sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Ni saa tano na robo usiku matokeo ya uchaguzi wa serikali za mtaa yanatangazwa kwa kumtangaza mshindi wa kiti cha mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa bondeni kupitia CCM na kusindikizwa na mabomu yaliyorindima.Sababu za kurindima mabomu hayo mpaka sasa hazijulikani,hali inayopelekea kuchafua jina la chama tawala kwa kutoweza kutangazwa mgombea wake pasi na mabomu.
Wananchi wa kata hiyo wameshangazwa na tukio hilo la mabomu kiasi cha kupelekea kupoteza imani na CCM kwa kutumia vyombo vya dola vibaya kwa maslahi ya binafsi na kusahau kuwa chombo hiki ni mali ya umma na kina wajibu wa kulinda mali na raia wake.]
Iko wapi demokrasia ya kweli ikiwa hata chaguzi za serikali za mitaa zinagubikwa na ukiukwaji mbaya wa vyombo vya dola.Hali hii imeleta picha mbaya kwa uchaguzi mkuu ujao.Nini tufanye kuinusuru hali hii,kama wananchi watachoka na kuamua kujibu mapigo na kutokukubali kuonewa?