzi,vitisho,fitna,dharau.......)
Hii ni aibu kwa timu kubwa kama serikali kutumia mbinu chafu za kushinda mechi dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu,ikichukua nafasi ya timu ya WALIMU iliyoonyesha kiwango kibovu msimu uliopita na kusababisha ishike daraja.

Mechi hii lazima mshindi apatikane safari hii,hata kwa ushindi wa penati...............................

duh... umenichekesha mkuu....
 
Back
Top Bottom