Madaktari: Hiki ndicho kilichomuua Kanumba

Yule mpiga picha anasema eti kwenye hiyo movie Kanumba kaigiza anaumwa figo hlf ana mpenzi wake ambaye anakuja kugundua baadae ana bwana mwingine, ugomvi unazuka binti anamsukuma kanumba chini kanumba anaanguka na kufariki dunia! Mh!
 
kilichomuuwa ndugu yetu ni kiharusi cha ghafla............,mtoto wa watu aachiwe akale maisha yake.................kama hajajifunza hatajifunza tena kukaa mbali na mibaba mijitu mizima......
 
aisee nashukuru kwa kupata taarifa maana nilikuwa sijajua mpaka dk hii kilichomuua mpendwa we2 sk. sasa lulu bora atolewe apumue na familia yake ifurahi ila nahisi akitoka roho yake itakuwa mali ya wengi
 
taarifa ya kitaalam kawaida hueleza CHANZO au SABABU ya mtikisiko huo. Ilivyowekwa hapa imekaa upande.

Sawasawa Mkuu,hata Mm nashangaa,maana sioni sehemu ambapo hiyo taarifa ya madaktari imetaja chanzo cha hiyo Brain Concussion,inatokea tu?!
 
Mods, naona wamejichanganya hii thread wameipeleka jukwaa la Celebrities.
Walichokosea ni kitu gani hapa? kwani wewe haujioni unavyochangia una tofauti gani na mshereheshaji? hapa Celebrity haswa ndio mahala pake. enjoy ur forum.
 
Daktari aeleza kilichomwua Kanumba

NI BAADA YA JOPO LA MADAKTARI MUHIMBILI KUMFANYIA UCHUNGUZI, BABA YAKE AZUNGUMZA, WABUNGE WAANGUA KILIO

Florence Majani na Suzzy Butondo | Mwananchi

MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”

“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”

Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.

Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.


Wana JF,

Kwa mtazamo wanguu me bado nasema hiviiiii Report hiii ni ya kidaktari tuuu na basi itabakia kuwa ni ya madaktari hao bingwa.

Ivi unapo niambia kuwa ni mtikisiko wa ubongo sawa na je ulitikiswa na kitu gani? au hii nayo ni police nao wanaitaji kuja na doctor wao kuchunguza kijiridhisha kuwa ilkuwa ni mtikisiko pia wa ubongo bila kuwepo chanzo cha mtikisiko?

wakati mwili ulipo chukuliwa kwenda Hospital au pale ulipo kutwa au? na je time of death ilisema ni muda gani japo wakadirie?

My Take;

Report ya Madoctor bingwa its more Theoretical
Report ya Police ije nayo more Practical

Sio kwamba nataka kumkandamiza mtuu hapa hili liko wazi kwa mtu makini tuuu anajua Report ni nusu ya walicho kifanya esp Doctors hao bingwa
 
concussion iliyosababisha kifo cha hapo hapo...bila jeraha kichwani...

according to J Murtagh, Principles of General practice; concussion is usually caused by significant blunt force trauma/injury to the head such as a fall, sports injury, car accident, or being hit/struck with hard object.
bado huyu mtoto wa watu ana kesi ya kujibu...


Mkuu naunga mkojo majibu yako na ndio maana bado nasema majibu ya madoctor wetu ati bingwa hao wametupa majibu mepesi sana kwa mtu wa kawaida atabaki kuishia hapo ila kwa watu wenye ufahamu zaidi ni ndipo wanatufanya tuchambue zaidi kujua wapi hawa madoctor bingwa wamtunyima kujua nini haswa kilichopelekea kifo cha kanumba

 
Madaktari wa bongo hawaaminiki. Hata tiba ya babu wa Loliondo waliibariki, kumbe ilikuwa feki!

Nafikili wewe ndiyo huaminiki hakuna daktali hata mmoja aliyebariki hyo tiba huyo babu zaidi ya viongozi wetu wa dini hasa wa kkkt na viongozi wetu wa serikali.lakini siwalaum kwakuwa suala lile lilichukuliwa kimzaha sana tunakumbuka shuka asubuhi.nakuomba usiwasingizie madaktali hata kidogo.
 
11507.jpg
Marehemu Kanumba​

NI BAADA YA JOPO LA MADAKTARI MUHIMBILI KUMFANYIA UCHUNGUZI, BABA YAKE AZUNGUMZA, WABUNGE WAMLILIA
Florence Majani na Suzzy Butondo
MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”

“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”

Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.

Baba mzazi azungumza Baba mzazi wa mwigizaji huyo, Charles Musekwa Kanumba alisema kwamba alipata taarifa za kifo cha mwanawe Jumamosi saa 10:00 alfajiri baada ya kupigiwa simu na dada wa marehemu, Sara Kanumba. “Sara aliniuliza: ‘Una taarifa yoyote kuhusu mwanao Kanumba?’ Nikamjibu kuwa sina taarifa yoyote, ndipo aliponieleza habari za kifo hicho. Aliniambia Kanumba hatupo naye tena amefariki kwa kuanguka, amekorofishana na mpenzi wake.” alisema taarifa hizo zilimsababisha aishiwe nguvu kwa kuwa kilikuwa kifo cha ghafla… “Basi kuanzia hapo, nilianza kupigiwa simu za kupewa pole, ndipo nilipoamini kumbe mwanangu amefariki.”

Akizungumzia kuchelewa kufika msibani, alisema kumetokana na tatizo la mawasiliano. Awali, alikuwa amepanga mtoto wake Kanumba akazikiwe Mwanza kwa babu yake ndiyo maana hakufika mapema msibani. “Nilikuwa nimepanga apitishwe hapa kwangu Shinyanga aagwe, halafu tumpeleke Mwanza kwa babu yake kumzika huko lakini alipokuja mama yake alinishauri kuwa huko kutakuwa na nafasi ndogo kwa sababu watu ni wengi pia alikuwa na marafiki wengi, wengine wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo alinishawishi na tukakubaliana kumzika Dar es Salaam,” alisema.

Pia alikanusha uvumi kuwa hajafika msibani kwa kuwa walikuwa na ugomvi na marehemu akisema walishamaliza tofauti zao. Alisema anatarajia kufika leo usiku tayari kushiriki mazishi hayo.

Wabunge kilio Jana, baadhi ya wabunge waliofika nyumbani kwa marehemu Kanumba waliangua vilio wakati walipotoa salamu zao za rambirambi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata hakuzungumza na badala yake aliimba kipande cha wimbo uliozungumzia kifo na maneno ya wimbo huo yalionekana kuwagusa wafiwa na kusababisha vilio kuanza upya huku baadhi wakipoteza fahamu.
Mbunge mwingine, Neema Mwinyimgaya aliongeza majonzi masibani hapo alipounganisha msiba huo na wa mama yake… “Mama yangu amefariki miezi mitatu iliyopita, huko uliko mama, nakuomba umpokee kijana mwenzetu,” alisema mbunge huyo na kushindwa kuendelea.

Wabunge wengine waliohudhuria msiba huo ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Aboud Juma (Kibaha Vijijini), Mussa Azan Zungu (Ilala), Abbas Mtemvu (Temeke), Peter Serukamba (Kigoma Mjini) na Ritha Kabati (Viti Maalumu).
Kova na mchango wa Kanumba Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema anakumbuka mchango wa Kanumba katika kuzuia uhalifu jijini.



“Tulishirikiana naye pamoja na wasanii wengine kuandaa bonanza maalumu ambalo lilidhamiria kukabiliana na uhalifu hapa jijini na kwa kweli mchakato ule ulifanikiwa kwani uhalifu ulipungua kwa kiasi kikubwa” alisema Kova.
“Kifo chake kimekuwa cha ghafla mno na nafikiri kujiweka tayari (kiimani) ni jambo ambalo kila mmoja anatakiwa kuwa makini nalo katika maisha yake,” alisema Kova.
Daktari aeleza kilichomwua Kanumba

 
heri angetafutwa mganga wa jadi apige ramli
kuliko hii ripoti ya wataalam wetu.
 
Watanzania kwa shughuli za udaku tumeshinda mana watuwanakuwa hata hawakumbuki imani zao za kiroho mkumbukeni mungu. jameni yeye ndiye aliumba na ametoa. alikuja kwa mavumbi na atarudi kuwa mavumbi huu ni wakati wakujiuliza je sisitumejiandaje kwa safari hii mungu anapomchukuwa kipenzi chako ankukumbusha kuwa nawewe safari ipo wakati wowote ikifika unakwenda haijalishi sababu ya kifo chako nini hapa tunataka kumpalawama Lulu hata kama alimsukuma hajakusudia kuuwa wewe marangapi umesukuma mwenzio kama sikwautani kwakukorofishana lakini hakunaswala la zamira ya kutoa roho. ukitizama upande mwingine hebu jaribu kufkiri jitu kama kanumba limeshiba na kitoto kama lulu kinaweza kumfanyizia kanumba mpaka akate kamba. halafu tunaongelea upande mja tu hatufaham chanzo nini saingine yeye marehem ndio sababu mana kuna madem wanamshutum kanumba kuwa alikuwa anatembezea ubabe mademzake anawapiga na kuna fununu alkuwa aikimpiga LULU na ubapa wa panga sasa kwakuwa LULU hajapata nafasi ya kuongea hazarani ndomana tunachonga sana. upande mwingine hapo ndio inasibitika vip marehem alikuwa hana hekima ukiangalia historia ya LULU kanumba ameanza kucheza filam na lulu akiwa mtoto sijui miaka mingapi lakini na uhakika hkuwa na miaka zaidi ya 7 amemlea yeye na kumkuza leo hii vipi amfanye mpenzi mtoto anaeweza kumzaa kwamtu mwenye busara hawezi kufanya hivyo hata hasa kwasisi waafrika ni tuna mila na desturi, kwahiyo tusiipelekee lawama kwa upande mmja ingekuwa wafu wanaongea kanumba angesemaukweli kwa mateso anyopata LULU kuwekwa nyuma ya nodo bila makosa na kwashutuma nzito ya mauwaji
 
Back
Top Bottom