Mabwepande kuna agenda gani?

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Najiuliza
Serikali inatumia nguvu na gharama kubwa kule mabwepande .yaani ni kama kuna UN operation ya refugees
Magari ya jeshi yanapishana kuweka mahema na kupeleka maji safi
mabomba yanavutwa na umeme unapelekwa.viwanja vimepimwa na wahanga watajengewa mabanda ya uani kwa gharama za serikali
chakula pia wanapelekewa
Najiuliza
mbona waathirika wa mabomu ya gongo la mboto hawakufanyiwa haya ilhali wao walikuwa wakazi halali wa eneo lililoathirika?
vp hawa wa jangwani watendewe kinyume wakati wao walikuwa ni wavamizi wa maeneo hatarishi na wakaidi wa amri za serikali?
Najiuliza
hadi wapangaji wao pia wanpewa viwanja fior free!
ndio tumefikia hapo?
kila kaya imesimika mti na kupeperusha bendera ya kijani kumshukuru jamaa na chama chake lakini je ni matumizi halali ya kodi za watz?
Matumizi ya resource kama hivi yangeelekezwa kwenye vipaumbele vya taifa hakika tungekuwa mbali
 
Wapiga kura hao wamagamba jiulizr wahanga wa gombs hali zao zikoje leo na wadau wamechangia mamilioni lakini mtu kaambulia sado ya harage na sembe na kagoro je wale wahanga wa mbagala nao vp cheque zao zinacheka au zimenuna?
 
Wapiga kura hao wamagamba jiulizr wahanga wa gombs hali zao zikoje leo na wadau wamechangia mamilioni lakini mtu kaambulia sado ya harage na sembe na kagoro je wale wahanga wa mbagala nao vp cheque zao zinacheka au zimenuna?
uwiano katika kuwashughulikia waathirika halali na waathirika wavamizi hat siuelewi
 
Ngoja nivute kiti nikae karibu na Sikirini kwani naona kuna picha inakaribia kuanza!!
 
Back
Top Bottom