Madaktari: Hakuna anayerudi kazini kesho!

Katika nchi hii serikali inaogopa wananchi wakawaida tu na si wafanyakazi wake maana inajua ikitia mkwara tu wengi watafyata mkia isipokuwa wachache ambapo itapata nafasi nzuri ya kuwashughulikia. Dio maana Pinda anakiburi. Wananchi walipokomaa kule mbeya tuliona serikali ikiufyata. Ilipoua januari 2001 kule Zbar na kuona wazazibari hawatishiki iliufyata na kurusu haki yao ya kuandamana,

Halafu hii serikali inayoshauliwa na mtu kama Wasira kweli inaweza kutoa wapi busara? Hebu mtazameni hata katika zile picha za Rais na ujumbe wa CHADEMA, kama vile hakupendezwa na kitendo kile. Atakuwa alitia husuda sana JK akamsusia. Serikali yetu haina washauri makini isipokuwa wale wanaongalia matumbo yao
 
ha ha ha haa! Najua mtarudi kesho, karibu wote. Tuweke dau, nchi hii watu waoga kudai haki zao. Wafanyakazi nao si ilikua hvi hvi, david kibamba na katiba je?
 
Pinda Pinda Pinda, hao unaowalazimisha wakafanye kazi sio makuli wa kubeba mizigo, hao ni wataalamu, tena taaluma yao ni nyeti sana, sasa wakirudi na kuanza kutibu isivyo itakuaje? Ukienda ukikutwa na Malaria waseme wakukate mkono. Ukiwa na pressure basi wafanya operation ya utumbo, ukiumwa kidole cha mguu, wakate masikio na kutoa macho. Unataka wakafanye hivyo???? Hawa si watu wa kuwalazimisha hata kidogo, bila muafaka hakuna kitakachoeleweka. Hembu tumia busara. Juzi tu mmeona viongozi wenzenu wanaotumia maguvu kilichowakuta huko Libya na Misri, bado tu hamjifunzi. Kwa hakika Ocampo lazima aje awafungulieni mashitaka ya hawa wagonjwa wanaokufa kwa kiburi cha Serikali.

Madaktari, hakuna kurudi kazini, wakiwafukuza kazi kesho, ndugu zenu tupo, hampo kisiwani, hamtakosa ugali na mchicha, tutakula tu huohuo, kwani tumekuwa tunakula kwa siku nyingi. Nawaomba na manesi kesho tangazeni nanyi kuweka zana chini tuone watafanya nini. Hawa wasicheze na nguvu ya Umma! Pinda umetia aibu, sijui utaficha wapi uso wako, na ukienda Bungeni wewe safari hii hurudi kama waziri mkuu tena, lazima ujiuzuru. kama mnashindwa kuongoza si muachie ngazi waje wenye uwezo?? Hao Askari mnajisumbua tu, wapelekeni hao wakatibu basi huko mahospitalini. Crazzy this Country!!
 
Sasa madaktari wadhihirisha immaturity tena. Wao wamesema hawawezi kukutana na waziri mkuu siku ya jumapili, lakini wameweza kukutana na waandishi wa habari!
Nadhani kuna madaktari wanapenda mgomo uendelee kwa sababu after all mshahara wao wanaendelea kupata na muda huu wa mgomo wanaendelea kufanya shughuli zao nyingine ikiwemo kwenda kutibia hospitali private...

Ukitoa hoja jaribu kutosahau akili nyuma,jaribu kuruhusu ubongo kutafsiri jambo,kukutana kuna maana nyingi na malengo tofauti,kwa pinda walikuwa wakutane kwa mkutano ambao unaweza kuchukua masaa mengi na hapo ni pande 2,na ulikuwa unahitaji watu wengi kuudhuria,kwa madaktari wametoa kauli/taarifa kitu ambacho kinaweza kutumia hata dk 2 na kutolewa na mtu mmoja au wachache kama ulivyoona,suala la jumapili unaliingizaje hapa.
 
ila ukiangalia vzr huu mgomo n kama una siasa ndn yake!km kwa wabunge karidhia posho n.k kwa nn c kwa wengine!?doctorz wana2fundisha kwamba ugumu w maisha n kwa kila m2 na lengo lao kuu ni kuondoa matabaka kwa waTz!km mshahar w ticha haufik hta robo ya posho yko Mbunge,wao waishi vp?
 
Manjua Hii mechi ni nzuri sana ee? Refa ajiamini tuu, Nitaifuatilia sana maana ipo interesting sana
 
Sitaki kuamini kwamba serikali imefikia mwisho wa hekima zake.
Watanzania wengi wanaumia kwa sababu ya huu mgomo, lakini badala ya kutafuta hata suluhu ya dharura, wamekalia kutunisha misuli dhidi ya afya za mafukara wa Tanzania??

How unwise!
 
Sitaki kuamini kwamba serikali imefikia mwisho wa hekima zake.
Watanzania wengi wanaumia kwa sababu ya huu mgomo, lakini badala ya kutafuta hata suluhu ya dharura, wamekalia kutunisha misuli dhidi ya afya za mafukara wa Tanzania??

How unwise!
hata wewe?
 
Personal attack ya pinda kwa dr. ulimboka!
Kwamba sio mtumishi wa serikali.....
 
jamani chonde chonde msirudi nyuma.
madaktari hawana vyeti feki hadi waogope kufukuzwa.
wasiwatishe kisa kusomeshwa na serikali, kwani wengine wamejisomesha wenyewe.
wamechoka kuona vifo vya watoto vikitokea si kwa sababu hawawezi kuwatibu bali hamna ventilator za watoto.
wamechoka kuona vifo vya kinamama sio kwa sababu hawawezi kuwaokoa bali maji ya uchungu yameisha.
wamechoka kupeleka watu nje si kwa sababu hawawezi kuwatibu bali hamna CT scan, MRA , hemodialysis machines.
wamechoka kudharauliwa kama loosers na wenzao wa proffesional zingine.

Intern ndio kizazi cha wale ambao hawakuchaguliwa na serikali kusomea udaktari, walichagua wenyewe. Hawakusoma sekondari zenye kula kuku, maharage mabovu tu ndiyo ilikuwa mboga yao. Wamesoma kwa mkopo, au kwa mkataba. Hawajui uzuri wa serikali hata kidogo. Wakirudishwa nyuma leo na wakongwe kabla ya 2015, tayari intake 4 watakuwa sokoni tena. Sasa hapo, kama bado hii serikali ipo ijiandae kwa matukio kama hayo kila mwaka.

Inawezekana mbona hadi wafagiaji wa reli S. Africa waliweza, sembuse nyie.
 
pinda anasema eti transport allowance kwa mtu anayeanza kazi haiwezekani...wakati kimei wa CRDB anampa kila mtumishi wake hata anayeanza kazi leo fungu la fuel allowance...govt acha kichaa!
 
Steve Dii,

Hebu jiulize, mnajaribu suluhu, jamaa wanasmea kama hamtaki acheni tuta-import from Cuba,

Kwani mkuu hao madaktari kutoka Cuba hawataki pesa? na sio rahisi kukupa lundo la madaktari,sana sana kama kungekuwa kuna madaktari wa kutosha JW serikali ingeweza ikakooa.Mazungumzo ni muhimu kufikia muafaka,ubabe wa serikali hausaidii ni kuongeza matatizo.
 
Personal attack ya pinda kwa dr. ulimboka!
Kwamba sio mtumishi wa serikali.....

pinda anataka kusema yeye na ulimboka,yeye anajua sana ngazi za udaktari,hajui kuwa mtu anaweza kutoka fom4 asisome form6 akaenda chuo cheti alaf digrii...anakaa kuoji mbona mtu flani akupita sehemu flani...
 
pinda anataka kusema yeye na ulimboka,yeye anajua sana ngazi za udaktari,hajui kuwa mtu anaweza kutoka fom4 asisome form6 akaenda chuo cheti alaf digrii...anakaa kuoji mbona mtu flani akupita sehemu flani...

Kimsingi anadai hakuna tatizo, isipokua ulimboka anatengeneza matatizo......
 
[/QUOTE]

mkuu nakumbuka PINDA aliwah sema maisha yapo juu wabunge hawabaki na chochote mwisho wa mwezi na zigo la posho kaachiwa yeye aamue mins imepita,cha kustaajabisha haoni huo ugumu kwa docs kweli mweshe shibe hamjui...doc never lose hope mpaka kieleweke
 
Kimsingi anadai hakuna tatizo, isipokua ulimboka anatengeneza matatizo......
You can imagine jamani!!

Na watamtoa kafara walivyo wababe. Wananikumbushia migomo ya chuoni. Na wakishampiga mchungaji wa kondoo, na kondoo wa kundi lake watatawanyika!
 
Back
Top Bottom