Machinga jijini Mwanza wasalimu amri

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
581
Leo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya wafanya biashara wadogo wadogo almaarufu kama Machinga.

kufanya biashara barabarani ambao uliItolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya jiji pamoja na mkuu wa wilaya wa nyamagana Mama Mary Tesha.

Hali ya jiji la mwanza kwa sasa ni tulivu baada ya machinga kukubali kuondoka na kwenda kwenye maeneo yaliyopangwa kwenye maeneo ya nyegezi stand , mkolani , pamoja na buzuruga ambayo ndiyo yatakuwa maeneo yao ya biashara kwa sasa.

Kwa upande wake mbuge wa jimbo la nyamagana Stanslaus Mabula wakati akihojiwa na kituo kimoja cha radio cha jiji Mwanza amesema kuwa hakuabaliani na uamuzi wa serikali wa kutaka kuwaondoa machinga jiji Mwanza bila kuwapangia maeneo mazuri ya kufanyia biashara , kwani kufanya hivyo ni kuwaonea hawa watanzania wanyonge amabao wanabangaiza kwa kufanya kazi na sasa serikali imeamua kuongeza idadi ya watanzania wasiofanya kazi hili halikubaliki kwani kwa kufanya hivyo ni kuwaonea.

Alipo ulizwa swali la kizushi je yupo tayari kuandamana na machinga kupinga kitendo hicho Mabula bila kupepesa macho alisema yupo tayari na atakuwa mstari wa mbele kupinga kitendo hicho cha serikali.

th

Kwa sasa hakuna tena matukio kama haya
 
Nmeona wa mama wanalia hadi wanagaagaa chini hapo sasa ndio namba inasomwa vizuri
 
Hii nchi kuna Kazi sana huyo aliyelala hapo ni binadamu police wanamwangalia tu.....?


Hivi kwa nini wakati wa uchaguzi uwa wanajazwa barabarani na kuondolewa baada ya uchaguzi?........

Je wamewapa maeneo ya kufanyia Kazi...?
 
Lakini ni kutoelewa tu....mji ukipangika vizuri kila mtu atapata riziki yake.
 
Waende katika maeneo yaliyopangwa maana wanawazuia wengine kufanya biashara, hata hivyo hauna eneo lisilofaa kufanya biashara hapo Mwanza japo kila biashara mwanzo ni mugumu.
Nakumbuka wenye mabasi yanayotumia MUSOMA Road walipoambiwa wahamie BUZURUGA waligoma goma mwanzoni, lakini Leo ni kuzuri kabisa watu wametajirikia BUZU hapo hapo.
Kadhalika wenye mabasi wanaotumia barabara Shinyanga walipoambiwa wahamie NYEGEZI ilikuwa kama wametusiwa, lakini leo wametajirikia hapo NYEGEZI bus terminal.
Kwa hiyo napongeza maamuzi ya kuwahamisha wamachinga ili wawapishe wenye maduka wanaolipa kodi wafanye biashara zao.
 
Back
Top Bottom