Mabomu Gongo la Mboto: Mwinyi asema hajiuzulu

Ajiuzuru halafu atamalizaje miradi yake ambayo source of capital alijua kabisa itatokana na nafasi aliyo nayo? Hajiuzuru mtu hapa! Bongo sio ya wote ni ya wajanja tu. Halafu ajiuzuru wakati anapiga hesabu kuwa Rais wa Ardhi independent ya mikarafuu??? Hapa yupo shuleni ambapo kujiuzuru sio msamiati ambao mwalimu wao hanapenda kuusemasema. Kwanza haupo msemo huo, arogwe bure hivi? No way! Mzee Ruksa alijiuzuru enzi zile sababu maadili ya viongozi yalikuwapo na kwamba mchonga aliweza kukukuonea huruma ukijiuzuru. Sasa hivi ukijiuzuru imekula kwako, sasa nani awe pionear? Labda Tunisia na Egypt ihamie Bongo!
 
Hawezi kujiuzulu kwa vile aliyemteua,that's JK,bado ana imani nae.Remember,despite milipuko ya 2009 na kukalia ripoti ya matukio hayo,bado JK aliamua kumteua tena kushika Wizara ile ile aliyovurunda.
 
Mwinyi asijiuzuru maana ye hana kosa kipindi kile aliunda kamati hakuipitia report na akaisahau kwa hiyo tatizo lake ni kusahau kwa asijizuru
 
Ndugu Dk Mwinyi,

Ningependa kuchukua fursa hii kukupongeza kwa zati kwa ufanisi wako kufuatia mlipuko wa mabomu ya Gongo la Mboto:

1)Mara hii hakukuwa na wahanga wa kijeshi kama ilivyokuwa kule Mbagala
2)Ulikuwa kiongozi wakwanza kuwepo kwenye eneo la tukio hata kabla halijaanza
3)Umekuwa jasiri kusema huwezi kujiuzulu kwa kuwa umefanya kazi yako vizuri
4)Ulimpokea Mkuu wa nchi alipokuja kuona maendeleo ya kazi huko Gongo la Mboto
5)Tunasubiri kwa hamu wapi kutafuata katika huku kulipua kwetu mabomu.

Kazi njema Bwana Waziri
 
Nimemsikia waziri wa Ulinzi Mh Hussein Mwinyi akihojiwa na VoA swahili. Pamoja na maswali mengine ameulizwa kuhusu kuwajibika kwa kujiuzulu.
Mwinyi: Kujiuzulu kunatoka na makosa yaliyofanywa na mamlaka iliyoko chini ya mtu kama itadhihirika. Tusubiri tume itakayoundwa na tupate matokeo yake kwanza.

My Take:
1. Hili ni tatizo la pili kutokea. Tume ni ya nini ikiwa ile ya kwanza hatukujua nini kilifanyaka?
2. Tunajua kuwa njia rahisi ya kiongozi asiyeweza kupambanua mambo ni tume ili kutengeneza mazingira ya kutengeneza hadithi.
3. Mh Mwinyi anataka kutufanya Watanzania mbumbumbu sana.
Dhana(concept) ya kuwajibika ina maana zaidi ya moja.
a) Kuwajibika kwa makosa ya watendaji kisheria kama alivyosema yeye Mwinyi.
b) Kupisha uchunguzi halali usioingiliwa na wale wanaochunguzwa
c) Kuonyesha machungu au kutoridhika kwa kile kilichotokea, na hapa ni vifo huku
kiongozi husika akiwa na dhamana.(sympath)

Zote (a), (b), (c) zinamgusa Mh Mwinyi moja kwa moja. Wakati leo kuna watu wana misiba mizito majumbani kwao, wengine wapo mahospitalini, watoto hawajui wazazi wapo wapi, mali zimeharibiwa na watu hawajui nini cha kufanya, makazi hakuna watu wapo kwa majirani, hivi kweli hata kama kifungu (a) na (b) hapo juu hakimhusu kiongozi, je kifungu (c) cha kuonyesha huruma na machungu nacho pia kiongozi hawezi kukifanya!!! Yaani hata huruma ya madhara yatokanayo hakuna!!, eti kwasababu tu mtu abaki kuwa waziri.

sad!!!

Nafikiri sio Mwinyi tu wa kujiuzulu, bali serikali nzima ijuuzulu na uongozi mpya uingie na wasitoke ktk vyama vya siasa.Tukubuli kuanze upya kabisa.Hapa inatakiwa geneius mmoja ambaye ataamsha morali na nyoyo za wananchi kudai hili dai.Dai halitafanikiwa kama litawekwa kwa mouno wa faida ya kisiasa.
 
Waziri mwenzetu huseni mwinyi tunakutakia maisha marefu katika kuritumikia taifa la Tanzania, kazi tunaiona undelea kuwatumikia watanzania kwa moyo wako wote.

Watu wanataka kukupunguza ili usilitumikie taifa lako

Nasema na kusema hakuna mtu hatakayejudhuru

Nasema na kusema hakuna mtu hatakayejudhuru

Nasema na kusema hakuna mtu hatakayejudhuru

No one will resign

No one will resign

No one will resign


Jeykeywaukweli
 
kwa kifupi anachosema ni kwamba kwa mtazamo wake yeye, hana kosa lolote.....sasa tume ikija na kusema anakosa, ndio ataona kuwa anakosa....kaazikwelikweli
 
hii nchi ya kingese sana,na hapa kuna tume tena OMG! hivi hizi tume zimefika ngapi sasa??mi naona kizunguzungu maana zingine hata hatukumbuki,hiyo ajali ya mama salma juzi haijaundiwa tume kweli??
 
Hadi mtakapojua kuwa nyie ndiyo wenye mamlaka ya kumweka mtu madarakani au kumtoa. Kwa vile bado nyie masikini mmegeuka watumwa wa watala, hakuna lolote mnaloweza kulifanya!

Very sad!


Mi nadhani hata wakiiga kutoa huko Arab World ni poa tu maana kuna wakati viongozi wetu wana kela sana unajua kabisa hichi ndicho kinapaswa fanyika yeye anakipindisha tena kutumia sheria fulani na vipengele fulani. Hawa viongozi watapata wakati mgumu sana 2015 kama tutakuwepo kwani huko ndiko watakapo wajibishiwa bila ubishi kabisa
 
I wish this could be possible. Mkwere huo ubavu hana, hadithi za rejea zinaonyesha kuwa Mzee Mwinyi ndiye aliyeenda kumuokota JK huko kusini (sikumbuki ilikuwa Mtwara au Lindi alikokuwa katibu wa ccm) na kuja mpa ubunge na unaibu Uwaziri, ambavyo baadae vilimfikisha hapa alipo. Kwa kuwa Tanzania hatufanyi mambo mengi kwa ujuzi tulio nao, ila ni kwa kujuana, hawezi kumfukuza kazi. Ingekuwa rahisi kwake kuridhia kujiuzulu lakini sio kumfukuza kazi. Vilevile kwa mkwere itakuwa rahisi kuridhia msamaha wa kutokulipa deni endapo atapewa ofa ofa hiyo na RA lakini sio kutumia sheria zilizopo! Hapa imekula kwetu. Labda kitakacholeta mabadiliko na hawa waondoke, ni sisi wananchi kushinikiza, yaani nguvu ya umma.

Shinikizo ndiyo suluhisho
 
Ndugu Dk Mwinyi,

Ningependa kuchukua fursa hii kukupongeza kwa zati kwa ufanisi wako kufuatia mlipuko wa mabomu ya Gongo la Mboto:

1)Mara hii hakukuwa na wahanga wa kijeshi kama ilivyokuwa kule Mbagala
2)Ulikuwa kiongozi wakwanza kuwepo kwenye eneo la tukio hata kabla halijaanza
3)Umekuwa jasiri kusema huwezi kujiuzulu kwa kuwa umefanya kazi yako vizuri
4)Ulimpokea Mkuu wa nchi alipokuja kuona maendeleo ya kazi huko Gongo la Mboto
5)Tunasubiri kwa hamu wapi kutafuata katika huku kulipua kwetu mabomu.

Kazi njema Bwana Waziri


Kazi yako inaonekana hapa chini wewe sijui tukuitaje shujaa au msaliti?


Gongo1.jpg
 
Back
Top Bottom