Mabondia wa TZ wakamatwa na madawa ya kulevya Mauritius

Mkuu hao ulio wataja ni tamaa tu,kwa maisha yao wako juu mno,shida yao kumaintaine status basi,coz ukuu wanao/walikuwa nao, ukwasi wanao/walikuwa nao na madaraka wanayo/walikuwa nayo.

Kwa hiyo, ukiondoa njaa kwa mabondia, bado kutakuwa kuna vyanzo vingine vya matatizo, kama vile tamaa.

Unaona pointi yangu?
 
ahh kumbe ni vijisenti tuu according to standards za currency za sangoma wetu chenge

loh i used to hear alot of stories zamani abt timu zilizokua zikisafirisha mambo pindi zikisafiri as zilikua hazikaguliwi....but i think mambo have changed now and huyo "bosi" wao bado anatumia windows 95 kwenye bnez yake hakuweza taarifiwa kuwa mambo yamechange for now kila mtu hukaguliwa!kasoro bush tu

Kichekoooooooooo, Mh Kutoka Msheria Mkuu, kwenda dalali wa ubepari hadi kuwa songoma wa vikongwe vya shinyanga..... Kweli malipo humuhumu juani. Ataokota makopo tar 26 August 2008
 
Nasikia eti ujumbe wa tanzania ulikuwa na watu watatu, waliokamatwa ni watano, wote wanadai ni ujumbe wa tanzania!
Inakuwaje?
 
Mzee wazaramo wana msemo mzuri sana; zilongwa mbali zitendwa mbali, yaani unasema kingine na unatenda kingine. Kukwambia idadi halali ya wanaosafiri si ndo kuzuia dili za wasafiri feki kama ilivyotokea !!

Ninachojua wachezaji wetu huwa hawajui lo lote kuhusu safari,kama wale waliokwenda na mipira sijui wapi kule.Umesahau juzi hapa kuna timu ilikwenda kwa madiba kufanya mazoezi wakaishia kucheza kijijini.Wiki ya pili wale wasanii maarufu si ilikuwa waende kwa madiba kujifua,mbona chuo kipo bagamoyo hatua chache tu.

Tamaa kweli ipo,lakini wengi hawajui kinachoendelea.Hukumu ya madawa ya kulevya kule Mauritius ni kifungo cha maisha,maana yake washikaji wanaweza wasirudi tena Vingunguti maisha yao yote.
 
Any updates za hawa mabondia?au ndo kusema wameshahukumiwa kifungo huko?
 
Any updates za hawa mabondia?au ndo kusema wameshahukumiwa kifungo huko?

Mabondia waliokamatwa na mihadarati nje...Polisi: Walitumwa na kigogo wa Dar

sogeza Habari Zinazoshabihiana
• Maiti aokotwa akielea bonde la Msimbazi 08.04.2008 [Soma]
• Siri za Uchaguzi Mkuu zaanza kufichuka 17.04.2006 [Soma]
• Msambaza mihadarati mstaafu ajitokeza 02.12.2006 [Soma]

*Wamo wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
*Walidakwa mtaani Morisi wakiiuza kwenye 'rambo'
*Jeshi lataka maelezo BFT walikwendakwendaje huko


Na Joyce Magoti

JESHI la Polisi nchini limethibitisha kukamatwa kwa mabondia watatu na raia wawili Watanzania nchini Morisi (Mauritius) wakiwa na mihadarati na kusema walitumwa na mfanyabiashara wa Dar es Salaam.

Mabondia hao, Fills Ramadhani (30) mwenye pasipoti namba AB 226128 ya Tanzania, Ally Rajabu (36) pasi namba AB 288440, Nathaniel Elias (39) pasi namba AB 279681 na Emilian Patrick (27) mwenye pasi namba AB 082456.

Wengine ni Petro Charles (30) mwenye pasi namba AB 083452 na Irenge Nasoro Mareo (43) pasi namba AB 080729 na walikamatwa pamoja na mwanamke wa Kenya Bi. Prisila Wanja 'Nyeri' mwenye pasi namba A 1039833 ya Kenya, wakiwa na pipi 373 za dawa ya kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilo sita.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Naibu Kamishna wa Polisi, Bw. Peter Kivuyo, wakati akitoa taarifa ya kuthibitisha kukamatwa kwa wanamasumbwi hao nchini Morisi wakiwa na dawa za kulevya.

Alisema upelelezi uliofanywa na Polisi, ulibaini kuwa dawa hizo ni mali ya mfanyabiashara wa Dar es Saalam, ambaye yuko katika mtandao wa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Bw. Kivuyo alisema Jeshi lake lilishindwa kutoa taarifa mapema kutokana na kosa hilo kuwa la jinai na kuhitaji muda ili kupata taarifa sahihi na za kweli, hadi taarifa hiyo ilipotumwa kutoka Morisi ikiambatana na picha za watuhumiwa.

Alisema watuhumiwa hao kabla ya kwenda Morisi wakitokea Nairobi kwa ndege ya Morisi namba MK 5355 walipekuliwa katika viwanja vya ndege vya Nairobi na Morisi bila kupatikana na kitu chochote mpaka wakafika na kuchukua vyumba viwili vya kulala katika hoteli ya Mount View.

Alisema kutokana na taarifa za shaka za nyuma zilizokuwapo juu yao, askari wa nchi hiyo waliendelea kuwafanyia uchunguzi na Juni 11 mwaka huu, wawili kati yao walikamatwa mtaani wakiwa na mfuko mweusi wenye dawa hizo.

"Baada ya watu hao wawili kukamatwa, walipelekwa hotelini na kuunganishwa na wenzao wanne na baada ya mahojiano, walimtaja mwanamke raia wa Kenya waliyesafiri naye ndege moja huku yeye akiwa amepandia Nairobi," alisema.

Bw. Kivuyo alisema uchunguzi ulionesha kuwa watu hao walisafirisha dawa hizo kwa kuzimeza zikiwa katika vifuko vyeusi, hali ambayo ni vigumu kuonekana katika vipimo vya usalama katika uwanja wa ndege.

Alisema watuhumiwa wote walikuwa na paspoti halali na walifikishwa katika Mahakama nchini humo na kwamba Watanzania hao wanashitakiwa kuingiza nchini humo dawa za kulevya na Mkenya anashitakiwa kwa kusaidia kuingiza dawa hizo nchini humo.

"Baada ya Jeshi letu kufanya uchunguzi wa kina, tumebaini kuwa dawa hizo zilitoka hapa na ni mali ya mfanyabiashara ambaye tumepata jina lake na namba zake za simu na ni mkazi wa Dar es Salaam, ambaye pia yuko katika mtandao wa wauzaji wa dawa za kulevya," alisema.

Alisema hadi sasa hawajapata taarifa sahihi kuhusu lini kesi hiyo itasikilizwa, lakini akasema itategemea na kukamilika kwa upelelezi ikiwa ni pamoja na kasi ya usikilizaji wa kesi wa Mahakama hiyo.

Katika taarifa nyingine iliyotolewa jana na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (MMJKT), ilisema miongoni mwa watuhumiwa hao, watatu ni wanajeshi.

Wanajeshi kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Ofisa Mteule Daraja la Kwanza wa JWTZ, Nassoro Michael ambaye Polisi imemtaja kama Irenge Nassoro Mareo, ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya ngumi; Koplo Usu Petro Mtagwa au Petro Charles na Praiveti Emilian Patrick.

Taarifa ilisema mabondia hao waliombwa na Shirikisho la Ngumi (BFT) kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Taifa ya Ngumi kwa michezo ya Olimpiki itakayofanyika China Agosti mwaka huu.

Ilisema JWTZ kwa kutambua umuhimu wa michezo na ushirikiano wa muda mrefu na BFT, iliwapa kibali cha kujiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya maandalizi hayo.

"Hata hivyo, wachezaji hao waliporuhusiwa kujiunga na timu hiyo kwa muda wote wa mazoezi, walikuwa chini ya uangalizi wa karibu wa BFT, kwa vile muda wote walikuwa nao katika kambi ya mazoezi.

"BFT walikuwa na mamlaka ya kuwatumia katika michezo ya majaribio ndani na si nje ya nchi. Kwa kutambua hilo, BFT iliandika barua yenye kumbukumbu BFT/GC/Vol 2/44 ya Mei 28 mwaka huu, ikiomba kuwatumia wachezaji hao nchini Morisi katika mashindano ya pili ya Afrika yaliyoanza Juni 12-22 mwaka huu," ilisema taarifa.

Iliongeza kuwa ombi hilo lilikataliwa na JWTZ kwa barua yenye kumbukumbu namba MMJKT/3095-3 ya Juni 6 mwaka huu na kwamba utaratibu wa mwanajeshi yeyote kwenda nje ya nchi ni lazima uwe na kibali cha Mkuu wa Majeshi.

"JWTZ ilipata taarifa ya kukamatwa kwa wachezaji hao kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, ambao walikwenda nje bila kibali cha mwajiri wao.

"JWTZ itahitaji maelezo kutoka BFT ni vipi mabondia hao ambao ni wanajeshi, walisafiri nje ya nchi bila idhini ya Mkuu wa Majeshi," ilisema.

Jeshi la Wananchi, ilisema taarifa, limeanza uchunguzi ili kubaini mazingira ya utoro wa wanajeshi hao ili hatua zinazostahili ziweze kuchukuliwa.

Source: majira


JE HUYU KIGOGO NI NANI?
 
hapo ndio napoichukia tz....yan majina ya hao mabondia yametajwa hadi passport namba zao zimewekwa lakini huyo kigogo in which im sure ameshatajwa somewhere bado ni siri n wil remain to be siri...
 
Hatimaye imejulikana kuwa bondia mmoja na Kocha wa timu ya ndondi ya Tanzania hawana hatia ya kuhusika na madawa ya kulevya. Inasemekana aliyewabebesha mzigo huu anaitwa William Michael Onesmo ambaye kwa mujibu wa Serikali ya Mauritius anatakiwa kuwa jela.
Kwa taarifa zaidi soma http://drfaustine.blogspot.com/
 
Dah afadhali maana nilikuwa namhurumia Super coach Nassoro Michael nilimsikia mkewe akilia kwa uchungu alipokuwa anahojiwa na Majura kwenye kipindi cha BBC-dira ya dunia.Siku zote huwa tunasema Kamba inakatikia pabovu...Huyu Onesmo inaonekana ni mafia kweli..yaani mtu anatakiwa awe lupango bado anacheza deal!! kweli bongo kunanuka!!
 
Mzee wazaramo wana msemo mzuri sana; zilongwa mbali zitendwa mbali, yaani unasema kingine na unatenda kingine. Kukwambia idadi halali ya wanaosafiri si ndo kuzuia dili za wasafiri feki kama ilivyotokea !!


Yaani Mkuu wewe wakwetu kabsa.......!
Duuu kumbe hata humu tumo wengi.....!
Haya mwanakwetu wacha nikupe stori yenyewe lkn ..........

Kuna mpemba mmoja hapo migo anajina la ajabu ajabu ndio mwenye mzigo wake..na wala sio mama wa kikenya.
Dili hii imeharibika kutoka na mazingira yenyewe kule Mauritues yalivyo,yaani jamaa mpaka walipokua wamefika walisha tusua ila wale viongwe wakule ndio wameangausha dili nzima.
Unaweza kufika salama kama hao jamaa alafu ukakaa na mambo kwa siku kibao huko,yaani jamaa wako very tight na mambo hayo,dereva wa taksi asikari,mpokea mizigo hotelin asikari,mfagizi wa vyumbani asikari yani tight kinoma hamna upenyo.NJAA TU NDIO ILIYO WAFANYA HAO JAMAA WAKUBARI HIYO KAZI.
Alafu hao mabondia na kocha wao wako safi,ila hao watatu ndio kimbembe kipo kwao.

Alafu mwanakwetu..Unajua hapa JF kuna watu wanaongea tu hawaangalii nini sababu ya hao jamaa papmoja na kujua risk ya hiyo kazi still waliaamua kuichua...!all they can think of ..... ni kulalama tu...ohh biashara haramu...NA UFISADI JE....!!!
na dhuruma za viongozi? hela zote wanazo kwiba na kupeleka huko wanakozipeleka?

Mtoto wa mlingotini mimi (mfano) elimu darasa la saba,sina ujuzi wala ajira serikali yangu hainitambui wala kunisaidia kujikomboa katika dimbi huli la umasikini wa kuletewa kutokana na mipango mibovu ya walio juu.Mtu anakuja ananiambia kubeba tu DOla 15,000/- nikatae nina wazimu?

Wengi ya hao wano laumu wapo kwenye sehemu nyeti maofisa wabenki na wengineo MJOMBA JAKAYA katoa yale mabiliono (kama kweli yalitoka) nikopeshwe mimi msajasiria mari ,mpaka leo sijui zimeishia wapi,sasa mantaka niendelee kuvua samaki kwetu mbegani kwanza chuo chenyewe cha uvuvi mmekiua alfu nyinyi mnaendesha tu MA_VOGUE

Sababuhiyo ndio inawafanya wale jamaa ku-risk maisha yao,kuna bwana mdogo mmoja katika wale walio kamatwa(mabondia fake) hana hata familia lakini mzigo aliokua nao nyumbani mkubwa wadogo zake wanahitaji kusoma na wazazi wake pia wamezeeka alikua anatafuta njia ya kuwasaidia kwani serikari imeshindwa kumsaidia na jamii pia imemwangusha.

Ni hayo mwanakwetu.!
 
A good news from

Daily News; Monday,July 07, 2008 @00:03



POLICE in Dar es Salaam are holding the President of the Boxing Federation of Tanzania (BFT) for questioning in a bid to establish his role in the drug trafficking scandal that hit the national boxing team in Mauritius.

The country's two boxers, Emiliani Patrick Polino, Petro Mtagwa and their coach Nassoro Michael were arrested in Mauritius last month, where they were due to take part in the 2nd African Cup of Nations (CAN) Boxing competition.

Police's Anti-Drug Unit arrested Shabaan Mintanga on Friday morning after gathering evidence pointing to his involvement in facilitating three Tanzanians to travel to Mauritius as part of the delegation.

The trio, Case Ramadhan, Ally Msengwa and former Simba player Nathanael Elia were arrested together with members of the country's team, with some 5 kgs of suspected heroin valued at US$1.8 million. Chief of Anti-Drugs Unit, Assistant Commissioner of Police Godfrey Nzowa, confirmed yesterday that the BFT boss was being held at the Central Police Station for further questioning before he is taken to court.

ACP Nzowa said: "We are still working on the evidence before taking him to court on Tuesday," he said. The team of two boxers and their coach left Dar es Salaam only to be joined along the way by the three suspicious individuals, who were fully accredited as being part of the delegation.

"We interrogated him several times about these three individuals, but he insisted he did not know them," said ACP Nzowa. He added: "However, we later established that he was the one who made travel bookings for them, which means he knew what they were going to do in Mauritius."

Officials of the Anti-Drug Unit searched Mintanga's house and office and according to ACP Nzowa, they found some exhibits, "We'll communicate with our Mauritius counterparts to see if those exhibits would assist them in the case," he added.

Na bado mpaka akaozee jela kumbe kutanua kote dar na mabaloon hizo ndio zilikuwa deal zake!!!!
 
Court denies BFT boss bail

2008-07-19 08:39:46
By Rosemary Mirondo


The Kisutu Resident Magistrate\'s Court yesterday dismissed an application for bail for the Tanzania Boxing Federation President, Shabaan Mintanga, (50), who is charged with conspiracy and unlawful trafficking of narcotic drugs worth 120m/-.

Presiding Principal Resident Magistrate Euphemia Mingi while delivering the ruling said that she agreed with the prosecution side that Kisutu Court had no jurisdiction over the matter.

She added that the accused would stay in remand custody because she had no authority to give bail.

The accused advocate, Jerome Msemwa, then asked the court to give them the decision so that they could appeal at the High Court for bail.

Earlier last week, the prosecution had asked the court not to grant bail to the accused because according to illicit trafficking law, the offence is not bailable if the person is found with drugs worth more than 10m/-.


Msemwa had asked the court to grant bail to his client because he is famous, and based here in Dar es Salaam and, therefore, could not jump bail.

He added that his client had reliable sureties and would always be present in court when required.

Msemwa also told the court that the prosecution was sighting a parliamentary law instead of the constitutional law which stated clearly that every person accused of a crime is innocent until proven guilty by the court of law.

He told the court that on that assumption the law required that he be granted bail because it was his right.

He also asked the court to look at the circumstances surrounding the case because his client had never been to Mauritius where the other accused were arrested.

He also told the court that the other accused were arrested while they were already in Mauritius, and not on arrival at the airport so it was likely that they got the drugs while they were in the country.

The accused is charged that on June 3, this year at an unknown place, he conspired with other persons to traffic narcotic drugs weighing 4.8kg from Tanzania to Mauritius.

In the second count, it was alleged that on June 10, this year, the accused did traffic the said drugs to Mauritius.

The case was adjourned to August 1, this year.

SOURCE: Guardian
 
I'll be happy huu mtandao wa huyu mdau Mintanga ukizimwa wote na ngebe hizi zisiwepo tena!!Inasemekana vijana walikuwa kule mauritius wamemtaja kuwa yeye ndie kinara wa mambo yote na hapa bongo Taarifa hiyo imeshafika so huyu bwana kupata bail itakuwa hadithi kwake!!
 
Jamani Yaani M,wintanga Tu Shida Mbona

Azim Dewji

Katarajika Na Mipira Ya Wachezaji Hatuongei??????????? Y????????

Mwisho

Cishauri Waedeleze Huu Mchezo Nchafu!!!1
 
Hatimaye imejulikana kuwa bondia mmoja na Kocha wa timu ya ndondi ya Tanzania hawana hatia ya kuhusika na madawa ya kulevya. Inasemekana aliyewabebesha mzigo huu anaitwa William Michael Onesmo ambaye kwa mujibu wa Serikali ya Mauritius anatakiwa kuwa jela.
Kwa taarifa zaidi soma http://drfaustine.blogspot.com/



WILLIAM MICHAEL ONESMO HUYU WATANZANIA MLIO NJE NDIE ALIEKUTWA NA MITAMBO YA KUTENGENEZEA NA KUPAKI MADAWA YA KULEVYA

PALE KUNDUCHI!!!!NA KESI IKAISHIA CHOONI AKAONGA MAHAKAMANI MILLION 100 MKUU WAPOLISI ENZI HIZO AKALA MILLION 30 PEKEE
SASA HIVI ANAKULA KUKU MWEMA JR!!!!

UKIMTAFUTA UKAMWEKA NDANI KAMA ATAFINYWA VIZURI UNAWEZA SIKIA MAWAZIRI WETU WAKIJIUZULU NA WENGINE WALIOJIUZULU WAKIKIMBIA NCHI !!!!!ANAKULA NA WENGI HUYU HATA UKO MAUITIUS LABDA ALIKAIDI TU MASHARTI,,PALE DAR AIRPORT ANA VIJANA WA USALAMA WATAIFA WAKIMWONA TU ANATOA ISHARA WALE WA TAA WANAKULA KAMA MILLION 10 …..
WAO SI CHINI YA 15---20 MILLION ……,

RUSHWA ITAISHA SIKU WOTE WAKIINGIA KABURINI SI UZAZI HUU WA NKAPA NA KIKWETE!!!1
 
kwa mwendo huu RUSHWA KAMWE HAITAKWISHA!! huyu onesmo inaonekana atakuwa ni MAFIA mkubwa hapa Tz..
 
Hatimaye imejulikana kuwa bondia mmoja na Kocha wa timu ya ndondi ya Tanzania hawana hatia ya kuhusika na madawa ya kulevya. Inasemekana aliyewabebesha mzigo huu anaitwa William Michael Onesmo ambaye kwa mujibu wa Serikali ya Mauritius anatakiwa kuwa jela.
Kwa taarifa zaidi soma http://drfaustine.blogspot.com/



WILLIAM MICHAEL ONESMO HUYU WATANZANIA MLIO NJE NDIE ALIEKUTWA NA MITAMBO YA KUTENGENEZEA NA KUPAKI MADAWA YA KULEVYA

PALE KUNDUCHI!!!!NA KESI IKAISHIA CHOONI AKAONGA MAHAKAMANI MILLION 100 MKUU WAPOLISI ENZI HIZO AKALA MILLION 30 PEKEE
SASA HIVI ANAKULA KUKU MWEMA JR!!!!

UKIMTAFUTA UKAMWEKA NDANI KAMA ATAFINYWA VIZURI UNAWEZA SIKIA MAWAZIRI WETU WAKIJIUZULU NA WENGINE WALIOJIUZULU WAKIKIMBIA NCHI !!!!!ANAKULA NA WENGI HUYU HATA UKO MAUITIUS LABDA ALIKAIDI TU MASHARTI,,PALE DAR AIRPORT ANA VIJANA WA USALAMA WATAIFA WAKIMWONA TU ANATOA ISHARA WALE WA TAA WANAKULA KAMA MILLION 10 …..
WAO SI CHINI YA 15---20 MILLION ……,

RUSHWA ITAISHA SIKU WOTE WAKIINGIA KABURINI SI UZAZI HUU WA NKAPA NA KIKWETE!!!1

Nimefuatilia kwenye hiyo blog sijaona hizo habari za Michael Onesmo!!..Ningependa kuona japo picha yake kama imetundikwa kwenye hiyo blog
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom