Mabomu Gongo la Mboto: Mwinyi asema hajiuzulu

Baba yake ndiye MSTAAARABU wa kwanza nchi kuonyesha kwa vitendo maana halisi ya uwajibikaji na ikampa heshima sana, japo kwenye KATIBA MPYA anatukera mno, sasa mtihani unahamia kwa Mwinyi mdogo na tutaangalia sana kwa ataendeleza KIBURI NA JEURI ile ile tulioizoea CCM au atatii historia iliowekwa na baba yake???
 
UYU waziri wa ulinzi ni ovyo kabisa anasubiri tume itoe majibu mbona tume ya mbagala hamjatuambia ilichogundua, shame on u!!!
Apishe tume itakayochunguza ifanye kazi yake kwa uwazi,asikae hapo na kuvuruga uchunguzi!!
 
Baba yake ndiye MSTAAARABU wa kwanza nchi kuonyesha kwa vitendo maana halisi ya uwajibikaji na ikampa heshima sana, japo kwenye KATIBA MPYA anatukera mno, sasa mtihani unahamia kwa Mwinyi mdogo na tutaangalia sana kwa ataendeleza KIBURI NA JEURI ile ile tulioizoea CCM au atatii historia iliowekwa na baba yake???

Precisely!ndiyo maana watanzania walimheshimu sana na kumpa urais!!
 
Apishe tume itakayochunguza ifanye kazi yake kwa uwazi,asikae hapo na kuvuruga uchunguzi!!
Tume ya nini tena!!!!! Ya Mbagala ipo wapi??? Inatakiwa wote waachie ngazi, ikiwezekana hata JK....
 
may be that is your next pezda...na bado mtakoma tu hadi mpate adabu ili mara ya pili msije kuchagua ccm tena...
 
Kaazi kweli! Nchi hii ni rahisi sana kuiongoza maan wananchi wake ni wapole, wakarimu nk. Tunaonyesha kukerwa na uwajibikaji wa viongozi wetu lakini kwa sababu ya upole tunaishia kusema " aaah Mungu anajuwa bwana!" Tunaendelea kuumia tuu.
Hizo tume hazileti chochote maana zinateuliwa na haohao waliowaweka sasa unategemea nini? Tume zooooote za hapa kwetu huwa si huru kabisa, zinajengwa na dhana ya kulindana.
Cha kujiuliza ni kwamba hivi ni tume gani iliyowahi kuundwa na kutoa ukweli? (Ukiondoa tume ya Richmond)
Tutabaki kuumia tuu. Hata wale wanaodhani suluhisho ni 2015 wasahau. Kura zitachakachuliwa na itaundwa tume ya kuchunguza.
Kutokana na uoga na unafiki tuliokuwa nao ya egypt hatuyawezi. Yaani pamoja na matatizo na mapungufu ya serikali yetu kuna mijitu bado inadhani tuko kwenye kampeni! Tutakufa bila kelele. Yaani huwa nakasirika sana!

ya richmond ni KAMAT si TUME
 
Huwa nikifika hapa natamani kupindua nchi tuanze upya, yani kiongozi anaweza kukwepa uwajibikaji basi hata kuonyesha sympathy? Huyu hafai, naomba CHADEMA waendelee kugandamizia azimio la kujiuzulu kwa MWINYI na MAMUNYANGE kwani naamini kabisa wanajua yaliyo chini ya kapeti bali wanataka kutufanya sisi wajinga hapa.
Mapinduzi lazima kwa maendeleo ya Taifa hili.:A S 20:
 
Mwinyi: Kujiuzulu kunatoka na makosa yaliyofanywa na mamlaka iliyoko chini ya mtu kama itadhihirika. Tusubiri tume itakayoundwa na tupate matokeo yake kwanza.

Shame on him,kwani mwaka1972 wakati baba yake anjiuzuru alisubiri tume ? Ona jisi mijitu mingine ilivyokuwa mibinafsi,kama linashindwa kujifunza toka kwa baba yake mzazi litajifunza kutoka kwa nani ?
 
Kama yeye Mwinyi na Mwamnyange hawataki kujiuzuru, JK anatakiwa awe bold na kuwafukuza kazi leo hii na wala siyo kesho
I wish this could be possible. Mkwere huo ubavu hana, hadithi za rejea zinaonyesha kuwa Mzee Mwinyi ndiye aliyeenda kumuokota JK huko kusini (sikumbuki ilikuwa Mtwara au Lindi alikokuwa katibu wa ccm) na kuja mpa ubunge na unaibu Uwaziri, ambavyo baadae vilimfikisha hapa alipo. Kwa kuwa Tanzania hatufanyi mambo mengi kwa ujuzi tulio nao, ila ni kwa kujuana, hawezi kumfukuza kazi. Ingekuwa rahisi kwake kuridhia kujiuzulu lakini sio kumfukuza kazi. Vilevile kwa mkwere itakuwa rahisi kuridhia msamaha wa kutokulipa deni endapo atapewa ofa ofa hiyo na RA lakini sio kutumia sheria zilizopo! Hapa imekula kwetu. Labda kitakacholeta mabadiliko na hawa waondoke, ni sisi wananchi kushinikiza, yaani nguvu ya umma.
 
Hatujui!! Mzee Mwinyi alijiuzulu enzi zile kwa sababu alikuwa chini ya utawala makini usiovumilia ujinga! Hilo alilijua na alilijua vizuri sana. Huyu Mwinyi Junior hawezi kujiuzulu kwa sababu aina ya utawala uliopo ni utawala tofauti sana. Kama unajua mambo yanavyoendeshwa chini ya utawala huu utasema hata kina Edo na washikaji zake Kina Msabaha na Kina karamagi walijiuzulu kwa sababu tu ya Jazba za Edo! Vinginevyo hata wasingejiuzulu maisha yangeendelea.

Lakini logic ya kujiuzulu iko wazi. Mabomu yamelipuka na watu wamekufa na mali zimeharibika. Mabomu hayo hayanunuliwi ili hatimaye yawalipukie watu walioyanunua kwa fedha zao wenyewe. Wenye dhamana ya kuhakikisha kuwa hayalipuki wameshindwa kufanya kazi yao. Suala si tume kusema kuwa aliyehusika ni fulani na fulani, suala ni kuwa mfumo mzima, ambao Mwinyi Jr ndo msimamizi wake, umeshindwa kuzuia jambo hilo kutokea. Mwinyi Jr. yuko 'accountable' kwa matokeo ya walio chini yake. Hana la kujitetea!

Isipokuwa katika hali ya uongozi mbofu mbofu iliyopo, mambo ya busara huwa inaonekana kama ni hovyo. Ndo maana tunasema mfumo uliopo (yaani CCM nzima) ni vigumu kwa mtu anayetumia busara kuendelea kuwemo. Ni vigumu kwa sababu kuna wakati unalazimika kutetea mambo ambayo unaona yamekaa upogo upogo ila unalazimika kusema yamenyooka. Sasa ikiwa hali ndo hiyo, huwezi kuwa mtu mwenye busara asilani.

Fikiria kwenye sakata lile la Mbagala kama jamaa angekuwa alijiuzulu, bila shaka chain ingeshuka chini zaidi. Hao wengine watakao kuja hakuna mtu ambaye angekubali kuweka rehani kazi yake kwa sababu ya uzembe wa walio chini yake, hivyo wangefanya kazi kwa umakini zaidi na Gongo la Mboto ingeepukika. Gongo la Mboto imetokea kwa sababu mbagala ilitokea na hatukufanya chochote. Hata Gongo la Mboto hatutafanya chochote, yatatokea mengine. Tutaishia kulaumu kuwa utawala una bahati Mbaya. Hii ndo Tanzania tulipofikia.

Tutaenda kwa kudra tu hadi lini? Rais jana alisikika akisema " aaa imeshatokea!!". Jambo hili bila shaka linaashiria ile akili mgando ya 'ajali haina kinga' ambayo wengi imetuandama. Bila shaka hata mijadala inayoendelea humu huoni depth ya kile watu wanachokiongea ndo maana hata hawa wanaopelekewa tuhuma wanadharau tu.

Ajali na matukio kama haya, mara nyingi huwa ni 'eye opener'. Ni kitu kinachowaonesha jinsi hali ilivyo mbaya katika mfumo wa uendeshaji wa nchi. Hatua tunazochukua zinazidi kuonesha jinsi tulivyo serious au tusivyo! Kwa kauli za rais jana inaonesha kabisa jinsi tusivyo 'serious' na kuwa mambo yetu yanaenda kibahati bahati. Ikiwa hali ndo hivyo, tutarajie lolote wakati wowote! Ila tusijitoe kuwa hatuhusiki. Wote tunahusika! Binadamu mnapoamua kujiendesha kizembe zembe kama ng'ombe mjue yale yanayowapata ng'ombe yanaweza kuwapata ninyi vile vile.

Ajali zote husababishwa na UZEMBE. Hapa uzembe umefanyika. Tulitarajia waziri awajibike kwa kutambua hilo. Kutowajibika ni kuwa waziri anasubiri aambiwe kama ni UZEMBE ndo afikirie cha kufanya! Hawezi kuwa waziri makini kamwe!
 
Back
Top Bottom