Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machungwa, zabibu hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi?

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,340
  Likes Received: 2,416
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani umesema ya kwamba kula machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke).


  Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu(Citrus Fruit) pekee kwa mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla.


  Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.


  Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu cha East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoidsambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.


  Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matunda na mboga za majani kwa kila kipindi cha miaka 4. Timu hiyo ya utafiti iliangalia uhusiano wa aina sita ya flavonoids - flavanones,

  anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols
  na flavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke. Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones kwenye matunda chachu walikuwa na

  asilimia 19 ya uwezekano wa kupunguza kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango kidogo cha matunda hayo.

  Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha 25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa

  katika jarida la Medical Journal Stroke umesema flavanones hupatikana kwa asilimia 82 kwenye machungwa na juisi ya machungwa na hupatikana kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu. Hata hivyo watafiti hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza

  kiwango kikubwa cha flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na si juisi za machungwa zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.


  Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition) na ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi”.
  Flavanones hutoa kinga dhidhi ya

  kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye ubongo na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi mwilini
  (Anti-inflammatory effect).

  Utafiti uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa matunda chachu na juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi aina ya Ischaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo (Intracerebral Haemorrhage).

  [​IMG]

  Utafiti mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna uhusiano wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano wa zabibu na mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.


  Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula kiwango kikubwa chaantioxidant karibia asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni wachache tu kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao walikuwa na kiwango kidogo cha antioxidant.


  Matokeo ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina nyingine pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika mwili wa binadamu.


  Kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula lishe bora iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za majani kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha ulaji chumvi (kwani watu wenye asili ya Kiafrika wana

  kiashiria cha asili kinachojulikana kama salt retention gene ambacho hufanya kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango kikubwa na hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi), kupunguza uzito (kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya kulingana na umri na urefu wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala masaa ya kutosha na kupunguza msongo wa mawazo.
  Tafiti za afya
   
 2. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,248
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  huwa sipendi kabisa matunda chachu!
  kwa kusoma hapo ngoja nitajitahidi kuanza kuyatumia!
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,033
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu
  nisaidie hili, nimekuwa kwa karibia miezi miwili sasa natumia juisi
  ya mchanganyiko wa chungwa na limao badala ya chai asubuhi
  nishauri je niendelee na hili zoezi au linaweza kuniletea tena shida huko mbele.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,340
  Likes Received: 2,416
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri na kuhusu mwili wako ukoje? samahani kama nitakukwaza?Mnene au mwembamba? Mamndenyi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,033
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  mimi ni saizi ya kati siyo kibonge wala mwembamba.
  nashukuru MUNGU kwa kuwa sina tatizo la sukari wala presha,
  japo kwa ukweli wakati mwingi najibana sana kwenye kula na kunywa.

   
Loading...