Madai ya Wenyeviti wa CCM Vs Kubenea

Selous

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
1,325
144
Na Salim Said - Mwananchi

JOPO la wenyeviti nane wa mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameibuka na kusema kuwa wanaenda mahakamani kumshitaki mhariri mtendaji wa gazeti la MwanaHalisi, Saed Kubenea kwa madai kuwa gazeti lake liliandika habari ya kuchonganisha.

Wenyeviti hao, John Guninita wa mkoa Dar es Salaam, Clement Mabina (Mwanza), Khamis Mgeja (Shinyanga), Deo Sanga (Iringa) , Onesmo Kangole (Arusha), Hypolitus Matete (Rukwa), Nawab Muila (Mbeya) na William Kusila (Dodoma), wamechukua hatua hiyo siku chache baada ya serikali kulifungia gazeti hilo kwa miezi mitatu.

Serikali iliamua kufungia gazeti la MwanaHalisi baada ya kuandika habari iliyoelezea harakati zinazoandaliwa za kumuondoa mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kwenye mchakato wa kuwania urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, akiitaja mikoa hiyo kuwemo kwenye mipango hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wenzake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye jengo la CCM la mkoa jana, Guninita alisema habari hiyo imewasikitisha sana na wanaenda mahakamani kumfungulia kesi mwandishi na kudai fidia.

“Kwa kuwa Kubenea hakututendea haki kwa kutuingiza katika tuhuma nzito ambazo sio za kweli, sisi viongozi nane kama alivyotutaja kwa majina tumeamua kumfikisha mahakamani,” alisema Guninita.

Alisema tayari wameshazungumza na mawakili wao ambao hakuwataja na kwamba muda wowote kuanzia leo Kubenea ataitwa mahakamani.

Alifafanua kuwa kutokana na tafsiri yao kuhusu habari hiyo, wameona kuwa Kubenea anataka kuwagombanisha na mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete kuwa wana mpango wa kumng'oa.

Alisema kwamba Kubenea amewapaka matope na kuwafanya wasiaminike kwa viongozi wenzao pamoja na wanachama wenzao wa CCM.

Guninita alieleza kuwa habari iliyochapishwa katika gazeti la Mwanahalisi toleo namba 118 la Oktoba 14 yenye kichwa cha habari ‘Njama za kumng’oa Kikwete zafichuka’ iliyoandikwa na Kubenea ilikiuka maadili ya uandishi.

Alisema lengo la kwenda mahakamani ni kumtaka Kubenea athibitishe ukweli mbele ya sheria juu ya uzushi, uchochezi, na uongo wake mbele ya wananchi ili waweze kuona dhahiri uongo wa madai yake.

“Pia tutadai fidia, kuhusu kiwango... hilo ni suala kisheria na baada ya kushauriana na mawakili wetu tutajua ni kiasi gani tutadai,” alisema Guninita.

Guninita alikanusha vikali kwa niaba ya viongozi wenzake, kuhusika na taarifa hiyo na kuiita kuwa ni ya kizushi, uchochezi na uongo mtupu.

“Kubenea ameandika habari hizo kwa maslahi yake binafsi na sisi hatuhusiki na taarifa hizo za uongo. Bado ni viongozi watiifu kwa mwenyekiti wetu pamoja na chama chetu kwa ujumla,” alilalamika Guninita.

Akiongea na Mwananchi, Kubenea alisema njia iko wazi kwa wenyeviti hao kama wanataka kwenda mahakamani na kuongeza kuwa hawatapata kitu.

Alisema hizo ni katika harakati za kujikosha kwa mwenyekiti wa taifa wa CCM na kwamba yeye hana wasiwasi wowote juu ya vitisho vyao.

“Kama wanaenda na waende lakini watashindwa tu, huko ni katika kujikosha na mimi sina wasiwasi,” alisema Kubenea.

Tayari vyombo vya habari vimeshapinga hatua hiyo ya serikali ya kulifungia gazeti la MwanaHalisi vikisema kuwa serikali ilitumia sheria za kikoloni ambazo jumuiya ya wanahabari imekuwa ikizipinga kwa kuwa zinaendeleza ukandamizwaji wa haki ya kutoa habari.

Jumuiya hiyo ya wanahabari ilitaka serikali ilitumie itumie mahakama katika kutaka kuliadhibu au Baraza la Habari, ambalo limekuwa likilinda maadili na uhuru wa vyombo vya habari.


Hivi Guninita usipoenda tukufanye nini? Ole wako usiende....
 
huyu guninita si yule alikuwa ccm, then chadema tena ccm? mahakama ndo mtoa haki kikatiba karibu kwenye ulingo bwana guniata, hata hivyo uwe tayari kujibu maswali mengi ndani ya kiapo, kuhusu uhusiano wako na mafisadi, ushirikiano wako na akina mulla ambao kule mbeya wanajulikna kama majangili wa mali asili za nchi yetu. ukimaliza kujibu hayo maswali watanzania watapenda pia kujua ulivyoshiriki kifiadi kuua ule maradi wa mabasi wa wanafunzi jijini dsm wakati huo ukiwa ndo sijui mshika dau kwenye uvccm
 
Sawa Guninita tumekusikia baba.Sijui wakati huu ukitoka CCM utahamia chama gani,manake wewe umekaa kama sakayonso
 
Baada ya Wenyeviti wa CCM kutoa taarifa kutishia kulishitaki gazeti la MwanaHalisi na Mhariri wake, Saed Kubenea,

Tanzania Daima - CCM kumshitaki Kubenea

Gazeti hilo limetoa taarifa ifuatayo, ikiwa ni siku moja kabla ya Waandishi wa habari kufanya maandamano kupinga kufungiwa kwa gazeti hilo.

Taarifa kwa vyombo vya habari

KUH: MPANGO KUSHITAKI MwanaHALISI

TUMESOMA na kusikia katika vyombo vya habari kauli za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita kwamba yeye na wenyeviti wenzake saba wana mpango wa kushitaki gazeti la MwanaHALISI kufuatia habari iliyochapishwa katika Toleo Na. 118 la 8 â€" 14 Oktoba 2008.

Viongozi wanaotaka kwenda mahakamani, wakiongozwa na Guninita, wana haki ya kufanya hivyo ili kujiumba au kujiumbua mbele ya chombo kinachoaminika â€" mahakama â€" pale saa ya kesi itakapowadia.

Kinachosikitisha ni kwamba hata kabla hawajaenda mahakamani, tayari wanatishia na kutoa hukumu kwamba watalipwa fidia na kuwa watamfunga mkurugenzi au mhariri wa MwanaHALISI. Hivi ni vitisho ambavyo vimekuwa sehemu ya utamaduni wa baadhi ya viongozi wengi nchini.

Uongozi wa Hali Halisi Publishers Ltd (HHP), wachapishaji wa MwanaHALISI, hauogopi vitisho bali unaamini kuwa katika nchi hii hakuna mwenye hodhi ya sheria wala haki. Kwa msingi huo, tunasubiri wahusika mbele ya sheria.

Hata hivyo uongozi wa MwanaHALISI unaendelea kusisitiza kuwa kile kilichoandikwa ni kweli na sahihi na utaendelea kusimamia ukweli huo.



Saed Kubenea
Mkurugenzi Mtendaji

Taarifa
 
Last edited:
hakuna anayeza kuzui haki hata siku moja . kwenye ukweli haki utawala daima.
propaganda CCM hazijaanza leo wala jana tumezizoea .
Mwana Halisi keep it.
don`t fear those who destroy body .fear who can destroy body and soul.
 
Wameshindwa ile mbaya Tarime sasa they are creating another Tarime .Hizi ni dalili tosha za dola dhaifu kuanguka vibaya .Wacha tungoje tuone .Wako wengi walisema wanaenda huko Mahakamani hadi sasa hawajafika akiwemo Masha na kundi lake .Sasa Guninita .Haya yetu macho
 
Hivi huko mahakamani mbona hawaendi na kucha wanatangaza wana mpango huo? Hivi kuna sababu ya wao kutoa kauli kuwa wataenda mahakamani badala ya kuamua tu kwenda mahakamani?
 
Guninita hana jipya akae atulie ameona JK ameshajua nini anafanya....anatapatapa
 
washazoea kuonekana kwenye tv na wasomwe magazetini vitendo
loh!!!!!1

lowassa mahakama no

mgonja mahakamani no

msabaha mahakamani no

miakamba mahakamani no

vifisadi vidogo vidogo

heeeeeeeeeeee gunnita nae loh!!!!!!!!!!!! we baba uchoki na aibu za duinia hii!!!!

m nafikiri hata kuendelea na hii mada haina maana wakati toka lini majambazi yakajipeleka mahakamani!!!mlifikiri mkono mjinga kukaa kimya??????????????


.......

.........
 
Mahakama ni sehemu ya haki.
Kubenea alisema aliyosema akijua kuna mahakama.
Kubenea anajua hatari ya kwenda mahakani na ndiyo sababu yule mjinga Mkuchika hakuthubutu, badala yake katumia mabavu.
Ole wake Guninita asipokuwa makini atakimbia na huo uenyekiti wake wa sisiemu.
Haya. Shauri yake. Ngoja ninyamaze maana kesho atatishia tena gazetini kumshitaki mchukia mafisadi kwamba alisema kuwa atamshitaki Kubenea. Mwene, mimi sina ubavu huo wa kwenda mahakamani au kumwagiwa na tindikali.
Kwa heri.
 
Mzee mwenzangu Kubenea, ...chukua zangu tano.

Mtu mzima hatishiwi nyau!! Kama wanataka kwenda wambie wakaishi huko huko mahakamani hadi kesi iishe. Tumechoka na vijimaneno vyao visivyo na mshiko,... kama jibwa kuuubwa linalobweka bweka hovyo lakini halina meno. Waambie tena, "neeendeeeni hata usiku wa manane", tuone kama wathubutu kukanyaga huko!
 
Kikubwa ninaiomba mahakama ifanye kazi kama chombo huru kabisa cha kutetea haki. Kitakuwa kitendo cha aibu sana na kudhalilisha mahakama iwapo mahakama itakubali kutumimiwa na mafisadi hawa wa CCM ili kuisupress haki ya mtanzania, ya habari na kujieleza, ili tu kuwaridhisha mashetani ( mafisadi) wachache akina Guninita na wenzake wanaomtuma.

Huyu Guninita atakuwa anatumiwa na akina Lowassa, na wenzake ili kunyamazisha sauti thabiti na kweli ya MwanaHalisi.

Kwa ufisadi huu wa nchi yetu hata kama Kubenea na watanzania wote tutanyamazishwa kwa vitisho vya mafisadi hakika hata miti na mawe vitasema maana huu ufisadi uko kila kona.

Aluta continua Kubenea
 
Hivi huko mahakamani mbona hawaendi na kucha wanatangaza wana mpango huo? Hivi kuna sababu ya wao kutoa kauli kuwa wataenda mahakamani badala ya kuamua tu kwenda mahakamani?


Mkjj,Hao ni kawaida yao kutisha wakitaka kugain public confidence.Ni maneno ya mfa maji haachi kutapatapa.Aibu imewakaa mpaka shingoni.
 
Hata hivyo uongozi wa MwanaHALISI unaendelea kusisitiza kuwa kile kilichoandikwa ni kweli na sahihi na utaendelea kusimamia ukweli huo.

Saed Kubenea
Mkurugenzi Mtendaji

Kubenea for president!,

wakienda huko tuna ushahidi mwingi wa kukusaidia dhidi ya hao mafisadi, wasidhani uko peke yako, I promise you ndugu yangu mbingu zitashuka chini wakithubutu kwenda huko, watu wazima huwa hawatishianii nyau!
 
Namshukuru sana Guninita na wenzake na nawahimiza waende mahakamani haraka kwa sababu naamini kupitia kesi hiyo tutajua mengi, hata yale ambayo Mwanahalisi waliamua kutoyaandika. Bravo Guninita, suiishie njiani please
 
Maskini Gegeduka akisikia joto la maji basi hujivua gamba akifikiri atapata nafuu ya joto na kumbe ndio anaiva kuwa kitafunio
 
Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Deo Sanga, Clement Mabina, Khamis Mgeja, John Guninita, Onesmo Ngole, William Kusila na Hypolitus Matete, wamewaita waandishi wa habari na kudai kwamba wamepelaka barua kwa MwanaHalisi wakitaka kuombwa radhi vinginevyo wataenda mahakamani.

Hata hivyo, Saed Kubenea, hadi saa 7.58 mchana huu hajapokea hiyo barua ambayo waandishi wameambiwa imepelekwa toka juzi.

Kimsingi wanataka waombwe radhi na MwanaHAlisi, gazeti ambalo halipo mtaani, ni amri ambayo hakuna JAji atakeyeitoa maana ni sawa na kumwambia Jaji atoe hukumu ya kumtaka mtu ajirushe toka gorofa ya 20 au ajirushe baharini
 

Attachments

  • Kubenea.pdf
    135 KB · Views: 128
Last edited:
Back
Top Bottom