Madaktari kukutana kesho kufanya tathmini ya makubaliano na serikali, kuna harufu ya mgomo kuendelea

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
111
Heshima kwenu wanaJF,

Wakuu kama mtakumbuka wakati mwenyekiti wa jumuia ya kuratibu mgomo wa madaktari Dr.Ulimboka alivyotangaza kwenye taarifa yake ikumbukwe alisema mgomo UMEAHIRISHWA na wala HAUJASITISHWA na kutoa nafasi kwa serikali kushugulikia madai ya madaktari ambayo yalikubaliwa na serikali na yasingeweza kupatiwa ufumbuzi kwa wakati ule kwa haraka hivyo serikali iliomba wiki mbili.Kama ambavyo taarifa ile ilivyotanabaisha kuwa kikao cha kutathmini utekelezaji wa msingi wa maridhiano yaliyofikiwa kitafanyika tarehe 3/3/2012.

Taarifa za uhakika zilizonifikia mkutano wa madaktari wote utanyika kesho kama ilivyotangazwa hapo awali kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa WATERS FRONT jijini Dar es Salaam.

Pamoja na taarifa hizo madaktari wengi wanaonyesha kutokuridhishwa na utekelezaji wa madai yao kwa wakati kama ambavyo walivyoombwa na serikali kuwa ndani ya wiki mbili wangekuwa wamemaliza zoezi zima la kutanabaisha nini serikali itafanya juu ya madai hayo.Wengi wakionyeshwa kukerwa na serikali kutowafuta kazi ya uwaziri, waziri wa Afya na Naibu wake ambao mpaka sasa bado wako ofisini.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinazidi kupasha kuwa maamuzi magumu yanaweza kufikiwa kwa mgomo ambao uliahirishwa sasa unaweza kuendelea kuanzia jumatatu.

Zaidi wamekerwa na taarifa juu ya madaktari iliyotolewa jana na TBC iliyokuwa kipropaganda ili kuwagawa na kada nyingine na kuonyesha kuwa madaktari hawataki kwa makusudi kufikia maridhiano ya mwisho.

Habari zitatolewa zaidi kadri itakavyowezekana kutoka kwenye chanzo changu huko Dar es Salaam.


UPDATES

Gazeti la Mwananchi leo tarehe 03/03/2012 inapasha kuwa

Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa moja ya sababu za kuvunjika kwa kikao hicho ni madaktari kupinga hoja ya kuhusisha makundi mengine kutoka sekta ya afya kama wafamasia na wauguzi.
Lakini Rais wa chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Namala Mkopi aliliambia Mwananchi kuwa wao walikwenda katika ofisi za Waziri Mkuu kufuata majibu ya barua yao waliyoiwasilisha kabla ya mkutano, lakini hawakupewa barua ya majibu.

Alisema barua hiyo pamoja na mambo mengine ilikuwa na maswali kadhaa yanayotaka ofisi hiyo ijibu huku ikieleza namna wao wanavyotaka mkutano wa majadiliano baina yao na Serikali uwe.

"Sisi hatukwenda kukutana kwa ajili ya majadiliano na wahusika bali tulifuata majibu ya barua yetu tuliyowasilisha kwao kabla ya mkutano huo, taarifa ya kuwa sisi tulitoka kwenye mkutano kutokana na kukataa makundi mengine ni za uongo na wameamua kufanya propaganda katika hilo, lakini sisi ni watu wazima tunaelewa.

"Acha wao wafanye propaganda, sisi ni watu wazima tunajua itafika wakati tutakaa nao chini na kufanya uamuzi wenye kuzingatia masilahi yetu na ya umma," alisema Mkopi.
 
Maumivu ya kichwa huanza pole pole.

ACTION huondoa maumivu haraka.
ACTION ni dawa bora.
ACTION kutoka Ikulu ya Tanzania.
ACTION tunayoitaka ni ile ya serikali kuyashughulikia madai ya madaktari.
ACTION ya kuwaondoa Waziri na Naibu Waziri wa Afya
ACTION ya kumwondoa Katibu wa MoHSW na CMO
ACTION isipotumiwa maafa ya watanzania na madhira ya maradhi yatakuwa makubwa.

Kama serikali haitaki kutumia ACTION ili kumaliza mgogoro, madaktari hawana budi kuitumia dhidi ya serikali ili kutimiziwa madai yao.
 
Jamani Jamani,
haya mg0m0 mwema!ila juzi ba'mwanaasha kasema file lipo mezani kwake
 
Serikali imelalia masikio.
Hakika taarifa ya habari ya jana TBC1 ilikuwa inawaonyesha madaktari kama watu wenye maringo sana, na kwa mtu wa kawaida angeweza kuwachukia sana madaktari.
Na no wonder, watakaa kimya hadi madhara ya vifo yaanze tena kutokea.
Kama suala hili liko mezani kwa JK anasubiri nini kukata mzizi mwa Fitna?...anadhani kuongea kwa mbwembwe na vicheko kwenye vyombo vya habari kuna mashiko zaidi ya kuwalipa watu wanaodai stahiki zao?
Hili sio suala la katiba, ambalo anaweza kusema hataki kukurupuka, haya ni maslahi ya watu nafamilia zao ambapo yana msukumo wa uharaka.
 
Serikali imelalia masikio.
Hakika taarifa ya habari ya jana TBC1 ilikuwa inawaonyesha madaktari kama watu wenye maringo sana, na kwa mtu wa kawaida angeweza kuwachukia sana madaktari.
Na no wonder, watakaa kimya hadi madhara ya vifo yaanze tena kutokea.
Kama suala hili liko mezani kwa JK anasubiri nini kukata mzizi mwa Fitna?..
Hili sio suala la katiba, ambalo anaweza kusema hataki mkukurupuka, haya ni maslahi ya watu nafamilia zao ambapo yana msukumo wa uharaka.

pj,ataishia kusema NG0MA NZITO
 
pj,ataishia kusema NG0MA NZITO
Ujinga mtupu huu mkuu.
Mbona masherehe na maadhimisho mbalimbali ya serikali yanafanywa kwa mbwembwe sana, kwanini miaka mingine yasiadhimishwe kwa namna ya tofauti, mfano kupeleka bajeti ya maadhimisho hayo kwenye malipo kama haya ya doctors?
Ngoja wazibe masikio hivyohivyo, na watu wafe, huu utakuwa ni mtaji mkubwa sana kwa wanasiasa kwenye uchaguzi wa Arumeru na 2015!
 
Jamani Jamani,
haya mg0m0 mwema!ila juzi ba'mwanaasha kasema file lipo mezani kwake

wote wanaleta siasa za kukimbilia vyombo vya habari. Mi nawashangaa sana viongozi wa nchi hii,mgogoro unapotokea wao wanaenda kuongea na vyombo vya habari. Wanafikiri hawa waandishi wasiojua hata kufanya utafiti kwenye habari zao ndo wawe negotiators? Kwa nini hawataki kutimiza wajibu wao? Wanataka huruma ya wananchi huku wananchi wakijua madudu yanayofanywa na wao kwenye matumizi ya kodi zetu. Jana madaktari waliomba round table na waziri mku yeye akaja na makatibu na watendaji wa wizara zote. Wengine wamekuja kufanya nini? Wao ndio waziri mkuu? Baada ya wawakilishi wa doctor kutoka nje kwa kutokuwa na imani na ujumbe ule wao wakapeleka taarifa vyombo vya habari kwamba doctors wametoka nje kwa kuwabagua pharmacists,nurses,lab techs ili kujaribu kuwagawa watumishi wa afya. Hivi ukijiuliza hii serikali,au genge la majambazi wanaotumia mgongo wa wananchi?
 
Mie nishajichokea kwa kweli na nchi hii. Utendaji unasikitisha sana!

Unasikitisha na kuuwa matumaini kwa kweli.

Cha kusikitisha zaidi ni upole,uvumilivu na ukarimu wa sisi watanzania. Tupo tupo tu kama ZOMBIES.
 
kesho ngoja niende hospital nikatibu uti mapema kabla ya mgomo.
but i support your boycott
 
Back
Top Bottom