Madaktari kanda ya ziwa wafanya mkutano leo ...madai yao yakipuuzwa kugoma

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
111
Kwa taarifa zilizonifikia pamoja na taarifa ya habari ya STAR TV jioni hii chama cha madaktari kanda ya ziwa MAT LAKE ZONE leo walikuwa na mkutano kuanzia saa sita mchana ambapo baada ya mkutano huo wameungana na wenzao wa Muhimbili na nchini kote kupinga hatua ya wizara ya afya kupuuza madai yao na kuazimia kusimama kwa pamoja kutetea taaluma yao ambayo sasa imepuuzwa kiasi cha madaktari kugeuzwa waandika rufaa za mabwana wakubwa kwenda kutibiwa INDIA wakifuata sophisticated diagnostc and therapeutic machines ambazo hawanunua zihudumie watanzania wote.

Wamelalamikia upotoshwaji wa kuwaita INTERNS wanafunzi wakati nimadaktari walio-graduate na kula kiapo cha udaktari na INTERN ni muda wa kujiongezea uzoefu zaidi.Akiongea kwa hasira rafiki aliyenipa taarifa hizi amesisitiza hawatarudi nyuma.

Wameazimia kusubiri mazungumzo na waziri mkuu na muafaka usipofikiwa wataweka vifaa chini

UPDATES

Katika ukurasa wa facebook Dr.Hamis Kigwangala ameandika

Naibu Waziri, Wizara ya Afya, Dr. Lucy Nkya (MB) naye avuliwa uanachama kwa kipindi cha mwaka mmoja kama mwenzake Daktari Mkuu wa Serikali, Dr. Deo Mtasiwa, kwa kosa lile lile la kusaliti fani ya udaktari na lile la kuvunja miiko na maadili ya udaktari kama yanavyosomeka kwenye kiapo cha udaktari, kwamba kila daktari atawatambua na kuwathamini madaktari wenzake kama ndugu zako na kuwatendea wema, kuwapenda na kuwaheshimu. Chama cha Madaktari Tanzania kitawafikiria kwenye Mkutano ujao wa kawaida. Hii maana yake nini? Wamepoteza sifa ya kuwa medical 'professionals!' Wamebaki kuwa wataalam wa Udaktari tu!

Akaandika tena hivi

Hivi ni nini chanzo cha kiburi na madharau ya watendaji wa serikali? Maana hata kura hawakumwombea Rais, sasa kwa nini wanakosa heshima kwa wapiga kura wetu kiasi hiki? Viongozi wa CCM wanasubiri nini kuilazimisha Wizara itoe majibu kwa madaktari? Hivi mpaka wagome ndiyo watasikilizwa kweli? Sasa tayari Bugando, KCMC wameishashika kasi, hawa Wizara ya AFya wanatoa wapi kiburi cha kutowasikiliza askari wao? Wanataka watu wafe ndiyo waje wawasikilize?
 
Nimependa hapo pa kusema "kugeuzwa waandika rufaaa....,,wanafuata sophisticated diagnostic na therapeutic machines".. real wangekuwa na maana halisi kwa nchi wangezinunua zije hapa TZ zihudumie na wagonjwa wengine wasioweza gharamia nauli ya India. Gomeni tu wataalam,nawaunga mkono!
 
Hizo sophisticated diagnostic na therapeutic machines wakiwekewa kwenye mahospitali wanaziharibu makusudi na wengine wanaiba vifaa. Waache upupu.
 
Hizo sophisticated diagnostic na therapeutic machines wakiwekewa kwenye mahospitali wanaziharibu makusudi na wengine wanaiba vifaa. Waache upupu.

sasa wewe ndugu yangu hivi kweli mtu anaweza kuharibu kifaa cha kazi yake?kwenye kuiba lazima tujiulize kwa nini waibe....kama ndiyo kukesha usiku kucha na wagonjwa halafu night allowance ni elfu kumi kama magazeti yalivyoripoti kwa nini wasiibe
 
karata aisee jaribu kujiweka kwenye shoes za madkt then toa honest opinion pliz

na btw, vifaa vilivyomo mahospitalini ni very outdated but vinatunzwa sana cz hujui lini utapata kipya!!!

naomba tu uwe kidogo sensitive kwa ma dkt
 
Kaka Hospitali zetu za rufaa zimegeuka BIG DISPENSARIES NA MAJUMBA YA MAKUMBUSHO
 
Hizo sophisticated diagnostic na therapeutic machines wakiwekewa kwenye mahospitali wanaziharibu makusudi na wengine wanaiba vifaa. Waache upupu.

Wewe nadhani huna sifa ya kuwa mtz na huna machungu na nchi yako. Hivi kwanza unajua tunafanya kazi ktk mazingira gani mpaka utoe ushuz* wako huo? Tutagoma na tutaendelea kugoma kama tunafanya kazi kwenye mazingira hatari ya kupata Hepatitis na HIV kama ya tz, wakuu wa nchi hawaoni haya na wala hakuna cha malipo ya kufanya kazi ktk mazingira hatarishi 'risk allowance'. Kama huna cha kuchangia humu bora kawinde panzi na watoto wenzako huko nje. Aaagghh!
 
Hizo sophisticated diagnostic na therapeutic machines wakiwekewa kwenye mahospitali wanaziharibu makusudi na wengine wanaiba vifaa. Waache upupu.
sasa machine ya mtumba itaacha kuharibika?kilaza kweli wewe
 
Nasikia kuna watu Kama wawili hivi pale wizara ya Afya wamekalia haki za Madaktari zaidi ya 2,000 mpaka madaktari wengine wame opt kukimbilia inji za Botswana n south coz of kubabaishwa MoH? Just imagine watu wawili tu wanaua na kudhalilisha fani ya udaktari hivi hivi wengine wakiangalia? In a country where Doctor to patient ratio is 1: 35,000 ilihali WHO in recommend 1:4,000? One wonders ???? Mie ninashauri hawa madaktari wasipuuzwe na wasikilizwe na kupewa kipaumbele coz tunawahitaji sana
 
Back
Top Bottom