Mabina: Sipingi ushindi wa Diallo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Sunday
October 28, 2012


HABARI
Posted Sunday, October 28 2012 at 10:34


Na Frederick Katulanda, Mwanza


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza Clement Mabina, amefuta uamuzi wake wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa chama hicho ambayo yalimpa ushindi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Anthon Diallo.

Mabina ambaye alitangaza kupinga matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kuwa haukuwa huru na haki na kwamba ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, alieleza maamuzi yake mapya jana ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka Dar es salaam alikodaiwa kwenda kuwasilisha rufaa yake.

Alisema ameamua kuachana na uamuzi wake wa kupinga matokeo hayo kwa ajili ya kukinusuru chama na mpasuko, lakini aliendelea kusimamia msimamo wake kuwa pamoja na kufuta uamuzi wake huo ni kuwa uchaguzi huo uliomuingiza Diallo kushinda haukuwa haki na ulitawaliwa na rushwa.

"Nimeamua kuachana na rufaa yangu sasa naangalia mambo mengine.., najua kwamba hali hii inaweza kusababisha mpasuko ndani ya chama, hivyo nimeamua kuachana na uamuzi wangu wa kukata rufaa lakini zaidi kuheshimu pia uchaguzi wa wapiga kura ambao nina hakika uliathiriwa na rushwa," alieleza Mabina.

Katika uchaguzi huo, Mabina aliangushwa na Diallo kwa tofauti kubwa ya kura baada ya kushinda kura 611 dhidi ya kura 328, lakini alipinga matokeo hayo akidai kuwa uchaguzi huo ulitawalia na vitendo vya rushwa.

Akitoa tuhuma hizo baada ya kupewa nafasi ya kushukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CCM mkoani Mwanza, alidai kwamba ameamua kukata rufaa katika Kamati Kuu ya CCM, kupinga matokeo hayo.

Alisema kwamba licha ya hali hiyo yeye ataendelea kubaki mwanachama mtiifu ndani ya CCM na kusema anamuachia mungu zaidi ya hayo alitangaza kuwa atakuwa tayari kushirikiana na wanachama wenzake kupitia ngazi mbalimbali za uongozi wa Chama kukijenga chama chake.

= === == == = = == = = = =









 
Na ndivyo itakavyokuja kuwa kwa UMVCCM na wengine wote wanaopinga matokeo ya UVCCM yaliyogubikwa na malalamiko lukuki.
 
Mabina mzee wa madili nakumbuka ashawahi tapeli mtu gari imejaa vifaa vya majumbani kutoka nje lakini leo hii ni kiongozi ndani ya chama tawala inasikitisha kwakweli
 
Sijui ni kwa nini anaeshidwa ndo anaiona rushwa mbaya!! Ukweli hawa wagombea wote tena wa ngazi zote bila kubagua huyu kashinda au kashindwa WALITUMIA RUSHWA sema leo kashindwa yeye ndo imekuwa rushwa ilitawala.
Ukweli wanasiasa wengi kama sio wote ni wanafiki kwenye hili swala la rushwa, HAKUNA MSAFI.
 
wanajua kuwa wanapinga mfumo ambao ndiio huo huo uliowaingiza hata wao madarakani. Bora agundua hilo awasaidie na akina Sumaye na UMVCCM kujua kuwa rushwa ni mfumo halali ndani ya CCM na ukizidiwa dau jipange next time
 
Back
Top Bottom