machafuko Syria maonyesho Arusha !

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,917
31,157
Maonyesho ya Syria mjini Arusha ni aina vituko vinavyoendelea hapa na kudhihirisha jinsi diplomasia ya Tanzania ilivyochoka.

Dunia inashuhudia ukatili na mauaji ya kutisha yanayofanywa na serekali ya Syria dhidi ya raia waliochoshwa na mfumo kandamizi ya Rais Bashar al Assad.Umoja wa mataifa kupitia mjumbe wake maalamu Koff Annan umekuwa na mazungumzo juu ya usitishwaji wa mapigano baina ya majeshi ya serekali na wapinzani.

Nilitegemea serekali ya Tanzania ingesitisha maonyesho ya Syria mjini Arusha ikiwa ni ishara ya kukerwa na mambo yanayoendelea Syria.
 
Mkuu Ngongo nchi haina diplomasia hii inajiendesha tu kama treni inavyofuata reli. Nilipata fursa ya kutembelea hayo maonesho nikakuta wanauza chupi za "made in China" hakuna lolote ni upuuzi tu
 
Hawa jamaa nimejaribu kuwatembelea,wana uza bidhaa zilizo kwe standard za kimataifa ila siamini kama wanatoka syria kweli au wana asili ya syria.Maana kama kweli wanatoka syria miji kama sanaa,wasingekuwa TZ wanakula Bata wakati ndugu zao wanatolewa wenge kila kukicha kuko sanaa.
 
Nchi hii haina mwenyewe enzi za Kmbarage asingekubali aibu ya aina hii.

Mkuu Ngongo nchi haina diplomasia hii inajiendesha tu kama treni inavyofuata reli. Nilipata fursa ya kutembelea hayo maonesho nikakuta wanauza chupi za "made in China" hakuna lolote ni upuuzi tu
 
Maonyesho ya Syria mjini Arusha ni aina vituko vinavyoendelea hapa na kudhihirisha jinsi diplomasia ya Tanzania ilivyochoka.

Dunia inashuhudia ukatili na mauaji ya kutisha yanayofanywa na serekali ya Syria dhidi ya raia waliochoshwa na mfumo kandamizi ya Rais Bashar al Assad.Umoja wa mataifa kupitia mjumbe wake maalamu Koff Annan umekuwa na mazungumzo juu ya usitishwaji wa mapigano baina ya majeshi ya serekali na wapinzani.

Nilitegemea serekali ya Tanzania ingesitisha maonyesho ya Syria mjini Arusha ikiwa ni ishara ya kukerwa na mambo yanayoendelea Syria.

Grasshoper head type! =magamba style.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom