Madai ya mgomo Chuo kikuu Dar hayana upeo mkubwa

Gharama za maisha zimepanda jamani...Wakati hii posho inaongezwa (2007/08 nadhani) ilikuwa inatosha kabisa lakini kwa jinsi hali ilivyo sasa naona inatosha kula tu...photocopying? vocha (hata jero tu)? sabuni? rangi ya viatu? dawa ya meno? intaneti? dharura?.....
 
Funguka akili yako tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato uwapo likizo.
Ulimwengu mzima hakuna anayeweza kujitosheleza kwa kutegemea msaada tu ila mwenyewe ufunguke akili namna gani uongeze ziada
 
sijui huwa mnatumwa kuitetea serikali? chukulia mwanafunzi anakaa hostel haruhusiwi kupika. chukua hiyo elfu 5 mpangie budget. hizo kazi za part time zipo wapi? graduates hawana kazi sembuse wanafunzi? fikiria plz
 
Nimegundua hii nchi haiendelei sababu ya wapumbavu wachache. Unakurupuka tu kutoa tuhuma bila kufanya uchunguzi wa Kina. Udsm wako sawa, 5000 hela gani kwa sasa. Ngoja nikupe bajeti yangu uone. Mimi niko St Joseph College, ada ni milioni 2 na laki 7, napata 80% ya mkopo (piga hesabu 20% bei gani), chakula asb, mchana na jioni sh 3000, kodi ya chumba(cha kawaida sana) elfu 80 kwa mwezi(umeme na maji juu yangu). Bado nalipa elfu 70 za mitihani kila semister, hapo sijaweka gharama za internet(chuo hakina huduma hiyo/ hata kama kinayo hostel ndo kila kitu), vocha, nauli etc. Unadhani 5000 inatosha? Tena kila likizo niende mwanza na kurudi(elfu 5 ni hesabu ya siku unazosoma darasani pekee). Watu wana hali ngumu, mabinti wanajiuza huku, watu wanadhaliliika acheni ushabiki wa kijinga. Kushnda njaa na kua omba omba tushazoea. Kufukuzwa hostel tushazoea. Ndio maana vijana wa vyuo wanakichukia chama tawala, kimewasahau na kuwaletea propaganda kama sa hvi wanalaumiwa bodi ya mikopo, wakati serikali ndio hawana kitu. Udsm ni wapganaji wa kweli, wanataka ukombozi wa wote, hata sie tulio magerezani(hapa ukigoma tu huna chuo) wanatufikishia kilio chetu. Hvi mnajua wangapi wanaacha chuo kwa kushindwa gharama? Bahati mbaya sana wengi ni watoto wa masikini(hasa kanda ya ziwa kwenye mbu mbumbu wengi) ambapo ndio walikua wanategemewa kukomboa. familia zao duni. au unadhani kila mtu anapenda kusomea education(ili apate mkopo 100% apunguze gharama). Tuache ushabiki. Nitakuja nimchane mtu humu ndani ohoo!
 
Ishu hapa siyo kama 5,000 inatosha au haitoshi; ishu ni je, pesa hiyo isipotosha nani ana jukumu la kutop-up?
Tujiulize, kwani wanafunzi hawa wakati wanasubiri kuingia chuo walipata wapi pesa za chakula? Kwanini huyo aliyewawezesha wakati ule hana tena nafasi katika kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ya chakula wakiwa shule?
Tutambue kuwa mahitaji ya chakula ni mahitaji ya kila binaadam na si wanafunzi wa chuo kikuu peke yao. \hivyo basi, tukiunga mkono wanafunzi hawa kupewa 10,000 kwa siku kwa ajili ya chakula basi tusiishie hapo, tuishinikize serikali kuwapa watanzania wote wasio na ajira kiasi hicho cha pesa. Je, tunaweza?
Uzalendo kwa kizazi cha leo haupo kabisa. Kizazi cha leo kimerithi Uhuru toka kwa kizazi kilichopita. Je, kizazi chetu kinajiandaa kurithisha nini kwa vizazi vijavyo?
 
Nimegundua hii nchi haiendelei sababu ya wapumbavu wachache. Unakurupuka tu kutoa tuhuma bila kufanya uchunguzi wa Kina. Udsm wako sawa, 5000 hela gani kwa sasa. Ngoja nikupe bajeti yangu uone. Mimi niko St Joseph College, ada ni milioni 2 na laki 7, napata 80% ya mkopo (piga hesabu 20% bei gani), chakula asb, mchana na jioni sh 3000, kodi ya chumba(cha kawaida sana) elfu 80 kwa mwezi(umeme na maji juu yangu). Bado nalipa elfu 70 za mitihani kila semister, hapo sijaweka gharama za internet(chuo hakina huduma hiyo/ hata kama kinayo hostel ndo kila kitu), vocha, nauli etc. Unadhani 5000 inatosha? Tena kila likizo niende mwanza na kurudi(elfu 5 ni hesabu ya siku unazosoma darasani pekee). Watu wana hali ngumu, mabinti wanajiuza huku, watu wanadhaliliika acheni ushabiki wa kijinga. Kushnda njaa na kua omba omba tushazoea. Kufukuzwa hostel tushazoea. Ndio maana vijana wa vyuo wanakichukia chama tawala, kimewasahau na kuwaletea propaganda kama sa hvi wanalaumiwa bodi ya mikopo, wakati serikali ndio hawana kitu. Udsm ni wapganaji wa kweli, wanataka ukombozi wa wote, hata sie tulio magerezani(hapa ukigoma tu huna chuo) wanatufikishia kilio chetu. Hvi mnajua wangapi wanaacha chuo kwa kushindwa gharama? Bahati mbaya sana wengi ni watoto wa masikini(hasa kanda ya ziwa kwenye mbu mbumbu wengi) ambapo ndio walikua wanategemewa kukomboa. familia zao duni. au unadhani kila mtu anapenda kusomea education(ili apate mkopo 100% apunguze gharama). Tuache ushabiki. Nitakuja nimchane mtu humu ndani ohoo!

Ukichunguza sana utakuta ndio wale waliogomea maziwa na blue band....Kama hela haikidhi matumizi ya msingi ya mwanachuo nini kigezo cha kumpa hiyo posho?..ili iwepo kwenye ilani????
 
Funguka akili yako tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato uwapo likizo.
Ulimwengu mzima hakuna anayeweza kujitosheleza kwa kutegemea msaada tu ila mwenyewe ufunguke akili namna gani uongeze ziada
Lazima utakua abroad!..Box jema!
 
Nimegundua hii nchi haiendelei sababu ya wapumbavu wachache. Unakurupuka tu kutoa tuhuma bila kufanya uchunguzi wa Kina. Udsm wako sawa, 5000 hela gani kwa sasa. Ngoja nikupe bajeti yangu uone. Mimi niko St Joseph College, ada ni milioni 2 na laki 7, napata 80% ya mkopo (piga hesabu 20% bei gani), chakula asb, mchana na jioni sh 3000, kodi ya chumba(cha kawaida sana) elfu 80 kwa mwezi(umeme na maji juu yangu). Bado nalipa elfu 70 za mitihani kila semister, hapo sijaweka gharama za internet(chuo hakina huduma hiyo/ hata kama kinayo hostel ndo kila kitu), vocha, nauli etc. Unadhani 5000 inatosha? Tena kila likizo niende mwanza na kurudi(elfu 5 ni hesabu ya siku unazosoma darasani pekee). Watu wana hali ngumu, mabinti wanajiuza huku, watu wanadhaliliika acheni ushabiki wa kijinga. Kushnda njaa na kua omba omba tushazoea. Kufukuzwa hostel tushazoea. Ndio maana vijana wa vyuo wanakichukia chama tawala, kimewasahau na kuwaletea propaganda kama sa hvi wanalaumiwa bodi ya mikopo, wakati serikali ndio hawana kitu. Udsm ni wapganaji wa kweli, wanataka ukombozi wa wote, hata sie tulio magerezani(hapa ukigoma tu huna chuo) wanatufikishia kilio chetu. Hvi mnajua wangapi wanaacha chuo kwa kushindwa gharama? Bahati mbaya sana wengi ni watoto wa masikini(hasa kanda ya ziwa kwenye mbu mbumbu wengi) ambapo ndio walikua wanategemewa kukomboa. familia zao duni. au unadhani kila mtu anapenda kusomea education(ili apate mkopo 100% apunguze gharama). Tuache ushabiki. Nitakuja nimchane mtu humu ndani ohoo!

Wanachuo kushindwa kumaliza chuo sababu ya kukosa ada na mambo mengine si Tanzania tu ni tatizo la dunia nzima. Niliposoma chuo Tanzanzani wanachuo walioshindwa kumaliza chuo kwa matatizo mbalimbali haikufikia asilimia mbili (2%). Niliposoma chuo katika moja ya taifa kubwa duniani asilimia ya wanafunzi walioshindwa kumaliza chuo kwa matatizo mbalimbali ni asilimia nane mpaka kumi (8%-10%). Kwa maana hiyo usione tatizo la karo na matumizi kama ni tatizo la tanzania tu ila ni la dunia nzima. Na kwa taarifa yako ukiona mataifa makubwa yanatoa misaada kwa mataifa maskini kama tanzania kwa ajili ya huduma na miradi mbalimbali ni suala la kisiasa na si kiuchumi, na zaidi kwa wanaotoa pesa ni kitegauchumi. Huwezi amini maisha wanayoishi baadhi ya wananchi katika nchi hizo.

Bajeti za mwaka wa fedha serikalini ni kawaida kukwama na inabidi watengeneze mini budget ili kunusuru mambo muhimu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na huduma za umma. Nimeshuhudia watumishi wa serikali kupunguzwa serikalini kama polisi na idara nyingine ili kubana matumizi ya budget. Hayo yangefanywa Tanzania tungeinua majambia kuwafuata viongozi maofisini.

Sijaona homeless wa kutisha Tanzania ukilinganisha na homeless walivyozagaa nchi za UK, USA na nchi nyinginezo za magharibi. Nchi hizo mtu kama huna kazi moja kwa moja ni homeless vionginevyo umefanya kazi kwa kipindi kinachokubalika na hivyo unaweza kupata huduma za humanity toka serikalini na mafao mbalimbali tokana na makato ya kazi uliyofanya. Lakini huduma hizo utaishi kimaskini hakuna mfano, na wanabaki kuwa ombaomba mitaani kupata cha dinner ya kupatia usingizi. Usiku wanalala chini ya madaraja ya crossing highways. Na mtu kama huna kazi hakuna njia nyingine kabisa ya kujikimu, kwani kupata kazi ni gharama nafuu kwenda kusoma kuliko kupata ardhi.

Watanzania mnacheza na mambo kinadharia bila upembuzi yakinifu. Tuliotembea tumeshuhudia mambo na tunaona mengi mazuri kwetu, ila tu tunapenda mambo ya juu sana kwa njia ya mkato bila jasho. Mwalimu anayeelimisha taifa kwa sasa analipwa wastani wa laki mbili tu na polisi pungufu ya hizo halafu mwanachuo unataka upate laki tatu maana yake waajiriwa wanaoliingizia taifa na kutoa huduma muhimu kwa umma waendelee kukandamizwa halafu matatizo ndo yatazidi.

Maandamano ya kudai nyongeza za posho mlimani dar hapana
 
Tuache kuchanganya kila kitu na siasa unnecessarily!
Kinachozungumzwa hapa ni 5000 inatosha au haitoshi bila kujali tangu lini inatolewa...
Jibu liko wazi kuwa inatosha. Pesa inatolewa na bodi kwa ajili ya meals and accomodation. Kama kuna mtu anasema haitoshi aweke wazi budget yake ya meals and accmdtn kwa siku tuone namna inavyozidi 5000 na kufika 10000.
Let's talk by evidence!
By the way, 2kumbuke kuwa Tukitaka vingi, vingi vitatakiwa toka kwetu. Tuhakikishe kuwa tunavyotaka tunavitumia kwa msingi na si anasa.
 
Ni hatari Msomi yeyote kukinzana na kile walichokifanya wana Ud juzi, mtu upaswi kuangalia Chakula tu cha Mamantilie,,weka nauli hapo, wengine hosteli hawana wanaishi maisha ya kupanga uswahilini ambako kodi zinapandishwa kila kukicha kisa mwenyenyumba amepangisha wanachuo. Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia na yanayopelekea huitaji wa kuongeza bumu.
 
Candid ili kukwepa kutoa conclusion zisizofaa juu yako, naomba unieleze source ya tatizo hili la watanzania kutojiajiri kipindi cha likizo ni nini?tabia, ratiba, wanakuwa field au ni nini hasa??
 
Ni hatari Msomi yeyote kukinzana na kile walichokifanya wana Ud juzi, mtu upaswi kuangalia Chakula tu cha Mamantilie,,weka nauli hapo, wengine hosteli hawana wanaishi maisha ya kupanga uswahilini ambako kodi zinapandishwa kila kukicha kisa mwenyenyumba amepangisha wanachuo. Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia na yanayopelekea huitaji wa kuongeza bumu.

nafikiri tusiwe tuna'mention tu mambo bila digits...
Iweke wazi hiyo budget ya siku moja, tuone namna inavyozidi 5000.
Mgomo labda ungekuwa na logic kama ud wangeitaka bodi kuongeza items za kukopesha na sio kusingizia mfumuko wa bei kwenye same items ambao bado haujafikia threshold iliyowekwa.
 
Kiwango cha posho ya Tsh 5000 kwa siku kwa mwanachuo kwa mazingira ya sasa kwa Tanzania, ni kiwango kinachoweza msaidia kama anaakili ya kupanga vizuri bajeti yake. Kama wanachuo wanataka kuishi kwenye hoteli za gharama au kifahari ni jukumu lao na wazazi wao kuongeza pesa za kujikimu kifahari. Kiwango cha Sh laki moja na nusu kwa mwezi kama yuko makini na kufikiria zaidi future yake anaweza panga vizuri bajeti na akaishi bila tatizo kubwa. Ila kama anataka awe anakwenda kula Hamburgers McDonalds ni juu yake na familia yako kuongeza matumizi.

Tumepitia vyuo vya Tanzania na tumepitia vyuo vya mataifa makubwa, kwa ulinganifu katika masuala ya posho naweza sema kumbe Tanzania ni bora mwanafunzi anaweza pata posho hiyo kuliko vyuo vya nchi tajiri. Watu hatukulala usingizi ni darasa na kazi. Uwapo kazini wakati wa mapumziko ndo unafanya homework, hakuna kulaza damu.

Tusiwe watu wa kulaumu serikali katika kila kitu, tulaumu yale ya msingi lakini katika hili mimi binafsi nasema hapana.

Watanzania tuko wavivu mno wa kujituma na kufikiri. Mazingira yako huru mno kujishughulisha Tanzania kuliko mataifa yaliyoendelea.

Utakuta walimu wanakimbilia kufundisha shule za mijini, kumbe shule za vijijini zina nafasi zaidi kwa kujiongezea pato kwa kujishughulisha na kilimo au kufungua biashara ndogo ndogo kusaidia wanavijiji kupata bidhaa ambazo wanapata taabu kuzifuata mbali. Mshahara wake ungezalisha zaidi kuliko mijini anamalizia kwenye starehe na gharama kubwa ya maisha.

Athari wanazopata wanachuo katika migomo yao ni kubwa kwao wanafunzi kuliko viongozi wanaowanyooshea vidole wakati wanaishi maisha ya starehe, na waendapo vyuoni ni kwenda kuwapiga msasa wa kisiasa tu. Kinachofanyika sasa vyuoni ni kama cheer ambayo ni kufuata mkumbo tu na kulazimisha wasiotaka lazima wafanye vinginevyo watadhurika, huku ni kuwanyima wengine uhuru wao wa kujiamulia wanavyotaka. Haki ya uhuru ni uamuzi wa dhamira safi baada ya upembuzi yakinifu.

Serikali ina mengi ya kufanya si wanafunzi tu, elimu, mawasiliano, afya, na huduma nyingine za jamii. Hata Chama kingine kikitawala hakitamaliza matatizo hayo kwa siku moja.

mchanganuo wako ni mzuri lakini uko more theoretical.
Mfano tuchukulie matumizi ya mwanafunzi ya kila siku.
1.chai na chapati 2=600/-
2.sahani ya wali na nyama=2000/-(mchana)
3.chipsi mayai=1500/-(jioni)
4.maji madogo 2,soda 1=1500/-
5.fedha ya chumba kwa siku=500/-
Jumla =6100/-
hapa unaona ile fedha wanayopata kwa ajili ya meal na accomodation(5000/-) haitoshelezi hata ujaribu kujibana kiasi gani,yaani usinywe bia wala humberger.
Si hivyo tu,ukweli uliopo mtoto wa mkulima kutoka tandahimba anapochaguliwa kuja chuo anatarajiwa kuchangia ada ya mdogo wake pale kijijini.kuna gharama nyingine za msingi ambazo mwanafunzi anakabiliana nazo mfano nauli ya kwenda chuoni kwa wale wanaoishi nje ya campus,stationaries kwani hela wanayopewa kwa mwaka ina uwezo wa kununua kitabu cha course ya semester 1 tu,radio hata ya mkulima tu,simu na vocha kwa mawasiliano,surawili na tai ili uonekane mwanachuo kweli.

Tanzania haijaweka mazingira ya wanafunzi kufanya part time job.hakuna viwanda vinavyofanya kazi usiku,lakini pia mwanafunzi wa chuo(form vi leaver) hana ujuzi wowote wa yeye kuweza kufanya kazi.kuna mradi kama mlimani city ungeweza kuajiri wanafunzi but sidhani kama unafanya hivyo.
Sidhani kama unafurahia kuona watoto wetu wa kike wanachuo wakijiuza pale posta.

Kwa ufupi madai ya wanafunzi yana msingi na yanahitaji kuangaliwa kwa umakini bila ushabiki wa kisiasa.
Mapendekezo:badala ya kutoa fedha ya meal&accomodation serikali kupitia board ya mikopo ikopeshe fedha ya KuJIKIMU ambayo itajaribu kuadress mahitaji muhimu ya mwanachuo.lakini hii isiwe kwa wanafunzi wooote isipokuwa wale wachache waliofaulu vizuri(div one na two).hii itaondoa migomo ya mara kwa mara.
 
MAWAZO YAKO HAYATOFAUTIANI NA YULE MVIVU WA KUFIKIRI, EPHRAIM KIBONDE!
Kama viongozi wa serikali wenyewe wamekiri kuwa pesa hiyo ni ndogo kulingana na gharama za maisha ya sasa,,,,wewe umeibukia wapi na vimadai vyako vya kitoto!Infact wewe ndo unamawazo ya kitoto na kilimbukeni,,,embu kaa ufikirie,najua wewe ni kilaza ila fikiria hili:-
UNALINGANISHA KIPATO CHA WANAFUNZI NA MAASKARI??

KIMSINGI Mr. Kilaza tafuta kitu kingine cha kuzungumzia, NAONA ELIMU YAKO NI YA KUUNGAUNGA NA HAIJAKUSAIDIA HATA KIDOGO!!!!!!!!!!

mchanganuo wako ni mzuri lakini uko more theoretical.
Mfano tuchukulie matumizi ya mwanafunzi ya kila siku.
1.chai na chapati 2=600/-
2.sahani ya wali na nyama=2000/-(mchana)
3.chipsi mayai=1500/-(jioni)
4.maji madogo 2,soda 1=1500/-
5.fedha ya chumba kwa siku=500/-
jumla =6100/-
hapa unaona ile fedha wanayopata kwa ajili ya meal na accomodation(5000/-) haitoshelezi hata ujaribu kujibana kiasi gani,yaani usinywe bia wala humberger.
Si hivyo tu,ukweli uliopo mtoto wa mkulima kutoka tandahimba anapochaguliwa kuja chuo anatarajiwa kuchangia ada ya mdogo wake pale kijijini.kwa hiyo kuna gharama nyingine za msingi ambazo mwanafunzi anakabiliana nazo mfano nauli ya kwenda chuoni kwa wale wanaoishi nje ya campus,stationaries kwani hela wanayopewa kwa mwaka ina uwezo wa kununua kitabu cha course ya semester 1 tu,vocha,radio hata ya mkulima tu,simu na vocha kwa mawasiliano.

Tanzania haijaweka mazingira ya wanafunzi kufanya part time job.hakuna viwanda vinavyofanya kazi usiku,lakini pia mwanafunzi wa chuo(form vi leaver) hana ujuzi wowote wa yeye kuweza kufanya kazi.kuna mradi kama mlimani city ungeweza kuajiri wanafunzi but sidhani kama unafanya hivyo.
Sidhani kama unafurahia kuona watoto wetu wa kike wanachuo wakijiuza pale posta.

Kwa ufupi madai ya wanafunzi yana msingi na yanahitaji kuangaliwa kwa umakini bila ushabiki wa kisiasa.
Mapendekezo:badala ya kutoa fedha ya meal&accomodation serikali kupitia board ya mikopo ikopeshe fedha ya kujikimu ambayo itajaribu kuadress mahitaji muhimu ya mwanachuo.lakini hii isiwe kwa wanafunzi wooote isipokuwa wale wachache waliofaulu vizuri(div one na two).hii itaondoa migomo ya mara kwa mara.

hoja yako inanguvu mheshimiwa,,,,bravoooo!!!
 
:sad: mi nadhani we hujui maisha ya vyuo vikuu vya Tanzania, maisha huwaga ni magumu sana, acheni kuongelea wanafunzi ambao wametoka kwenye familia zinazojiweza, maana hao ndio wanaweza kufanya na kununua vitu vya anasa kama hivyo sababu wanaogezewa fedha na familia zao, lakini kwa mwanafunzi anayetegemea bumu la 5000 kwa siku hawezi fanya hayo hata siku moja, waacheni wanafunzi wapiganie haki yao. wanastahili kufanya hivyo.
 
Hi members, naomba hili swala la mgomo wa chuo kikuu kuhusu nyongeza ya pesa za matumizi mliangalie kwa umakini. Hivi sh 5000 inaweza tosha kula milo 3, kodi,stationary na nauli? SO, MGOMO WAO NI HALALI NA SERIKALI WANATAKIWA WAUFANYIE KAZI.
 
Hivi majukumu ya UVCCM yamebadilika au yameongezeka kuitetea serikali kwenye JF
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom