samora10
JF-Expert Member
- Jul 21, 2010
- 7,594
- 4,798
Wakuu ni muda mrefu nimejaribu kufuatilia sakata la mgomo wa madaktari na serikali yetu.. Kiukweli sijafurahishwa na jinsi serikali inavyolishughulikia suala hili, Ni kama vile viongozi wetu wanaendesha nchi kidikteta na hapa sitataka kuanza kuongelea mkasa uliompata ndugu yetu Ulimboka na mengineyo mengi ila kuna mambo sio ya kufumbia macho asilani..
Fikiria ndugu yako anakufa pale muhimbili halafu mtu anasimama pale bungeni na kuuambia uma eti wamepandisha posho ya kuchunguza maiti na eti huduma ziko sawa na wananchi wasiwe na wasiwasi wakati anajua kabisa kwamba hali sivyo anavyoongea.
Turudi kwenye hoja ya msingi.. Tumesikia Serikali ikijisifia kupandisha POSHO YA KUCHUNGUZA MAITI toka 5000/= mpaka 100,000/= wakati posho ya daktari anayeacha familia yake nyumbani na kuhudumia wagonjwa masaa 24 akilipwa elfu 20!
Najiuliza hivi hawa watawala hua wanafikiria nini? Yani walimaanisha nini kuongeza posho ya kuchunguza maiti na kuacha posho ya muhimu kabisa? Ndio kusema kwamba viongozi/wanasiasa wetu wanathamini maiti kuliko huyu anayeokoa maisha ya wagonjwa? Wanataka madaktari waanze kuua ili wapate posho nene za kuchunguza maiti?
Naomba tutafakari hili..