Maboga yanaweza kuzuia magonjwa yanayotokana na kuvu au Fungus

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
boga.jpg

Kwa muda mrefu maboga yamekuwa yanajulikana kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutumika kama dawa, vilevile chakula hicho kina protini yenye nguvu ambayo inaweza kupambana na magonjwa mbalimbali yanayotokana na kuvu au fungus.

Maboga yamekuwa yakitumika sana katika tiba za kiasili katika kutibu magonjwa tofauti kama vile kisukari, shinikizo la damu, kiasi kikubwa cha mafuta mwilini pamoja na saratani katika nchi kama vile China, Korea, India, Yugoslavia, Argentina, Mexico, Brazil na kwingineko.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Vyakula, imeonyeshwa kuwa protini inayotokana na boga iitwayo Pr-2, inapambana vilivyo na ugonjwa unaosababishwa kuvu au fungus wa sehemu za uke (Vaginal yeast infection). Vilevile michubuko inavyotokana na mkojo au nepi (diaper rashes) pamoja na matatizo mengine ya kiafya.

Protini hiyo ya Pr-2 iliyoko kwenye maboga halikadhalika inazuia aina 10 za fungus au kuvu ikiwemo aina hatari ya fungus wajulikanao kama Candida Albicans. Fungus hao ni maarufu kwa kusababisha matatizo kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari na kupelekea kupata fungus midomoni, katika ngozi, chini ya kucha pamoja na katika mfumo mzima wa mwili.

Wataalamu wana matumaini kuwa, protini hiyo inayopatikana kwenye maboga inaweza kupelekea mafanikio ya kutengezezwa tiba asilia ya kupambana na magonjwa ya kuvu au fungus.

Haya kama ulikuwa unadharau kula maboga, nafikiri inakubidi ufikirie tena!
 
Back
Top Bottom