Machangudoa walalamikia biashara mwezi huu mtukufu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
BAADHI ya akina dada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wamelalamikia kuwa mwezi huu umezorota kibiashara kwa kuhisi huenda mwezi huu wa Ramadhani umeharibu biashara hiyo. Wakizungumza na NIFAHAMISHE kwa masharti ya kutotajwa majina wamesema biashara hiyo imeshuka mwezi huu na wateja ni wachache wanaofika kuhitaji huduma zao.

Wamesema wanahisi sababu ni mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wao hawafiki kwa kuwa huenda wanafunga kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kutofika kuhitaji huduma hiyo.

“Yaani hapa unavyotuona toka tufike hakuna hata mteja mmoja aliyefika kutaka kupata huduma yetu na ni lisaa limoja sasa toka tufike hapa mimi na shoga yangu” walilalama akina dada hao kwa kusikitika bila ya wasiwasi hata chembe ya aibu usoni

NIFAHAMISHE ilibahatika kupita mtaa mwingine mbali na huo wa mwanzo na kukuta akina dada wengine wanaojiuza wakilalamikia tatizo hilo hilo la kukosa wateja

Akieleza kwa masharti ya kutajwa jina moja msichana Janeth alisema “ni kweli kwa kipindi hiki wateja ni wachache naona ni kutokana na mwezi huu ambao waislamu wanafunga”

“ Hata wale watoa huduma wenzetu wakinadada waislamu hawafiki kwa kipindi hiki inaonekana na wao wanafunga wanamkumbuka mungu, lakini kwa kutofika kwao tunashukuru wateja wanaofika tunawachukua sisi kwa wingi kwa kuwa wao wanapumnzika”

Hiyo ndio hali halisi kwa baadhi ya mitaa ambayo mtandao huu ulibahatika kufanya nao mahojiano ikionyesha kuwa hata wateja na watoa huduma wanauthamini mwezi huu na kumuogopa mungu.

Lakini kama ni kweli wanamuogopa Mungu kwa nini wafanye hivyo pindi mwezi huu unapoishia. Je ni kumuogopa Mungu kweli?

Wakijibu swali hilo madada poa hao walidai kuwa hiyo ndio ajira yao ambapo serikali iliyo madarakani inasema kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.

Machagudoa hao walizema kuwa hawataacha kufanya biashara hiyo mpaka serikali itakapowawezesha na wao wapate kati ya hizo ajira zilizoahidiwana kwani na wao ni moja kati ya vijana wa nchini hii.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3023106&&Cat=1
 
Jana usiku nilipita maeneo ya sokota sugaray, palikuwa pamedorora ile mbaya,nahisi the same problem!wavute subra,bado siku chache if so!
 
Lol! Vijana wa kiwembe Muhhamad wako likizo. Hata biashara ya kitimoto pia imedorora, du!
 
Nadhani hata ile ya Makaka poa nayo itakuwa imepwaya...ngoja leo nitapita pale corner bar!
 
Back
Top Bottom