Madaktari bingwa Muhimbili Watangaza mgomo rasmi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Edwini Chitage katibu wa jumuiya madaktari.


Madaktari bigwa wagoma rasmi wamesema hawawezi kufanya kazi peke yao na wako tayari kwa lolote na wamesema liwalo na liwe. Hatuwezi kufanya kazi katika mazingira haya hatarishi na magumu

Wamedai Rais kapotosha umma na wamehoji iweje rais asikilize hoja za upande mmoja?

Kwa habari zilizopo wagonjwa hakuna na waliopo wodini wametelekezwa


KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA
02.07.2012

PRESS RELEASE


TAARIFA YA JUMUIYA YA MADAKTARI KUHUSU MAAMUZI YA SERIKALI KUFUATIA HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YAWA TANZANIA TAREHE 1 JULAI 2012 JUU YA MGOGORO KATI YA SERIKALI NA MADAKTARI

Utangulizi

Jumuiya ya madaktari imepokea kwa masikitiko hotuba ya Serikali kuipitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaina

Ifahamike kuwa mgogoro huu umedumu kwa takribani miezi saba bila kupatikana kwa suluhu ya dhati baina ya pande mbili.

Kutokana na Hotuba iliyotolewa na Mhe Rais ya tarehe 01.07.2012 kwa wananchi wa Tanzania kupitia vyombo vya habari, Kamati ya Jumuiya ya Madaktari inapenda kutoa ufafanuzi katika mambo yafuatayo;

Ni wazi ikafahamika kuwa mjadala juu ya hoja/madai ya Madaktari kwa mara kadhaa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekuwa ukizuiwa na Mhe. Spika wa Bunge kwa kigezo kuwa suala hilo liko mahakamani, je ni sahihi Serikali kutoa maamuzi juu ya suala hilo?

Pia, kuhusu suala la kutekwa, kupigwa na kuumizwa kikatili kwa Dr. Ulimboka Stephen, Serikali kupitia Jeshi la polisi lilitangaza kuwa Tume imeundwa ili kuchunguza suala hilo mpaka sasa hakuna mwenye uwezo wa kuthibitisha kuwa Serikali haijahusika moja kwa moja, je ni sahihi kwa Mhe. Rais kutamka waziwazi kuwa Serikali haihusiki kwa namna yoyote ile hata kabla ya tume kutoa ripoti yake ya uchunguzi? Hii itatoa uhuru kwa tume ambayo kimsingi imeundwa na Serikali?

Nini dhamira ya Madaktari katika kusuluhisha Mgogoro huu

Kwa kuamini kuwa Madaktari ni upande muhimu katika kufikia suluhu ya dhati, tulishiriki katika meza ya ya Majadiliano kwa takribani miezi mitatu na jumla ya vikao sita vilifanyika, katika vikao hivyo takribani vikao vine kati ya vikao sita (asilimia 66% ya vikao na muda wa vikao) tulijadiliana juu ya Uboreshaji wa huduma ya afya kwa Watanzania, ni masikitiko yetu kuwa Ripoti ya Ufafanuzi juu ya Hoja/Madai ya Madaktari ya tar 31 Juni 2012, Taarifa ya Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Taarifa ya Waziri Mkuu ndani ya Bunge na hata hotuba ya Rais haikuzungumzia chochote ni kwa jinsi gani serikali itaboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Pia tulijadiliana kuhusu Uboereshaji wa Mazingira ya Kazi, ambapo tuliishauri Serikali kupitia kamati ya Majadiliano kuwa ni muhimu kurejesha motisha kwa watumishi wa sekta ya afya kwa kurudisha posho mbalimbali ambazo ziliondolewa.

Kuhusu suala la mshahara, tulishauri serikali iwe wazi kuhusu uwezo wake wa kulipa mishahara, cha kushangaza ni kwamba Serikali imekuwa ikitoa taarifa tofauti juuya ongezeko hilo mfano: Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii amelihutubia Bunge kuwa ongezekoni 15%, Hotuba ya Mhe. Rais ametoa ongezeko la 20%. Ripoti yaWataalamu iliyotokana na Kamati ya Waziri Mkuu ilitoa pendekezo la 25%. Je, nia ya Serikali iko wapi? Wakati viongozi wa Serikali wakitoa taarifa zinazotofautiana, Ripoti ya Ufafanuzi wa madai/hoja ya Madaktari iliyotoka na Majadiliano sisi tukiwa wajumbe haikutoa pendekezo (ofa) yoyote juu ya ongezeko la mshahara.

HITIMISHO

Kwakuwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya ndugu zetu Watanzania wazalendo wengi wamepoteza maisha kutokana na ukosefu wa vifaa tiba na madawa.

Na kwakuwa tumefanya kazi kwa miaka mingi sana tukishuhudia haya tunadhani muda umefika wa kubadilisha hali hii na kuwasaidia ndugu zetu Watanzania.

Na kwakuwa Serikali imeshindwa kuweka mazingira ya kazi kuwa bora na kuwezesha huduma bora kwa wananchi na watoa huduma.

Hivyo basi, Madaktari Bingwa tumeamua kuacha kufanya kazi ambayo haiendani na kiapo cha Madaktari mpaka hapo Serikali itakapokubali kurejesha interns wote na kufungua meza ya Majadiliano yenye nia ya dhati ya kumaliza mgogoro.

Na Wawakilishi
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari
Imesainiwa na
Katibu Jumuiya ya Madaktari.
 
Breaking news ITV

Ni kwa sababu

1. wameelemewa na mzigo na pia hawawezi kufanya kazi bila madaktari registra na interns
2. hotuba ya Rais iliyopotosha ukweli wa majadiliano na hali halisi ya utoaji huduma
3. Rais kuonekana kutokujua hali halisi ya utoaji huduma za afya tanzania
 
Katibu Dr Chitage..................waliobaki kazini wanaendelea na mgomo mbali ya madaktari bingwa kutangaza mgomo
 
Edwini Chitage katibu wa jumuiya madaktari.


Madaktari bigwa wagoma rasmi wamesema hawawezi kufanya kazi peke yao na wako tayari kwa lolote na wamesema liwalo na liwe.

Wamedai Rais kapotosha umma na wamehoji iweje rais asikilize hoja za upande mmoja?
Wanachonifurahisha hapa ni "sababu ya kugoma" Wengine " wakati ma dr wakawaida wanadai maslai bora specialist wao aaah "hatuwezi kufanya kazi peke yetu" kwa hiyo wakiletewa watu watanya sio
 
Nimeipenda hii movie, nafikiri sasa LIWALO NA LIWE, "DHAIFU" amechokoza nyuki kwenye mzinga, yeye anafikiri madaktari bingwa walifurahi jinsi serikali yao ilivyomdharirisha dokta ULIMBOKA!
 
Back
Top Bottom