Macho Ulaya, masikio China

Gitaa

Member
Nov 10, 2014
18
14
MACHO ULAYA, MASIKIO CHINA.

Umewahi kuona mtu anaangalia Tv huku anasikiliza redio? Hapo utakuta sauti ya Tv iko chini sana. Hii ina maana kuwa anapenda kutazama kinachooneshwa lakini pia hataki kupitwa na kinachotangazwa redioni. Bahati mbaya ni kwamba hauwezi kuwa unasoma gazeti, unaangalia Tv na kusikiliza redio kwa wakati mmoja kwasababu njia za fahamu zitumikazo hapo ni mbili tu, macho na masikio. Kwahiyo ili uelewe unapaswa aidha kuzingatia kimoja ama viwili huku ukigawa majukumu kwa masikio kusikiliza na macho kuona. Zamani tulikuwa tukipata taabu sana kuweza kugawanya majukumu ya milango hii ya fahamu hasa katika masuala ya mpira. Ulikuwa unalazimika aidha kwenda uwanjani kuangalia ama kusikiliza kwenye redio. Ilikuwa ni nadra sana kufanikisha viwili hivi kwa pamoja. Lakini kwa jinsi teknolojia ilivyokua hata ligi kuu ya Tanzania unaweza kuitazama huku unasikiliza muziki redioni.

Unatambua kuwa ligi kuu ya China ina umri wa miaka 12 tu? Eeeh hii hii inayoitwa China Super League(CSL) kabla ya 2004 walikuwa na ligi daraja la kwanza tu. Katika kipindi kama hiki jamaa wameifanya ligi kusimama, usiniambie kuwa ni suala la utandawazi wakati kwetu, ligi ina umri mkubwa kuliko mimi na utandawazi haujaivusha. Siku zote nimekuwa muumini wa "opportunists" waviziaji ama watu wanaotumia fursa vyema. Turudi kwenye CSL. Ligi hii ina jumla ya timu 16 (kama ligi ya Tanzania). Mtindo wa kushuka na kupanda daraja ni timu mbilimbili. Kama ilivyo uingereza CSL ina ligi ya timu za akiba lakini cha kufurahisha ni kuwa, kila timu iliyoko ligi kuu ina timu ya U20, U17 na U15, ambazo nazo hucheza ligi yake. Ligi hii huanza mwez wa pili au wa tatu na kuisha mwezi wa kumi na moja au wa kumi na mbili. Timu saba tu zimekwisha shinda ligi hii huku Guanghzou Evergrande ikiongoza kwa kubeba mara tano.

Yatakuwepo mengi sana uyajuayo kuhusu ligi hii ya China, pengine kwa kusoma ama kusikia. Ninachotaka tuzingatie leo ni maajaby yanayotendeka nje ya viwanja vyake, yaani katika ofisi za timu. Ligi nyingi za nje ya ulaya zimekuwa ni vyanzo vya kuzalisha vipaji vchanga(mfano ligi za Brazil na Argentina) ama zimekuwa zikipokea vipaji vilivyochoka ulaya. Wataalamu wa mambo husema watu huenda kula pensheni huko (mfano ligi ya Marekani na Uarabuni). Hata ligi ya China ilipoanza kuwanunua akina Anelka na Drogba tuliichukulia ni "ligi ya pensheni" lakini nionavyo sasa hilo si kweli tena. Kilichonishtua mimi ni mkataba wa TV walioupata hawa jamaa billion nane dola za Kimarekani!!!! Inashangaza iliyoje, hata Eredivise hawajafika.

Kinachonifurahisha katika ligi hii ni kuwa mambo haya sio ya kupita tu. Rais wa nchi, ndiye ameshikia bango suala hili. Ndiye ameainisha uanzishwaji wa sera bora ya mpira wa miguu nchini humo. Wachina ni watu wa kutazama, kupenda na kuamua. Wakiamua jambo lao linakuwa. Walipoamua kutengeneza nakala za vifaa vya kielektroniki vya makampuni makubwa wakaweza, walipoamua kuwekeza Afrika, mzungu amewapisha. Kwasasa China ndio nchi inayoongoza kwa uwekezaji na kufanya biashara Afrika. Kwa lugha nyingine ndio wanaoongoza kwa umiliki wa rasilimali duniani maana Afrika ina rasilimali za kutosha sana. Sasa hizi pesa wanazozitoa kwetu huku ambazo kila siku tunawapelekea zinawekwa wapi kule kwao? Ubunifu wao umeingia katika soka.

Tofauti na inavyoaminiwa sana kuwa waChina ni watu wa vitu rahisi kwa bei rahisi, kwenye mpira wameingia na gia nyingine. Ni kama wamekuja kupambana na vilabu vya ulaya. Wengi tusingeshangaa kununuliwa kwa Drogba au Anelka kule lakini kwa habari ya Texeira, Ramirez, Jackson Martinez, Gervinho mhh. Wako serious. Kumbuka huko kuna Robinho, Asamoah Gyan na kocha kama Scolari. Asubuhi nikipita mitandaoni ninakutana na habari kuwa Rooney, Obafemi Martins na Ezequiel Lavezzi wanahitajika huko nikatabasamu tu. Kwa kasi hii hawashindwi kumshawishi Mata ambaye Mourinho hamtaki pale Utd na si muda mrefu watapiga hodi kwa Akina Coutinho, Herera, Ox na wengine. Kwa Remy wameshafika sasa cha kufurahisha ni kuwa wameweka hata dau kwa Messi.

Kinachonifurahisha mimi sio hizo bei zao bali ni kuwa tunapata sehemu nyingine ya kusikiliza mambo mpira, lakini kizuri zaidi ni kuwa hawa wataalamu wanaonunuliwa huko hawaendi kula pensheni tu, wanakwenda kuwapa motisha vijana wa umri wa chini ya miaka 20 ambao wanacheza kule. Ni funzo zuri toka kwa wachina. Ni kweli hatuna rasilimali pesa lakini kwanini tusipate sera nzuri ya michezo? Wachina wametupita kuanzia teknolojia na sasa wanaenda 'kutuzidi sana' kwenye mpira. Kuna timu zina uwezo wa kumiliki shule za mpira wa miguu lakini zinasubiri mpaka 'club licencing' ya CAF iseme kuwa ni lazima kumiliki timu za vijana. Hata hivyo bado hakuna sera nzuri kwa soka la vijana ambayo hata hizi timu chache zenye timu za vijana zinapaswa kuitumia. Sisemi kuwa na sisi tuanze kuwanunua akina Abou Diaby kuja kuwapa motisha wadogo zetu, la hasha, hatuna uwezo huo lakini je, uwezo wetu umeishia hapa?

Bw. Malinzi alipokuwa akigombea urais wa TFF nilimfurahia na kuona ni tumaini jipya kwa soka la vijana, sijui amefika TFF akanywa maji yaliyowalevya akina Rage naye akasinzia au amenogewa na utamu wa mgawo. Kajitahidi kuwa nchi yetu itaandaa fainali za U17 mwaka 2019 lakini akasahau kuwa tunahitaji maandalizi ya kudumu sio ya u17 fainal za afrika tu. Magufuli wa hapa kwetu anaweza asiwe na kipaumbele kama Magufuli wa China(Rais Xi), je Malinzi wa hapa kwetu hawezi kufanya kitu angalau tukawa tu na kanuni zenye kulazimu ligi iwe na timu za vijana? Au suala ni udhamini? Kama ni hvyo ichezwe ki kanda tu kama ligi daraja la kwanza.

Kiukweli nmechoshwa na timu kufungwa michuano ya kimataifa halafu sababu ikawa uzoefu. Tutautoa wapi uziefu ikiwa mtu anatoka kucheza ndondo anaenda ligi kuu? Tunategemea zali la Vardy? Uzoefu tutaupataje ikiwa mtu wa miaka 24 aliyeko mtaanindo kwanza anawaza namna ya kucheza afike daraja la tatu. Anyway nisiumize sana kichwa kuhusu mpira wa Tanzania yangu maana najua Samatta atabaki Samatta, na sisi ni wawindaji wa vipaji maana hatutambui kuwa jua la mawio na machweo yanafanana lakini sio sawa, tuko bize kuangalia ujuzi wa Messi na Ronaldo na kusikiliza dau wanaloweka waChina. Sio mbaya maana kwa sasa macho yako Ulaya na masikio yetu yako China kuja kutahamaki wao mbele sisi nyuma.

GULINJA E. GASPER
 
Uchambuzi mzuri sana...jaribu kuupeleka na kwenye magazeti ukasomwe na huko pia.
 
Macho yanatakiwa yawe Afrika, na Ligi haina Miaka 12, kubadili jina au muundo hakuifanyi Ligi irejee utotoni... Bado inakuwa Top League, kama ilivyokuwa!
Tutaendelea kuwa wateja kwa kujiendekeza...
 
hivi michezo Kung Fu na Tai Chee bado ipo tena china

Maana enzi zetu china walitamba sana na hii kitu siku hizi wao ni simu feki tu
 
hivi michezo Kung Fu na Tai Chee bado ipo tena china

Maana enzi zetu china walitamba sana na hii kitu siku hizi wao ni simu feki tu
...wachina wana bidhaa za kila aina;ukitaka feki wanakupa,ukitaka original wanakupa.Unadhani huwa wanapeleka bidhaa mbovu kwenye masoko yao ya Ulaya na Marekani?!
 
Alishindwa tajiri wa Anzhi Muchachkala FC ambae alispend big na akashindwa ije kuwa China.
China ni kama MLS ilivyoanza na itaishia kufa tu
 
...wachina wana bidhaa za kila aina;ukitaka feki wanakupa,ukitaka original wanakupa.Unadhani huwa wanapeleka bidhaa mbovu kwenye masoko yao ya Ulaya na Marekani?!

Naelewa hii mkuu ila naongelea kwetu nyumbani kwanza na pia kuhusu hiyo michezo yao
 
Unaonekana una elimu kiasi lakini swala dogo tu limekupita
'ukubwa wa soko wa bidhaa'
ukubwa wa soko wa baadhi ya bidhaa unategemea sana idadi ya watu
china ina watu bilioni 1.3
huwezi linganisha na Tanzania
hata kama ligi yetu ni kongwe....Tanzania klabu za kujaza uwanja wa taifa ziko ngapi?

wakati uwanja wenyewe ni elfu 60 tu
wachina wanaweza nunua wachezaji wa nje sababu tayari wao wana soko la TV na waingiaji uwanjani
kabla ya kufanya haya walidhamini timu za ulaya kwenda kwao wakaona soko likoje
na ligi za ulaya zinaoneshwa kwao wanajua soko likoje

wao tayari wana soko...kinachofanyika now ni kuwashawishi tu wateja
 
Unaonekana una elimu kiasi lakini swala dogo tu limekupita
'ukubwa wa soko wa bidhaa'
ukubwa wa soko wa baadhi ya bidhaa unategemea sana idadi ya watu
china ina watu bilioni 1.3
huwezi linganisha na Tanzania
hata kama ligi yetu ni kongwe....Tanzania klabu za kujaza uwanja wa taifa ziko ngapi?

wakati uwanja wenyewe ni elfu 60 tu
wachina wanaweza nunua wachezaji wa nje sababu tayari wao wana soko la TV na waingiaji uwanjani
kabla ya kufanya haya walidhamini timu za ulaya kwenda kwao wakaona soko likoje
na ligi za ulaya zinaoneshwa kwao wanajua soko likoje

wao tayari wana soko...kinachofanyika now ni kuwashawishi tu wateja

Sijasema tununue wachezaji wa ulaya kama umesoma vzur ila nmeongelea sera ya sokka la vijana
 
Unaonekana una elimu kiasi lakini swala dogo tu limekupita
'ukubwa wa soko wa bidhaa'
ukubwa wa soko wa baadhi ya bidhaa unategemea sana idadi ya watu
china ina watu bilioni 1.3
huwezi linganisha na Tanzania
hata kama ligi yetu ni kongwe....Tanzania klabu za kujaza uwanja wa taifa ziko ngapi?

wakati uwanja wenyewe ni elfu 60 tu
wachina wanaweza nunua wachezaji wa nje sababu tayari wao wana soko la TV na waingiaji uwanjani
kabla ya kufanya haya walidhamini timu za ulaya kwenda kwao wakaona soko likoje
na ligi za ulaya zinaoneshwa kwao wanajua soko likoje

wao tayari wana soko...kinachofanyika now ni kuwashawishi tu wateja
mkuu ni kweli population ni factor ya msingi ila mbona nchi kama india ina population kubwa still hawana mpira mkubwa.

pamoja ya backup ya population ila bado kuna kitu cha ziada...sera.. commitment...hivyo ndivyo tumekosa...

tanzania inauwezo wa kuendelea kimichezo kwa hii population yake...

china pia wanauwezo wa kudrop endapo hawatakuwa makini
 
Back
Top Bottom