Lambardi
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 16,497
- 17,372
wadau mimi nimejaribu ku-google madai kuwa prof alikuwa akishauri mambo ya uchumi kwa kutumwa na UN sioni kitu
nimepata haya
Prof.Ibrahim Lipumba/UN - Google Search
hivi siyo danganya toto na kutafuta umaarufu kwa kisiasa.
ebu wenye japo link,inayoonesha hivyo atuwekee ili tuamini,maana wengine ni THOMASO
nitashukuru
Safari yake nchini Marekani
Akizungumzia safari yake ya Washington nchini Marekani, ambayo alikaa huko kwa takriban miezi mitano, alikokwenda kwa ajili ya kufanya utafiti kuhusu demokrasia na maendeleo, utafiti ambao ulilenga kuleta demokrasia itakayoleta maendeleo na ajira katika nchi za Afrika, alisema katika utafiti alipata nafasi ya kutoa mjadala kuhusu miaka 50 ya Uhuru Tanzania na hatua ya maendeleo ambayo nchi imeifikia.
Kwa mujibu wa profesa huyo, miaka 200 ndiyo miaka ya maendeleo ya kisiasa, lakini cha kushangaza sasa hivi nchi iko katika robo ya miaka hiyo 200 ya maendeleo lakini asilimia 70 ya wananchi wake wanatumia chini ya dola moja huku mkazi wa Dar es Salaam ambaye anahesabiwa ndiye tajiri ana uwezo wa kupata sh 650 kwa siku.
Alisema suala la kuendelea uchumi na demokrasia linaenda pamoja hii ikiwa ni pamoja na wananchi kupata fursa ya kuikosoa serikali, kuchagua viongozi wanaowataka na kuwawajibisha.
Mapendekezo yaliyofikiwa katika utafiti huo wa uchumi duniani, Profesa Lipumba alisema aliona kuna haja ya kuwa na asasi muhimu zitakazowezesha uhuru wa wananchi kujieleza na kuikosoa serikali.
Pia mapendekezo mengine ni kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi na asasi huru ya kupambana na rushwa kwa kuwa Takukuru haina uwezo ikizingatiwa kwamba haiwezi kumpeleka mtuhumiwa wa rushwa mahakamani mpaka Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai atie saini jambo linalorudisha nyuma juhudi za kupambana na rushwa.
Vilevile utafiti huo ulitaka kuwepo kwa asasi huru ya kukusanya fedha itakayofanya kazi kwa uwezo na uwazi zaidi na kuwa na matumizi mazuri ya fedha zitakazopatikana katika makusanyo hayo.
Katika hili wananchi wa Tanzania wanaweza kufunguliwa kila mmoja akaunti yake bila kujali ni mtoto au mkubwa ambapo rasilimali zote kama gesi, mafuta na madini kiasi cha mapato yake kinagawiwa kwa kuweka katika kila akaunti ya mwananchi na makato ya kodi yanatolewa humohumo hali itakayofanya kila Mtanzania kufaidika na rasilimali zilizopo badala ya sasa hivi rasilimali hizo kufaidiwa na wachache.