Madaktari Dodoma wapo bar

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
Nipo hapa mkoani dodoma , nimetembelea muda huu bar maarufu ya carribean jirani na ofisi ya bunge nimekuta madaktari wengi sana wakiondoa stress kwa kupata vinywaji source ni phd mwenyewe nimeungana nao na heniken yangu ya baridi
 
vigumu kukuamini inawezekana heineken zimeshaanza kukulevya..ongeza kiroba bili kwangu.
 
Safi sana madaktari wananchi tupo na nyie katika kutetea haki na utu wao pamoja na wananchi kwa serikali legelege na dhaifu ya CCM kuboresha hospital na vifaa na madawa kwa ajiri ya wananchi wanaoteseka kwenye nchi yao.
 
CAREBEAN panauzwa KITIMOTO!!!! Na madaktari waislamu wapo au umeona wawili wakipata lunch umejumuisha wote???
 
Lazima mchochee mgomo maana hata nyie mnatibiwa HOSPITALI binafsi mkiteleza bafuni!!!
 
Nipo hapa mkoani dodoma , nimetembelea muda huu bar maarufu ya carribean jirani na ofisi ya bunge nimekuta madaktari wengi sana wakiondoa stress kwa kupata vinywaji source ni phd mwenyewe nimeungana nao na heniken yangu ya baridi

Mkuu mbona nami nipo maeneo hayo lakini sioni madaktari hapo? Nielekeze meza mliyokaa
 
Maswali ya kujiuliza juu ya mgomo huu wa madaktari walio mafunzoni na wale mabingwa ni:

1. Nani anayepata adha kati ya hawa?
(a) Ni sisi wananchi kwa kukosa huduma
(b) Ni serikali kwa kuchukiwa na wananchi wanaokosa huduma

2. Ni kweli kuwa sharti la kwanza la kuacha mgomo la kujiuzulu mawaziri wa afya linalinganya kwa asilimia kwa uzito na wananchi wanyonge na maskini kutaabika usiku na mchana?

3. Je, serikali kupitia kauli ya Mh. Pinda jana ipo katika wakati mwafaka wa kusubiri hadi hali ngumu itokee kwa wagonjwa ili ichukue hatua stahili?

Hebu tujiulize waungwana juu ya majibu ya maswali haya.......
 
Si jambo la kufurahia madaktari kugoma maana wanaoteseka ni maskini lakini kama ndio njia pekee mimi naona sawa kwa muda mfupi ili serekali itekeleze wajibu wake na iache kufanya kazi kwa mazoea. Halafu hii inadhihirisha serekali haina plan B kwenye hali kama hizi, wao wanajua wanaodai haki zao wataandamana ili walete askari wanaofanya kazi kama marobot wawatawanye kwa maji ya kuwasha. Kumbe wanadeal na kizazi cha digital wakati serekali bado ni analogue. Watu wanagoma tu sasa hv. Lazimisheni tena tuone. Serekali ya CCM watu hawawataki maana hamna mbinu mpya mmebakia kuamini ushirikina, majungu, fitina na umbea. Hii chini ni ya watanzania na ndio wenye maamuzi na wala sio viongozi. Wakati wananchi wanaamini sisi sio maskini viongozi wetu wanaolazimisha kuingia madarakani kwa kutumia rushwa na dola wanaona nchi ni maskini sana na ili uwe tajiri lazima uwe kiongozi ambaye utaiba mali ya uma.
 
Mkuu mbona nami nipo maeneo hayo lakini sioni madaktari hapo? Nielekeze meza mliyokaa

Nani asiyejua kuwa umetumwa kuchunguza? Mkuu PHD usijaribu kumkaribisha huyu jamaa,ni gamba linaloanza kujitokeza kama pembe vile.
 
Nani asiyejua kuwa umetumwa kuchunguza? Mkuu PHD usijaribu kumkaribisha huyu jamaa,ni gamba linaloanza kujitokeza kama pembe vile.
Mkuu kuna cha kuchunguza kweli hapo? Naona siku hizi kila nikipiga kona unanishambulia tu. Kumbuka kwamba si kila mtu atakuwa akikipigia makofi chama unachokipenda! Mimi najiongoza Mkuu sina chama nina mawazo huru. Vyama niliachana navyo zamaaaani enzi hizo CDM ikiwa mtaa wa Kisutu karibu na Kisutu Girls Secondary School, NCCR ikiwa na makao yake makuu mtaa wa Agrey na CCM ikiwa pale Lumumba, NRA ikiwa maeneo ya kariakoo na UMD wakiwa MAgomeni. Hivi kwa sasa makao makuu ya CDM yako wapi mkuu?
 
Nipo hapa mkoani dodoma , nimetembelea muda huu bar maarufu ya carribean jirani na ofisi ya bunge nimekuta madaktari wengi sana wakiondoa stress kwa kupata vinywaji source ni phd mwenyewe nimeungana nao na heniken yangu ya baridi

.
Fanya fujo uone wataizingira hiyo bar sasa hivi.
.
 
Mkuu mbona nami nipo maeneo hayo lakini sioni madaktari hapo? Nielekeze meza mliyokaa
Mkuu location yako mara nyingi huwa inakwenda na matukio....hasa pale unapokanusha jambo.....Tusishangae kwenye thread nyingine ukaja ukadai upo Muhimbili...
 
Nipo mida hii Dom..hebu nielekeze umekaa sehemu gani tuje tuchape mtindi...nimefika maeneo ya CBE
 
Nipo hapa mkoani dodoma , nimetembelea muda huu bar maarufu ya carribean jirani na ofisi ya bunge nimekuta madaktari wengi sana wakiondoa stress kwa kupata vinywaji source ni phd mwenyewe nimeungana nao na heniken yangu ya baridi

Hata madaktari wafanyeje Dr Haji Mponda na Nkya hawataachia ngazi. Kikwete yupo Tayari ikiwezekana watu wafe lakini siyo kuwatoa kafara maswahiba wake:bange::bange::bange:.
 
Mkuu mbona nami nipo maeneo hayo lakini sioni madaktari hapo? Nielekeze meza mliyokaa

njoo karibu na kaunta kwa huyu mama mchaga hapa nipo na madaktari wanne utatuona mkuu
 
Back
Top Bottom