Machungu ya mgawo wa umeme kuongezeka - NANI WA KULAUMIWA?

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
MAKALI ya tatizo la umeme yamezidi baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kueleza kuwa mgawo wa umeme sasa si wa mikoa saba pekee, bali mikoa yote inayopata umeme kupitia gridi ya taifa.

Shirika hilo limesema hali hiyo inatokana na mitambo na mashine takribani minne ya kuzalisha umeme kupata hitilafu, ukiwamo wa Kihansi mkoani Morogoro, ambao uzalishaji wake umepungua kutokana na maji katika bwawa hilo kupungua kwa sababu za ukame.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa shirika hilo, Badra Masoud, aliitaja mitambo hiyo iliyopata hitilafu kuwa ni mashine namba tatu ya Songas na mtambo wa Ubungo unaotumia gesi ambao injini zake mbili ndio zilizopata hitilafu.

Pia alisema, pamoja na mitambo hiyo, mashine namba mbili ya Pangani New Water Falls nayo ilipata hitilafu na kupunguza uzalishaji na mtambo wa Kihansi ambao uwezo wake wa kuhifadhi maji ni mdogo hivyo kutokana na uhaba wa mvua, maji yamepungua na kupunguza uzalishaji wa mtambo huo wenye uwezo wa kuzalisha megawati 180.

“Pia hivi karibuni mgawo wa umeme ulikuwa mkali kutokana na mitambo ya IPTL yote kuzima baada ya mafuta kuisha na kusababisha sasa upungufu wa megawati za umeme 150,” alisema Masoud.

Alisema, pamoja na matatizo hayo, Tanesco imekuwa ikijitahidi kutafuta ufumbuzi ili mgawo huo usidumu kwa muda mrefu ambapo tayari kwa kushirikiana na Menejimenti ya IPTL, mafuta yamewasili na mitambo ya kampuni hiyo ilianza rasmi kuwashwa jana na inatarajiwa kutoa megawati 80.

Alisema, kumalizika kwa mafuta ya IPTL kulitokana na kampuni hiyo kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme baada ya mitambo mingine kupata hitilafu, hali iliyosababisha mafuta hayo kumalizika kabisa na hivyo mitambo hiyo kukata uzalishaji.

Kwa mujibu wa Tanesco, ratiba ya mgawo wa umeme itaendelea katika mikoa hiyo inayopata umeme kupitia gridi ya taifa katika baadhi ya maeneo yake na aliitaja maeneo yatakayoathirika kuwa ni Kinondoni Kusini, Mwanza, Tabora, Iringa, Shinyanga, Morogoro, Kilimanjaro, Kinondoni Kaskazini na Tanga.

Maeneo mengine kwa mujibu wa tovuti ya shirika hilo ni Arusha na Ilala ambapo ratiba za mgawo wa umeme katika maeneo hayo zimeishia hadi Jumapili Ijayo.

Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara walizungumza na gazeti hili, walilalamikia hali hiyo ya mgawo ambayo wamedai kuwa imekuwa ikikwamisha shughuli zao za kibiashara na kusababisha kuongezeka kwa gharama za majenereta.

“Sasa hapa hata ukimuongezea mteja bei ni malalamiko, lakini kiukweli kabisa, mgawo huu siku zote unaturudisha nyuma kwa kuwa inabidi kutoa fedha za ziada za mafuta ya petroli kwa ajili ya jenereta na hizi mashine zinakula sana mafuta,” alisema Prakash, mfanyabiashara wa duka la bidhaa za jumla.

Kwa upande wake, mkazi wa Kinondoni, Nasri Ali aliomba serikali ijitahidi kumaliza mapema matatizo yanayosababisha mgawo huo wa umeme kwa kuwa kipindi cha sasa joto limezidi hivyo majumbani na maofisini hakukaliki bila umeme.

“Huwezi hata kununua chakula cha bajeti kwa kuwa kitaharibika kwenye jokofu,” alisema Ali. Mapema mwaka 2006, Tanzania ilipata ukame uliosababisha matatizo makubwa ya umeme kiasi cha serikali kulazimika kuagiza mitambo ya dharura ya kufua umeme kutoka nje ya nchi.
 
- Mitambo kupata hitilafu!
- Maji kupungua kwenye mabwawa ya kuhifadhia maji!
- Mafuta ya kuzalishia umeme kwenye mitambo ya IPTL kuisha kabisa!
Hivi katika orodha hiyo hapo juu kuna hata siku moja mgawo wa umeme nchini umetokana na sababu tofauti nje ya hizo? Do we learn anything from the past kama waafrika wa Tz.
My take is that waafrika ni wagumu sana kujifunza kutokana na makosa/history!
 
- mitambo kupata hitilafu!
- maji kupungua kwenye mabwawa ya kuhifadhia maji!
- mafuta ya kuzalishia umeme kwenye mitambo ya iptl kuisha kabisa!
Hivi katika orodha hiyo hapo juu kuna hata siku moja mgawo wa umeme nchini umetokana na sababu tofauti nje ya hizo? Do we learn anything from the past kama waafrika wa tz.
My take is that waafrika ni wagumu sana kujifunza kutokana na makosa/history!
we ni mzungu?kama siyo it means bado una colonial hangovers.
 
Back
Top Bottom