Mabondia wa TZ wakamatwa na madawa ya kulevya Mauritius

Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,370
234
TIMU ya ngumi ya Tanzania iliyokwenda kushiriki michuano ya ngumi ya Ubingwa wa Afrika, wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin.

Waliokamatwa ni kocha wa timu ya taifa, Nassor Michael, bondia wa uzito wa feather Petro Mtagwa na bondia pekee aliyefuzu kucheza michezo ya Olimpiki, Emilian Patrick.

Hata hivyo, katika watu hao ambao picha zao zimewekwa kwenye mtandao huo, hawajaweza kutambulika majina yao.

Emilian Patrick ambaye anapigana kwenye uzito wa bantam (kilo 54) alipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki baada ya kupata medali ya fedha kwenye michezo ya kuzufu iliyofanyika mapema mwaka huu, Namibia.

Timu hiyo iliondoka Jumatano kwenda kushiriki michezo ya Ubingwa wa Afrika na walikabidhiwa bendera ya taifa Jumatatu iliyopita kwenye uwanja Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Le Défi Media Group wa Mauritius unaoandikwa kwa Kifaransa, umeripoti kuwa msafara huo ulikuwa na Watanzania sita wakiwamo mabondia wanne.

Mabondia hao walikamatwa na kikosi cha kupambana na dawa za kulevya cha nchini humo kwenye hoteli yao juzi usiku na dawa hizo zina thamani ya randi milioni 40 (sawa na takribani Sh milioni 600).

Taarifa hizo zinasema jana mchana wachezaji hao walitarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya Mahébourg kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya.

Maofisa wa Shirikisho la Ngumi la Mauritius walikiri kukamatwa kwa mabondia hao na kuwa Tanzania imeondolewa kwenye michuano hiyo inayotarajia kuanza leo na kufikia kilele chake Juni 25.

Alipoulizwa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania, Shaaban Mintanga, alisema hana taarifa za kukamatwa kwa watu hao na kuwa alipowasiliana nao walimwambia kuwa wamefika salama. Alisema timu yake iliondoka Jumanne ikiwa na wachezaji wawili na kocha, wakati awali ulikuwa uondoke msafara wa watu watano na kuwa yeye na bondia Ali Kimwaga walishindwa kusafiri kutokana na uhaba wa fedha.

" Timu imeondoka na watu watatu; kocha Nassoro(Michael), Emilian(Patrick) na Petro(Mtagwa) na nimewasiliana nao juzi (Jumatano) na waliniambia wamefika salama.

"Sijui kama hayo unayoyasema ni kweli kwani nilipozungumza naye alisema hakukuwa na tatizo lolote zaidi ya kunieleza kuwa wameongeza gharama za malazi kutoka dola 40 mpaka 70.

Lakini mimi niliwaambia kuwa nitazungumza na Rais wa Shirikisho la Ngumi la Mauritius, lakini mawasiliano hayakuwa mazuri," alisema Mintanga na kutoa namba + 230 9129197 ambayo hata hivyo gazeti hili lilishindwa kupata mawasiliano.

Alipoulizwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Patrick Mombo alisema hana taarifa zozote za kukamatwa mabondia hao.

na Anastazia Anyimike
wa Daily News
 
haya kazi imo humooo maofisa wa mauritius wanasema vijana wamekamatwa na kutiwa ndani,maofisa wetu wanasema vijana wamefika salama!!aibu aibuuuuu!!!
 
this reminds me of enzi za simba na yanga wakati zinavuma.....! inasemekana kila mchezaji alikuwa na mpira wake...! (kila mpira umesheheni madawa)1990's!
na hata mabondia ambao walienda italy miaka ya nyuma kulikuwa na tuhuma kama hizi.....!
TUACHENI BIASHARA HARAMU KWANI HAIINGIZII SERIKALI MAPATO NA KUHARIBU AKILI ZA WATU....!
 
Aisee hii noma kweli na aibu kwa Taifa hili.Wasije kuwa wamebambikiwa huko Hotelini kuchafua sifa ya Tz
 
taifa letu limesemaje? waziri wetu wa michezo na yeye ametoa kauli gani ?

au ndio kigugumizi kimetupaata
 
Huyo kiongozi nae fisadi tu hasemi ukweli.lakini labda waliokamatwa sio wakina Emili patrick
 
taifa letu limesemaje? waziri wetu wa michezo na yeye ametoa kauli gani ?

au ndio kigugumizi kimetupaata

si ndo mmojawapo wa maofisa wetu wa kutegemewa nasi wananchi kakwambia yeye keshaongea nao na wameshafika vyumbani mwao hao mabondia hadi na namba za simu wakampa.....sijui ni namba za huko lock up waliko au vyumba vyao ni humo jela??!!
tz is full of usanii kila kona hadi aibuu!!!
 
duh! sasa taabu kweli. wanamichezo wetu watapata taabu sana za kupekuliwa
mpaka nguo za ndani watakapokuwa wakisafiri.
 
Wamebebeshwa mizigo ya watu hao...ukute...hawajui hata thamani ya mzigo wenyewe mama mmoja wa kenye kawamaliza ..kawabebesha mzigoo yeye yuko pembenii...walijua sababu wanamichezo watapita tu...wameliwa
 
hapa lazima pana kitu hapa.....walijisahau misemo ya zamani eti wachezaji hawapekuliwi kama kweli wamekamatwa yaweza kuwa njaa
 
Malila,

Tatizo ni njaa kama uliwahi kutembelea kambi za timu za ngumi wanapofanya mazoezi unaweza kudhani ni wahuni wa Tandale kwa mtogole kuanzia mavazi yao hadi vifaa vya mazoezi na kila siku wanalia njaa....Huyo Rais wao Mintanga kila siku anatembeza bakuri kutafuta pesa...

Juzi tu hapa alikuwa analia kuwa Kampuni moja ya kutoa mikopo inaitwa Easy Finance waliahidi kuwasaidia pesa alhaj Mintanga masikini akapiga mapicha na dummy cheques wanaume akina Isaack wa Easy Finance wakala kona sijui walipiga hesabu wakaona huenda jamaa hawatapata safari ya maana ambayo wangeweza kunufaika nayo... Sasa hao mi sishangai njaa waliyonayo ni mbaya sana hawashindwi kujitoa muhanga kubeba mzigo...

hakuna siri hapo tutajua ukweli tu very soon...
 
Wamebebeshwa mizigo ya watu hao...ukute...hawajui hata thamani ya mzigo wenyewe mama mmoja wa kenye kawamaliza ..kawabebesha mzigoo yeye yuko pembenii...walijua sababu wanamichezo watapita tu...wameliwa
mkuu iweke vema hio tafadhali
 
Inasemekana thamani ya mzigo huo ni dola za amerika 1,000,000/ ambazo ni sawa na tujisenti bilioni moja.

source; BBC London
 
Inasemekana thamani ya mzigo huo ni dola za amerika 1,000,000/ ambazo ni sawa na tujisenti bilioni moja.

source; BBC London

ahh kumbe ni vijisenti tuu according to standards za currency za sangoma wetu chenge

loh i used to hear alot of stories zamani abt timu zilizokua zikisafirisha mambo pindi zikisafiri as zilikua hazikaguliwi....but i think mambo have changed now and huyo "bosi" wao bado anatumia windows 95 kwenye bnez yake hakuweza taarifiwa kuwa mambo yamechange for now kila mtu hukaguliwa!kasoro bush tu
 
Sijui ni njaa au ujinga au vyote viwili ?
Malila,

Tatizo ni njaa kama uliwahi kutembelea kambi za timu za ngumi wanapofanya mazoezi unaweza kudhani ni wahuni wa Tandale kwa mtogole kuanzia mavazi yao hadi vifaa vya mazoezi na kila siku wanalia njaa....Huyo Rais wao Mintanga kila siku anatembeza bakuri kutafuta pesa...


Na Diria nae, kama alivyodaiwa, nae alikuwa na njaa?

Na dili za Chenge je?

Na za Mkono, na Rostam, na Karamagi nao wana njaa?
 
Mkuu hao ulio wataja ni tamaa tu,kwa maisha yao wako juu mno,shida yao kumaintaine status basi,coz ukuu wanao/walikuwa nao, ukwasi wanao/walikuwa nao na madaraka wanayo/walikuwa nayo.
 
Back
Top Bottom